Mapishi ya ndizi mzuzu

malisak

JF-Expert Member
Mar 16, 2006
694
773
Mahitaji:-

Ndizi mzuzu (mbivu) 15

Nazi ya azam pkt 3

Maji kiasi

Hiriki ilopondea kijiko 1 1/2 cha chai

Zabibu kiasi ,ukipenda

Cornflour/custard powder vijiko 2 vya chai

Sukari kiasi

Chumvi kijiko 1 cha chai

Vanilla ya unga 1/2 kijiko cha chai

Mafuta kijiko 1 cha chai, sio lazima

MAELEKEZO:-

1. Menya ndizi zako vizuri, pasua kati kisha toa mzizi wa Kati na zigawe upendavyo.

2. Tia katika sufuria pamoja na maji kiasi ya kutosha kuivisha pamoja na chumvi, mafuta na hiriki.

3. Acha zichemkie kidogo kisha Tia nazi moja, sukari na zabibu ,acha ziendelee kuchemkia.

4. Ukiona zimeanza kuwa laini Tia Nazi zilizobaki katika bakuli koroga pamoja na vanilla, custard au cornflour kisha mwagia juu ya ndizi acha zitokote na kuwa nzito. Enjoy !

Note:

Unaweza tumia nazi fresh kupata tui, kama nazi 2 kubwa zatoshe

Inapendeza zaidi usiache zikapondeka ziive ziwe laini lakini zipaki katka Shep yake. Pia mapishi haya ni mazuri sana kipindi hiki cha mfungo, na mazuri kunywea uji wa chumvi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom