Wapinzani wameshaishiwa sera. Mbona hata kwenye mikutano yao hawaelezi namna watakavyoedeleza pale wenzao walipofikia? Hawasemi wanatarajia kujenga barabara ngapi, Mashule mangapi, Hospital ngapi, wataborashaje maisha ya mtu wa chini kama mkulima, nini kipaumbele chao wakipata madaraka, watanuifashaje mtanzania kutokana na rasilimali za nchi, je mikakati yao ya maendeleo ikoje kodi wanazolalamikia kuwa hazikusanywi watatumia mbinu gani mbadala kuzikusanya (maana wanapinga mfumo wa EFD na kusapoti wafanyabiashara kugomea kulipa kodi) je nchi wataiendesha kwa mgawanyo upi wa mapato na matumizi, yale wanayowakataza wananchi wasichangie (eg maabara) watapataje kuendeleza mashule n.k, Haya hawayaelezi! Kila kukicha ni Escrow! Well, hili tumeshalisikia, so what is the way forwad? Mi ninaona hawana sera zaidi ya kulala na kuamka wakitafuta kashfa bila plan ya kumuendeleza mtanzania, kifupi upinzani umefeli, wanatumia matatizo madogomadogo ya watanzania kama mtaji wa kuingia ikulu bila plan za maendeleo.