kweli mkuu wabongo hatuna, afu mi nahic tatizo sio makocha,
cjui tatizo nn
Tatizo hatuna mipango ya muda mrefu. Hebu fikiria tu kidogo mkuu wangu, kuna vijana pale jangwani chini ya miaka 17 wananolewa ili baadae waje kuingizwa kwenye team ya wakubwa? Jibu ni kuwa kama wapo basi ni kwa kinafiki tu si kwa mipango mikakati ya ushindi.
Hizi team kubwa kama yanga na simba zina wanachama kila kona. Swali: Ni bahati iliyoje kwa timu kuwa na mashabiki wengi kiasi hivyo, lakini viongozi wake hawajui ni vipi wawashirikishe kuziendeleza timu zao zaidi ya kujipa mashavu na kupigana majungu kila timu inaposhindwa bila kurudi kwenye vyanzo vya tatizo.
Kitu kingine ni huu mtindo wa kujipendekeza kwa matajiri kama Manji kisa mfadhili! what the hell is this? Haiwezekani team nzima pamoja na kuwa na mashabiki wote hao hawana mawazo ya kujiondoa na hii minyonyoro ya mtu mmoja kuwa kama ndo mwenye kuimilki timu, wengine wakabaki kupiga makofi na kubebeshwa mizigo na pengine wanatumiwa kama daraja tu. Kuna namna nyingi za kuiongoza klabu bila kutegemea mtu mmoja aaafor 100% kila kitu {lazima awafanyie anavyotaka yeye} Mfano: Kuza vipaji, weka standards za mshahara kulingana na hali ya uchumi pamoja na kuweka mikakati yakitaalamu ya kukusanya mapato kwa kuwashirikisha wadau na wanachama. Tuchukulie tu Yanga leo hii ingekuwa na vijana wa soccer academy kutoka kila mkoa, nani angekataa kuchangia ile team 500 - 10000TZS watu wangetoa bila kuuliza inaenda kufanya nini. Wanamatawi mengi ya wanachama, lakini ukiuliza yanakazi gani? utaambiwa ni wakereketwa au wanapiga mavuvuzela. Hatuna viongozi wabunifu, ni wachumia tumbo kama ilivyo kwa TFF, wanaendesha tu kwa mazoea.
Navyojua mimi, mchezo wa soka ni dynamic game! its a living inakuwa kiwango vile vile inashuka kiwango! kwa hiyo lazima tuwe na mawazo ambayo ni dynamic yanayoweza kuforecast miaka hata 20 ijayo kuwa mchezo wa soka utakuwa unachezwaje, unaendeshwaje na utakuwa unahali gani ya kupendwa.