Mapungufu makubwa ya Serikali ya awamu ya nne

Mapungufu makubwa ya Serikali ya awamu ya nne

ccm hawastaili kuendelea kutawala vinginevyo hali itakuwa mbaya zaidi
 
Mambo aliyofanya JK kwa maendeleo ya nchi ni makubwa sana wala hayaelezeki wala hayapimiki ni zaidi ya maendeleo.
 
Kwa lugha nyepesi nyepesi, serikali haikuwa na kipaumbele,ilikuwa inataka kote kote kufanya vizuri matokeo yake tumebaki pale pale ilipotukuta wakati inaingia madarakani.
 
Huna hoja katunge uongo mwingine huu umekwama bavicha wenzako pamoja na mambo mengine wanauwezo angalau wa kulea watoto wewe sijui unaweza nini.
mkuu kwani kakwambia ni bavicha?
 
ccm hawastaili kuendelea kutawala vinginevyo hali itakuwa mbaya zaidi
Watanzania karibia wote wanahitaji ccm iendelee kutawala ila wajinga wachache kama wewe ndiyo wanazungumza utumbo huu.
 
thibitisha kauli yako?
Mambo mengi tu hii ni kwa uchache tu.
View attachment 219333 image.jpg
 
Kwa lugha nyepesi nyepesi, serikali haikuwa na kipaumbele,ilikuwa inataka kote kote kufanya vizuri matokeo yake tumebaki pale pale ilipotukuta wakati inaingia madarakani.
Utakuwa unaumwa siyo bure ona hapa.
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    9 KB · Views: 194

usituoneshe picha ambazo mnatumia kuwahadaa watanzania tuambie hizi ahadi
Baadhi ya ahadi za Rais:
1. Kununua meli mpya Ziwa Victoria
2. Kujenga reli mpya Kati kutoka Dar Salaam kwenda bara
3. Kumaliza migogoro ya ardhi
4. Kutokomeza ugonjwa wa malaria 2015
5. Kumaliza matatizo ya walimu
6. Kununua bajaji 400 za kubebea wagonjwa
 
Mafanikio ya jk ya yanawaumiza wengi kaweza kathubutu na sasa anasonga mbele.
 
usituoneshe picha ambazo mnatumia kuwahadaa watanzania tuambie hizi ahadi
Baadhi ya ahadi za Rais:
1. Kununua meli mpya Ziwa Victoria
2. Kujenga reli mpya Kati kutoka Dar Salaam kwenda bara
3. Kumaliza migogoro ya ardhi
4. Kutokomeza ugonjwa wa malaria 2015
5. Kumaliza matatizo ya walimu
6. Kununua bajaji 400 za kubebea wagonjwa
Mengi yamekamilika machache yapo hatua za mwisho kukamilika.
 
Wanajamvi it it hightime tujadili mapungufu ya serikali iloyopo madarakani ili hawa wanaojipitisha kutaka urais, watupe sera zao zitakuwaje: mimi niliyoyaona ni yafuatayo
1. Elimu imeendelea kushuka ubora
2. Maslahi ya wafanyakazi hayakujaliwa ili waongezeg tija.
3. Suala la afya kwa jamii halikupewa kipaumbele
4. Vijana wengi hawana ajira
5. Rushwa imekithiri kila maeneo mpaka inaonekana ni jambo la kawaida.
6. Muungano umetetereka kwa kuruhusu zanzibar izidi kufanya mambo yao
7. Heshima ya tanzania imepungua sana nje rais amekuwa ombaomba sana.
8. Usalama wa wanainchi umezidi kuwa shakani kuibuka kwa mabomu kila kona ya tanzania
9. Nchi yetu kuanza kumegwa huku tunatizama eg lake nyasa.
10. Kushidwa kuyaboresha makampuni yaliyochini ya serikali eg ATCL serikali haijatoa mtaji wala kununua ndege hata moja.
etc etc etc............wana jamvi kazi kwenu!!
Kuhusu namba moja, sijui umetumia kigezo gani kusema kuwa elimu imeshuka. Binafsi napingana na wewe kwa hilo kwani kwa sasa idadi ya wanaohitimu shule ya msingi na sekondari imeongezeka. Shule za sekondari zimejengwa mpaka kwenye kata na sasa wanaendelea kujenga maabara kwa kila shule za sekondari. Yapo mengi ya kueleza
 
Mengi yamekamilika machache yapo hatua za mwisho kukamilika.

Huyu amekuuliza maswali, umejibu nini katika haya?

quote_icon.png
By jme

usituoneshe picha ambazo mnatumia kuwahadaa watanzania tuambie hizi ahadi
Baadhi ya ahadi za Rais:
1. Kununua meli mpya Ziwa Victoria
2. Kujenga reli mpya Kati kutoka Dar Salaam kwenda bara
3. Kumaliza migogoro ya ardhi
4. Kutokomeza ugonjwa wa malaria 2015
5. Kumaliza matatizo ya walimu
6. Kununua bajaji 400 za kubebea wagonjwa
 
thibitisha kauli yako?
MAZURI ya Kikwete ambayo hayajawahi kufanywa na marais waliomtangulia HAYA HAPA
Katika kipindi cha Kikwete masuala yafuatayo lazima tumpe Credit kwani baadhi yamefanywa na JK wa mwanzo tu na hayakufanywa na Mwinyi wala Mkapa.

