Maprofesa "wajamaa" wa vyuo vikuu huu ni wakati wa kumsaidia rais.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Rais George Bush alipofanya ziara ya kwanza enzi za awamu ya nne, kulikuwa na kundi kubwa la wanaharakati wakiwemo maprofesa maarufu wa vyuo vikuu, ambao walijitokeza hadharani na kupinga lengo zima la ziara ile.

Vyombo vya habari vikawaonyesha wakiwa kwenye maandamano hayo. Kama kawaida katika ile mida ya jioni kwenye vipindi vya runinga vya mahojiano, maprofesa maarufu wakajenga hoja nyingi na nzito za kuipinga ziara ya George Bush.

Leo Rais JPM ni kama vile anakifanya kile kilichokuwa ndani ya mioyo yao kwa wakati ule, anasisitizia katika kujenga nchi mpaka iwe na uwezo wa kuwa "donor country", na wote tunatambua kuwa nchi inayofadhili nchi nyingine inakuwa na kiburi kikubwa. Inawezekana awamu hii inaongozwa na dhana za kutaka kujitawala, kwa maana ya kutotaka kuwa bendera hufuata upepo.

Nadhani huu ni wakati muafaka kwa maprofesa wale walioipinga ziara ya George Bush kuingia kazini katika kutumia kuelimika kwao katika kutoa mawazo mbadala kwa uongozi wa awamu ya tano ili wazo lao la kujitegemea, ambalo msingi wake na unaanzia awamu ya kwanza, liweze kuwekwa katika uhalisia wa maisha yetu.

Siasa za harakati zilizofanywa na maprofesa wakati wa ziara ya Bush, kwa sasa zimepata kiongozi anayeziunga mkono kivitendo. Ni jukumu la maprofesa wetu kuja na fikra ambazo zitajenga ushawishi wa sisi wenyewe kuweza kujitegemea.

Maprofesa walitumia nguvu nyingi katika kupinga udhalimu wa George Bush, wanayo nafasi na kila sababu ya kuonyesha ni kwanini walikuwa sahihi kufanya vile, kupitia constructive ideas zitakazoelekezwa kwa rais wa sasa na wasaidizi wake, katika mfumo wa ushauri au katika mtindo wa zile hoja zao wakati wanahojiwa na watangazaji wa vituo vya runinga.

Huu ni wasaa muafaka kwa wananchi hii kwa wananchi wengi wa nchi kuyasikia mawazo mapya na ya kimaendeleo kutoka kwa maprofesa wetu.
 
Kwa hiyo walisema wanampinga Bush ila wanaunga mkono unyau na ushetani uliofanyikaZanzibar,sio?
 
Huyu jamaa amejiunga JF 29 December 2015 kwa lengo moja tu, la kumtetea JPM msukuma mwenzake kwa kila japo whether la hovyo au la sawa!
 
Kwa hiyo walisema wanampinga Bush ila wanaunga mkono unyau na ushetani uliofanyikaZanzibar,sio?
Unaelewa maana ya neno ushetani?, nenda kwa mchungaji wako halafu muombe kikao cha faragha atakuelezea maana pana ya neno ushetani.
 
Hata sisi Upinzani tunaunga mkono

wazo la Kujitegemea! Lakini hatuungi

mkono mchakato wa utekelezaji wazo

Hilo!

Kilichotokea Ni kwamba Jamaa wame

Tutosa Na sisi Kwa kujifariji tunajidai

Hatutaki msaada!

Hivi Kweli sisi ambao bado tunahanga

Ika Na malaria Na HIV/AIDS tunauthub

utu wa kuyatamka hayo tuyatamkayo?

Ifike Wakati tuwe wakweli tu tunapoko

sea!
 
Hata sisi Upinzani tunaunga mkono

wazo la Kujitegemea! Lakini hatuungi

mkono mchakato wa utekelezaji wazo

Hilo!

Kilichotokea Ni kwamba Jamaa wame

Tutosa Na sisi Kwa kujifariji tunajidai

Hatutaki msaada!

Hivi Kweli sisi ambao bado tunahanga

Ika Na malaria Na HIV/AIDS tunauthub

utu wa kuyatamka hayo tuyatamkayo?

