Nakiri sina takwimu, lakini kutokana na matukio ya ulipuaji wa mabomu ya machozi dhidi ya wananchi un aofanywa na Polisi wa FFU, ni dhahiri awamu hii ya JK idadi ya mabomu ya machozi yaliyolipuliwa ni mengi kuliko jumla idadi ya yale yaliyolipuliwa katika awamu zote tatu zilizotangulia.
Siku hizi haipiti wiki bila kusikia mahala fulani FFU wameshalipua, mara dhidi ya wamachinga, ugomvi wa wakulima na wafanyabiashara, wafuasi wa vyama vya upinzani, wanafunzi wa vyuo, wakina mama wauza pombe nk.
Na tunapozungumzia awamu ya Mwl Nyerere, kwa wanaokumbuka tuambieni ni matukio mangapi mabomu ya machozi yalilipuliwa dhidi ya wananchi. Mini nadhani mabomu ya machozi hayakuwahi kutumika wakati wa awamu, lakini pengine yalitumika.