Mapishi ya Mlenda wa bamia na nyanya chungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapishi ya Mlenda wa bamia na nyanya chungu

Discussion in 'JF Chef' started by FirstLady1, Nov 8, 2011.

 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Karibuni kwa Bibi yangu Singida>.

  [h=3]Mapishi ya Mlenda wa bamia na nyanya chungu[/h]
  Mahitaji
  Bamia (okra) 20
  Nyanya chungu (garden eggs) 5
  Magadi soda (Bicabonate soda) 1/4 ya kijiko cha chai
  Nyanya (fresh tomato) 1
  Chumvi (salt) kidogo
  Pilipili 1/4

  Matayarisho
  Osha bamia, nyanya chungu na nyanya kisha vikatekate katika vipande vidogovidogo. Baada ya hapo vitie kwenye sufuria na vitu vyote vilivyobakia na kisha tia maji kidogo.Chemsha mpaka bamia na nyanya chungu ziive na vimaji vibakie kidogo sana. Baada ya hapo ziponde na mwiko kidogo kisha zikoroge na uipue na mlenda utakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.
   
Loading...