Maprofesa wa Tanzania,hawafundishi lakini wanataka waendelee kuitwa maprofesa

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,897
19,080
Wasomi wa Tanzania wako obsessive sana na Uprofesa.

Profesa ni cheo kinachotokana na kazi ya mtu na sio sifa ya kitaaluma, hakuna mtu anasoma kua profesa, kiwango cha elimu cha juu duniani ni udaktari wa falsafa.

Uprofesa ni cheo cha kufundisha chuoni lakini cha ajabu hapa Tanzania mtu hafundishi anataka aendelee kuitwa profesa nje ya maisha ya kufundisha, mfano Muhongo, Maghembe, Ndalichako na wengine, hawako chuoni lakini bado wanataka waitwe maprofesa.

Dr Rice aliekua waziri wa mambo ya nje wa marekani ni profesa lakini alikua hatumii uprofesa maana alikua hafundishi, Dr Ahmenijad rais wa zaman wa Iran alikua prof kabla hajawa rais ha hakutumia jina la prof hadi pale alipomaliza urais akarudi kufundisha, Dr Abu Bakar Al Bagdadi mkuu wa ISIS ni profesa ila hajiiti prof maana hafundishi chuoni anafundisha mambo mengine, nimetaja kwa uchache

Nimebahatika kukutana na wazungu wengi waliokua maprof kabla hawajaacha kufundisha na kupractise profession zao hawajiiti prof tena,wanatumia doktas lakiini cha ajabu Tanzania mtu hafundishi karbu miaka 40 30 kama Lipumba bado wanataka waitwe prof.

Tanzania vyeo vya uprofesa ni kama vyeo vya kijeshi maana kanali hata akistaafu ataendelea kuitwa kanali mstaafu, basi na wao waitwe profesa mstaafu.

wasomi wa Tanzania wana shida gani na Uprofesa?
 
Unaujua mfumo wa utoaji uprofesa nchi hii?
Ni kweli Maprofessa wanatakiwa kufundisha zaidi kuliko kufanya research, wakati junior to senior lecturer wanatakiwa kufanya research zaidi kuliko kufundisha.
 
Unaujua mfumo wa utoaji uprofesa nchi hii?
Ni kweli Maprofessa wanatakiwa kufundisha zaidi kuliko kufanya research, wakati junior to senior lecturer wanatakiwa kufanya research zaidi kuliko kufundisha.
ukoje ? mtoa mada ameeleza vizuri tu , sasa ww kama unaelewa tofauti na hivyo tuambie
 
Maprofesa wa bongo ni kama nkurunzinza... Mimi sijaelewa huyu Maghembe na Lipumba wanapata muda wa kufundisha kweli?
Sasa why bado tuendelee kuwaita maprofesa?
 
je professor maji marefu naye anachukua nafasi gani hapa wadau?
Hapa tunazungumzia real professors na sio wanaojiita professor kama jina la kisanii! Yupo professor maji marefu, professor J. nk . Nadhani hii ni mada serious na hasa kwa waandishi wa habari ambao mara nyingi huandika habari za hawa watu na kuwa-address kama Professor Maghembe, Prof. Muhongo. The next document is from www.formsofaddress.info/Doctorate.html
upload_2016-3-28_13-27-12.png
 
je professor maji marefu naye anachukua nafasi gani hapa wadau?

Huyu ni profesa wa kutoa majini na mazongo. Namkumbuka miaka ile ya 80 na mwanzoni mwa 90.

Ametufilisi sana sisi wasambaa kwa yale maigizo yake ya kutoa majini. Watu waliuza ng'ombe ili wamlete reprofesari.
 
Back
Top Bottom