Mapokezi ya Kheri James yatikisa Mwanza

Mapokezi ya Kheri James yatikisa Mwanza

*KHERI JAMES APOKELEWA KWA HESHIMA KUBWA JIJINI MWANZA*

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Mwenyekiti we UVCCM Taifa Kheri James amepokelewa kwa heshima zote na Wanachama wa CCM na jumuiya zake wakati alipowasili kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani hapa akitokea Mkoani Shinyanga.

Mapokezi yake yameongozwa na viongozi kadhaa wa chama akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Anthony Dialo, Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Raymond Mwangangwala na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mwanza Rufungulo.

Akiwa kwenye ofisi za CCM Mwenyekiti wa CCM Mkoani humu Anthony Diallo alisema ushindi wa Kheri James na kuwa Mwenyekiti wa UVCCM si fahari tu ya mkoa wa Mwanza bali pia kielelezo cha malezi bora aliyoyapata toka akiwa Mwenyekiti wa tawi hadi Wilaya.

Diallo alisema Vijana wote wanahitaji kuiga mfano wa maisha ya Kheri katika siasa na uongozi kwani wakati wote amekuwa muaminifu kwa Chama na Serikali ya CCM na hakuwahi kuyumba kisiasa.

"Vijana fuateni na jueni maisha ya kijana mwenzenu Kheri. Angekuwa na kiburi au kukosa misimamo imara wa kukitumikia chama asingefika mahali alipo sasa na kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa " Alisisitiza Diallo.

Mara baada ya mapokezi hayo msafara wake huku akifuatana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Tabia Mwita na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ulikwenda moja kwa moja kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mjini hapa.

Kwenye viunga vya uwanja wa Kirumba mamia ya wanachama wa CCM na jumuiya zake walifurika kumlaki Mwenyekiti huyo mpya Mkoani hapa.
IMG-20180102-WA0182.jpg
IMG-20180102-WA0207.jpg
IMG-20180102-WA0183.jpg
 
Kila jambo na wakati wake, Naye Mugabe yalimkuta!
 
Naona mikutano ya hadhara imeruhusiwa rasmi.Kwani huyu naye ni mbungu, diwani au rais wa Tanzania????.
 
Mapokezi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu KHERI JAMES na Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa, Tabia Mwita katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza

[HASHTAG]#TukutaneKazini[/HASHTAG] View attachment 666450View attachment 666451


Huu ni ushetani ingalikuwa ni wapinzani wangeshapigwa mabomu na kulala rumande, madikteta ni manduli tu
 
inamana hako kajamaa kanamsafara wa kutosha kabisaaa
 
Hawezi kutikisa mwanza,bali uwezo wake ni kutikisa misukule.
 
We umesahau?,Cheo kimoja mtu mmoja. Anyway ,nmeposti ili kuona namna walimu walivyo tamalaki katika utawala huu.
 
Back
Top Bottom