Mapokezi ya Dr Slaa kutetemesha Karatu leo

Mapokezi ya Dr Slaa kutetemesha Karatu leo

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa leo ataanza ziara ya kichama kwenye jimbo la Karatu.

Ziara ya Dr Slaa ni ya kawaida ya kuimarisha chama na kuwanadi wagombea wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji.

Kama inavyokuwa siku zote kiongozi huyo anapozuru Karatu ni kwamba mapokezi makubwa sana yameandaliwa na inatarajiwa shughuli katika mji wa Karatu na viunga vyake kusimama walau kwa masaa 6 kupisha ujio wa kiongozi huyo maarufu zaidi Tanzania.

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Jumapili Chadema inatarajiwa kushinda mitaa,vijiji na vitongoji vyote jimboni Karatu kutokana na jimbo hilo kuwa ngome kuu ya Chadema kwa kipindi cha miaka 20 sasa.

Dr Slaa ni mzaliwa wa Karatu na ameongoza jimbo hilo kwa miaka 15 akiwa mbunge hivyo anaporejea nyumbani wanaKaratu wanasema ni mtoto amerudi nyumbani huku vijiji kadhaa vikitoa mbuzi na ngombe kuchinja na kufanya sherehe kwa heshima ya Kiongozi huyo wa kipekee.

Mapokezi katika picha:
10433937_595043210597777_9119763100152042000_n.jpg

10858600_595091103926321_3170641238429547717_n.jpg
10730993_595040857264679_1481196891995176623_n.jpg
10850045_595029290599169_1596058076531025311_n.jpg
 
Shughuli kusimama masaa sita ni sifa sana eeenh??!!!
Sehemu ambayo ni ngome kwa miaka ishirini bado unahitaji ushereheshaji wa aina hii yako muandishi??!!
Kuchinjiwa mbona ni jambo la kawaida saaana kwa jamii za kufuga, yaani hata bibi yangu nikienda hutoa japo kuku achinjwe!!!

Huku ndio kunaitwa kudekeza viongozi halafu wakipata madaraka mnataka watekeleze matakwa ya nchi wakati mnawazoesha wenyewe masifa na kujipendekeza bila sababu ya maana!!!
Ukombozi hauji kwa masifa kama anayopewa bibi harusi na muendesha sherehe!!!
 
Tunaomba updates za kutosha kutoka hapo karatu juu ya ziara ya dr. Slaa.
 
sasa huyo ---- aliejidai eti CHADEMA imefika mwisho karatu kazi kwake, jemedari anaingia karatu huyo
 
Haya wale viumbe wanaolipwa elfu saba ili kumtukana Dr Slaa karibuni.

Kutukana ni utovu wa nidhamu ila na nyie wafuasi muandike mambo yenye mashiko kuhusu hao mnaowalinda na kuwatetea!!!
Angeweza kuweka ratiba ya shughuli kwa mfano, malengo na matarajio chanya ya wanachi na Taifa kwa ujumla wake kutokana na ziara hiyo,

sio habari za kuchinjiwa mbuzi na ng'ombe mara ooonh ni mzaliwa wa huko, hajamaliza anakuja ni ngome na inatarajiwa kushinda ngazi zote!!!!

Kwa kiongozi wa Kitaifa hapo habari ni nini ?!
 
Mungu ambariki sana Dr Slaa. ...hawa akina mwigulu lameck na walaaniwe kwa kumtukana Dr Slaa bila sababu
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa leo ataanza ziara ya kichama kwenye jimbo la Karatu.

Ziara ya Dr Slaa ni ya kawaida ya kuimarisha chama na kuwanadi wagombea wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji.

Kama inavyokuwa siku zote kiongozi huyo anapozuru Karatu ni kwamba mapokezi makubwa sana yameandaliwa na inatarajiwa shughuli katika mji wa Karatu na viunga vyake kusimama walau kwa masaa 6 kupisha ujio wa kiongozi huyo maarufu zaidi Tanzania.

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Jumapili Chadema inatarajiwa kushinda mitaa,vijiji na vitongoji vyote jimboni Karatu kutokana na jimbo hilo kuwa ngome kuu ya Chadema kwa kipindi cha miaka 20 sasa.

Dr Slaa ni mzaliwa wa Karatu na ameongoza jimbo hilo kwa miaka 15 akiwa mbunge hivyo anaporejea nyumbani wanaKaratu wanasema ni mtoto amerudi nyumbani huku vijiji kadhaa vikitoa mbuzi na ngombe kuchinja na kufanya sherehe kwa heshima ya Kiongozi huyo wa kipekee.

Michael Hayshi na Botha waliojiunga na CCM si ndio watajuta leo kwa kujiunga na mafisadi ! Yetu macho na masikio.
 
Hao uliowataja ni makapi yasiyo na nafasi kwa siasa za Karatu

Watu wa karatu tunataka Dr slaa amuunganishe Lazaro Titus Masai na mwenzake Bota waelekee CCM diwani huyu wa chadema amefisdi Miradi Mingi ya maendeleo hasa kiwanda cha maziwa alichotapeli zaidi ya milioni 100 tunataka kauli kali ya dr slaa kuhusu kuwajibika kwa diwani huyu aka TUMBO
 
Huyo Botha aligombea ukatibu huko Karatu akakosa, jana amepiga hela za ccm kwa kijifanya yeye ndiye katibu! kweli wajinga ndio waliwao...

Huyo ni mwizi ndiyo maana Wanachama walimnyima kura
 
Huyo ni mwizi ndiyo maana Wanachama walimnyima kura

Jamaa kawaingiza kingi akina mwigulu na jamii yake wakaamini kuwa wamempokea katibu wa cdm Karatu! Kapiga hela na amesepa!!!!
 
Slaa hawezi kupata mapokezi makubwa kama aliyoyapata Mwigulu Karatu
 
Back
Top Bottom