Jamaa kagundua kua hata uchaguzi ukiitishwa Chadema watasusia atapita bila kupingwa.
Tubadili katiba, kama mtu anataka kuhama chama ahame bila kutuingiza kwenye hasara za uchaguzi.
Nchi hii bado masikini, vipaumbele ni vingi sana, pesa iende kwenye mambo ya msingi na sio kila siku ni uchaguzi.
By t way kuna majimbo zaidi ya 150 ya yanayoongozwa na ccm toka 2015, wabunge wake wanaunga mkono CCM since then, sioni tofauti yake ya maisha na majimbo yasiyo ya CCM. Kuunga mkono au kutounga sijaona tofauti.
Tufanye wabunge wote wa upinzani waunge mkono jitihada za rais, je itabadili hali yetu ya maisha na kua mazuri zaidi, Tanzania itaanza kutiririka maziwa na asali? Kwamba kutokuunga mkono ndio kunazuia hayo?
Mwalimu alipambana na matatizo kama ujinga, maradhi, nk lakini hili la ujinga bado ni tatizo. Mtu anasema akiunga mkono analeta maendeleo, mbona maendeleo hayapo kwenye wabunge ambao ni wa ccm toka 2015?