Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Baraza la madiwani Halmashauri ya Misungwi limesema halijawahi kutoa kauli ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hawakuunga mkono uamuzi wa Rais Dkt. John Magufuli kumfuta kazi aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga.
Taarifa ya baraza hilo baada ya kikao imesema kwamba ''Sii kweli kwamba kuna tamko lolote tulitoa kuhusu kufukuzwa Waziri Kitwanga na wala hatuna uwezo huo, taarifa hizo zibezwe na kupuuzwa.''
Madiwani hao wamesema wanaungana mkono na kauli ya Rais Dkt. John Magufuli kuhusu hapa kazi tu hivyo uamuzi wake alioufanya hawawezi kupingana nao.
Aidha baraza hilo limesema kama kuna mtu alitoa kauli kwa niaba ya baraza hilo siyo sahihi kwani baraza hilo hutoa taarifa zinazohusu mambo yao kwa kutumia vikao maalumu.