Ifike Wakati tuwe wakweli tu tunapoko

sea!
Nimekusoma mkuu, lakini kumbuka kuwa tunazalisha nguvu kazi kubwa kila mwaka, hii issue ya MCC ilikuwa inasubiri wakati, ingewezekana fedha ikasitishwa kuletwa hata mwakani au baada ya miaka mitano ijayo, lakini ipo siku nchi yetu ni lazima iongozwe na akili za kujitegemea. Ni aibu kwenda nje ya nchi unatangaza njaa kwa wazungu wakati kuna wapuuzi humu nchini wanajenga maghorofa kwa sababu ya mishahara hewa. Magufuli angeweza kutoshinda urais mwaka jana lakini wazo la kupambana na mishahara hewa lingekuja kuwasilishwa kwa jamii na mtu mwingine ambaye mimi na wewe wala hatumjui.
Ukweli usiposemwa leo basi tambua kuwa hata mwakani siku kama ya leo utakuja kusemwa.
 
Uko sahihi Kabisa Mkuu, tunajenga nyumba moja, hatuna haja ya kugombania fito! Ila kinachoumiza hapa Ni Sababu zilizopelekea kukosa FUNGU Hilo,

Kwa mfano; Jamaa wangesema tunawanyima FUNGU kwa sababu tumeshawasaidia sana Sasa Ni Muda wenu Na nyinyi msimame muwasaidie wadogo zenu! Tungesema sawa Na hata hivyo tunashukuru sana Kwa hapa mlipotufikisha kwakweli hatuna cha kuwarudishia ili kufidia Wema wenu kwetu, Mungu awape Maisha marefu Na ya amani hapa duniani.

Yaani amini nakwambia hili suala halitopita bila Madhara ya ki'diplomasia..
 
Hiki ni kipindi ambacho rais Magufuli ataigundua tofauti kubwa iliyopo kati ya waziri na rais. Ni kipindi kitakachomkomaza kiuongozi, ingawa lengo lake la kujitegemea daima halikwepeki.
Hao hao wamarekani wanaotupatia fedha za MCC ikawasikiliza wanazuoni wao utagundua kuwa wanafurahi sana pale ambapo kile kinachouzwa nje kinakuwa ni kikubwa kuliko kile kinachoingizwa nchini mwao.
Hilo ni somo kwetu pia, kwanini tuwe tegemezi milele?, kuna faida gani nchi ibarikiwe rasilimali halafu wananchi wake wawe maarufu kwa kuombaomba, tena kutoka kwa watu ambao nchi zao hazina wingi wa rasilimali kama huu tulionao?.
 
Unamaanisha kilichotokea Zanzibar hata shetani mwenyewe anashangaa?
Unayatazama mambo katika jicho la kisiasa, tambua kuwa mwanaccm wa leo anaweza kuwa mwanachadema wa kesho. na mwanacuf wa leo anaweza kuwa mwanaact wa kesho. Unayapima mambo kwa kutumia mizania ya kisiasa, anza kujivua akili za uchama na siasa za lawama, wengi wanapoteza muelekeo kwa sababu ya kuwa watu wanaofanana na wewe kimtazamo.
 
Ni kweli naamini katika siasa maana ndo inayotuendesha kila siku na hata haya yote ya MCC ni matokeo ya maamuzi ya wanasiasa wachache wanaoamini katika kuwa madarakani kwa kibaraka wao mmoja na kuwacha watanzania 45 vijijini wakibaki na maguzo ya umeme bila umeme.
 
Kwa hiyo walisema wanampinga Bush ila wanaunga mkono unyau na ushetani uliofanyikaZanzibar,sio?
Suala la Zanzibar ni suala lisilokuwa la kudumu kwa maana ya uchaguzi mkuu kufanyika, kumalizika na maisha kuendelea (licha ya uwepo wa malalamiko), maprofesa walioshiriki maandamano wanatofautiana kimtazamo na sera za kibeberu, rais anapozungumzia sisi kuja kuwa donor country anamaanisha kuanza kujitegemea kwa uwezo wetu wote. Usiishi kwa kutafuta uhalali unaotegemea matukio ya muda mfupi.
 
Back
Top Bottom