Mapokezi ya viongozi CUF yaota mbawa

Mapokezi ya viongozi CUF yaota mbawa

Pia piga U turn Jiulize kwa nn anaekubalika bara na Visiwani anaomba dola imsaidie kuingia Makao Makuu?

Umedhamiria Kupotosha! CUF haiombi Jeshi la Polisi Kuwaingiza Ofisini! Bali inafata taratibu Za Kisheria Kwani Haina Sababu Ya Kutumia Nguvu Kuingiwa Ofisini Kama alivyofanya Lipumba

Ndani Ya Ofisi Muna Lipumba na Wahuni Wenziwe, Sasa CUF ni lazima ifuate taratibu Za kisheria Kuwatoa Hao Genge la Wahuni! Kwani ikitumia Nguvu itakua ni Uvunjifu Wa Amani Na Dola itapata Nafasi Ya Kuzidi Kuukandamiza Upinzani Jambo Ambalo Dola Ndiyo Wanalolitaka.

Sasa Tulishuhudia Defenders Za polisi Zikimlinda Lipumbavu na Wahuni Wenziwe Wakimlinda Lipumbavu na Kumwingiza Kwenye Ofisi Ya CUF! Sasa Tunataka Haohao Polisi Waachane na Tabia Ya Kuwaunga Mkono Wahuni.
 
Kwa hiyo hii sinema ndiyo imeishia hapa? Au tusubiri part 2? Hii part 1 Professor kawagalagaza Wazenji. Mambo yatakuweje part 2? Tuvute subira.
 
Dar es Salaam. Hofu ya kutokuwapo usalama ndani ya ofisi kuu za CUF Buguruni, imesababisha kuahirishwa mapokezi ya viongozi wakuu wa chama hicho.

Mapema jana, ilitangazwa kwamba Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, wajumbe wa baraza kuu la CUF na kamati ya uongozi ya chama wangefanyiwa mapokezi makubwa katika ofisi hizo lakini yaliahirishwa ghafla baadaye usiku kwa kuhofia kuwapo vurugu.

Kiongozi wa wabunge wa CUF waliokuwa wameandaa mapokezi hayo, Riziki Shahari alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa wameahirisha mapokezi hayo baada ya kujiridhisha kuwa hali ya usalama siyo nzuri.

“Tunazo taarifa kuwa yapo makundi hatari ya watu yanayoishi ndani ya ofisi huku yakilindwa na vyombo vya dola tangu ofisi hiyo iporwe na aliyewahi kuwa mwanachama na kiongozi wa juu wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akishirikiana na watu wanaomuunga mkono.

“Tunajipa muda wa kushauriana na viongozi wa juu wa chama chetu huku tukiwaomba wanachama wote walioko Dar, mikoani na Zanzibar wawe watulivu kwani chama kina viongozi makini na hawawezi kuwa tayari kuona maisha ya wanachana na viongozi yanahatarishwa kwa kuigeuza ofisi kuu kuwa uwanja wa mapambano,” alisema Shahari.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro alisema wabunge 41 kati ya 43 wa CUF walioandaa mapokezi hayo walikuwa wamekwishafika Dar es Salaam, lakini wamechunguza na kubaini kuwa yangeleta maafa.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF – Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema pamoja na hayo, chama hicho kimeshamalizana na Profesa Lipumba na kusisitiza kuwa si mwanachama tena.

Chanzo: Mwananchi
Jee wanazungumziaje lile kundi lililokamatwa ambalo inadaiwa kuwa walitumwa na naibu katibu mkuu zbar[ wengine hadi sasa hawajulikani walipo]
 
Nyie Si Huwa Mnasemaga Kuwa Watanzania Tuilinde Amani Sasa Unataka CUF watoke Na Mapanga Wakapigane na Wahuni Wa Propesa Lipumba?? Hebu Tumia Akili katika Maongezi! Hili Litatatulika Bila Ya Mapigano Haina Haja Ya Kumwaga Damu.

Walipomaliza Kikao chao Zanzibar si walitangaza wenyewe kwa hiyari Yao kuwa watakwenda kumtoa Lipumba sasa wakat wanatangaza walikuwa hawajui kuwa kutatokea Vurugu ?
 
Half Time: Yunguru Ibrahim Haruna Lipumba (1)- Maalim Seif Sharif Hamad (0)
 
Kwanza hilo jahazi lililojaa wafuasi wa kaaf, kutoka visiwani lisachiwe mapanga na majambia.
 
Pia piga U turn Jiulize kwa nn anaekubalika bara na Visiwani anaomba dola imsaidie kuingia Makao Makuu?
anajua dola inahisi huenda dola inahusika na huo usumbufu anaoupata prof! kulala kwenye majimbu ya Buguruni kulinda cheo
 
Pro yuko kwenye himaya yake wangekuja wasinge amini macho yao kile ambaccho kingetokea naona wameona upepo sio mzuri
 
Nyie si Mnasemaga mwny Peoples Power hata dola Haiwezi sasa nyie hata Vibaka mnawaogopa!
Kwahiyo mkuu unataka Seif naye aende na Mapanga na majambia!? Tumia akili mkuu.
 
Heshma ya chama laziima irudi,bara na visiwani.profesa wewe ni shujaa huwezi kutuangusha.
 
Back
Top Bottom