1. Ujenzi wa Sekondari za Kata ni maamuzi sahihi ingawa yana changamoto zake zinazoweza kutatuliwa na watakaomfuatia, lakini hapa JK ametumia madaraka yake vizuri

2. Ameendelea na uendelezaji wa Miradi ya Barabara, suala lililoanza kujitokea wakati wa awamu ya 3, JK ameendelea nalo suala hilo kwa kasi kubwa na kwa kipindi chote

3. Daraja Kigamboni, Malagarasi na Kilombero ni miongoni mwa mambo yatakayokumbukwa forever

4. Ongezeko la Taasisi za Elimu ya Juu limefanyika vizuri sana katika awamu ya Kikwete, mbali na UDOM lakini taasisi na vyuo vingi vimeimarishwa, kupandishwa hadhi na vyuo vingi binafsi vimeanziswa. Kwa sasa Taifa haliko tena na dhana ya UDII, Mzumbe na SUA. Aidha ari na moyo wa watanzania kulipia huduma za elimu umeongezeka.

5. Kumekuwa na ongezeko kubwa la ajira ukilinganisha na awamu mbili zilizomtangulia. Mkapa aliendesha Serikali nyembamba, suala ambalo ni zuri lakini lina changamoto zake kwa wale waliokuwepo wameliona hata akapewa sifa ya mzee wa "ukapa"

6. Mradi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara kwa lengo la kutatua kero ya Umeme ni hatua nzuri ambayo haijawahi kufanywa katika awamu ya 2 na ya Tatu (Vyanzo vya Nishati)

7. Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Chuma (Kule Liganga?) ambao maandalizi ya ujenzi wake yamekamilika ni hatua nzuri ili kuvutia au kuanzisha uwekezaji wa zana za Chuma pamoja na Viwanda vikubwa.

8. Hatua ya Kujenga Bandari mpya eneo la Bagamoyo yenye hadhi ya 4th Generation ni tukio litakalokumbukwa na vizazi Dahri vijavyo.

9. Hatua ya Utekelezaji wa mradi wa DRT ambao ulikuwepo miaka mingi pia ni miongoni mwa mazuri yaliyotendeka katika awamu ya JK

10. Zoezi la kutambua na kuwarudisha kwao wahamiaji haramu pia ni zoezi zuri ambalo bila shaka halijawahi kufanywa katika uongozi wa awamu nyinginezo kwa kiwango na utashi wa namna hiyo

11. Kitendo cha utekelezaji wa mradi wa vitambulisho vya Taifa ni credit kubwa kwa JK ambao hakuna sababu za wazi kwanini nchi imekaa miaka 50 pasipo na vitambulisho vya uraia kwa wakazi wake na raia wake

12. Ameendelea kuiweka Tanzania kwenye mahusiano mazuri kimataifa hususan SADC, UN na nyanja nyingine za Kitaifa. Ukiacha EAC ambayo sababu za kuzorota kwake ziko wazi, lakini maeneo mengine ame-play well.
picha; maendeleo ya ujenzi wa daraja la kigamboni eneo la kurasini jijini dsm. ujenzi ulikuwa asilimia 47
 
Kuhusu namba moja, sijui umetumia kigezo gani kusema kuwa elimu imeshuka. Binafsi napingana na wewe kwa hilo kwani kwa sasa idadi ya wanaohitimu shule ya msingi na sekondari imeongezeka. Shule za sekondari zimejengwa mpaka kwenye kata na sasa wanaendelea kujenga maabara kwa kila shule za sekondari. Yapo mengi ya kueleza

Kigezo cha kwanza nipale wanafunzi takribani 70% walipata zero

Kigezo cha pili nikupanuwa goli, div - zero imegeuzwa div-V

Kigezo cha tatu nikushuka nakutoweka kabisa kwenye ubora shule maaruf za serikali

-Mzumbe

-Kilakala

-Ilboru

-Iyunga

-Tanga school

nk
 
Nakubaliana na wewe Mkuu. Serikali ya JK imefanya mambo mengi makubwa

ukienda MuHIMBILI hospita

-Madawa hakuna

-Madakitari wapo hoi, maisha magum

-Vitendea kazi hakuna

-Majengo yamechaa hovyo

-Bila ndugu huapati walau paracetamo

Sasaa hivi wenye uwezo wao wamegeuza India kama ndiyo muhimbili, maskini wakijifia hovyo.
 
Kuhusu namba moja, sijui umetumia kigezo gani kusema kuwa elimu imeshuka. Binafsi napingana na wewe kwa hilo kwani kwa sasa idadi ya wanaohitimu shule ya msingi na sekondari imeongezeka. Shule za sekondari zimejengwa mpaka kwenye kata na sasa wanaendelea kujenga maabara kwa kila shule za sekondari. Yapo mengi ya kueleza

Ww mpuzi kweli shule za kata zina towa elimu gani ikwa shule nzima Ina walimu 3 mpaka 2 tu sasa hapo kuna elimu gani msipende kuleta udugun wa kijinga
 
Back
Top Bottom