Mapokezi ya viongozi CUF yaota mbawa

Mapokezi ya viongozi CUF yaota mbawa

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,679
Reaction score
59,176
Dar es Salaam. Hofu ya kutokuwapo usalama ndani ya ofisi kuu za CUF Buguruni, imesababisha kuahirishwa mapokezi ya viongozi wakuu wa chama hicho.

Mapema jana, ilitangazwa kwamba Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, wajumbe wa baraza kuu la CUF na kamati ya uongozi ya chama wangefanyiwa mapokezi makubwa katika ofisi hizo lakini yaliahirishwa ghafla baadaye usiku kwa kuhofia kuwapo vurugu.

Kiongozi wa wabunge wa CUF waliokuwa wameandaa mapokezi hayo, Riziki Shahari alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa wameahirisha mapokezi hayo baada ya kujiridhisha kuwa hali ya usalama siyo nzuri.

“Tunazo taarifa kuwa yapo makundi hatari ya watu yanayoishi ndani ya ofisi huku yakilindwa na vyombo vya dola tangu ofisi hiyo iporwe na aliyewahi kuwa mwanachama na kiongozi wa juu wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akishirikiana na watu wanaomuunga mkono.

“Tunajipa muda wa kushauriana na viongozi wa juu wa chama chetu huku tukiwaomba wanachama wote walioko Dar, mikoani na Zanzibar wawe watulivu kwani chama kina viongozi makini na hawawezi kuwa tayari kuona maisha ya wanachana na viongozi yanahatarishwa kwa kuigeuza ofisi kuu kuwa uwanja wa mapambano,” alisema Shahari.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro alisema wabunge 41 kati ya 43 wa CUF walioandaa mapokezi hayo walikuwa wamekwishafika Dar es Salaam, lakini wamechunguza na kubaini kuwa yangeleta maafa.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF – Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema pamoja na hayo, chama hicho kimeshamalizana na Profesa Lipumba na kusisitiza kuwa si mwanachama tena.

Chanzo: Mwananchi
 
Kinachoendelea huku Bara ni dhahiri Seif hana wafuasi.
Maalim seif ndo kipenzi cha wanacuf hasa kule Zanzibar. Ungekuwa muungwana nyinyi mnaomuunga mkono Prof Lipumba alofilisika kisiasa mngemshauri aachie ngazi kwani tayari chama kimeshafanya maamuzi. Kuendelea kung'ang'ania kukaa ofcn ni kupoteza mda. Busara inaongea zaidi kuliko ubabe.
 
Ukweli upo palepale kitendo cha wajumbe na wabunge kumuunga mkono seifu tayari inaonyesha seifu anakubalika na cuf bara na visiwani
La hasha! Wajumbe wamehongwa bahasha ili wamkane profesa,wabunge wenyewe wamechimbwa mkwara ili waburuzwe.
 
Kama ni kwei unayoyasema ya nini watu wa lipumba kulala ofisini kwa kumuhofia asokubalika na Cuf?? wewe ni zaidi ya Mapumba

Pia piga U turn Jiulize kwa nn anaekubalika bara na Visiwani anaomba dola imsaidie kuingia Makao Makuu?
 
Pia piga U turn Jiulize kwa nn anaekubalika bara na Visiwani anaomba dola imsaidie kuingia Makao Makuu?
Ni kwa sababu lipumba AMEITEKA ofisi huku akilindwa na wahuni wenzake wenye Majambia, visu na chupa za kurusha zenye pilipili.
 
Wasiwasi wa lipumba ni nini hata basi kulala ofisini na kulindwa na vijana 10 nje ana hofu nini?
 
Ni kwa sababu lipumba AMEITEKA ofisi huku akilindwa na wahuni wenzake wenye Majambia, visu na chupa za kurusha zenye pilipili.

Nyie si Mnasemaga mwny Peoples Power hata dola Haiwezi sasa nyie hata Vibaka mnawaogopa!
 
Nyie si Mnasemaga mwny Peoples Power hata dola Haiwezi sasa nyie hata Vibaka mnawaogopa!

Nyie Si Huwa Mnasemaga Kuwa Watanzania Tuilinde Amani Sasa Unataka CUF watoke Na Mapanga Wakapigane na Wahuni Wa Propesa Lipumba?? Hebu Tumia Akili katika Maongezi! Hili Litatatulika Bila Ya Mapigano Haina Haja Ya Kumwaga Damu.
 
Back
Top Bottom