Mapishi ya Mixed vegetable fried rice | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapishi ya Mixed vegetable fried rice

Discussion in 'JF Chef' started by FirstLady1, Nov 8, 2011.

 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  [h=3]Mapishi ya Mixed vegetable fried rice
  Mahitaji
  Wali uliopikwa (cooked rice) kiasi
  Hoho la kijani (green pepper) 1/2
  Hoho jekundu (red pepper) 1/2
  Carrot 1
  Kitunguu kikubwa (onion) 1
  Njegere (pears) 1/2 kikombe cha chai
  Mayai (eggs) 2
  Uyoga (mushroom) 2 vikombe vya chai
  Soy source 2 vijiko vya chakula
  Chumvi (salt) kiasi
  Mafuta (veg oil) 3 vijiko vya chakula

  Matayarisho
  Katakata hoho, kitunguu,na uyoga vipande vikubwa kiasi(chunks) kisha katakata carrot zisiwe nene au nyembamba sana. Baada ya hapo weka mafuta katika katika frying pan yako isiyoshika chini acha yapate moto kisha tia uyoga na ukaange mpaka uive.Baada ya hapo tia vegetable zote na uzikaange pamoja na uyoga kwa muda wa dakika 2, kisha katika hiyohiyo frying pan zisogeze vegetable zako pembeni (ili kupata nafasi ya kukaangia mayai).Yakaange mayai katika hiyo sehemu yakiisha iva yavuruge na kisha yachanganye pamoja na vegetable na kisha tia chumvi kidogo sana. Baada ya hapo malizia kwa kutia wali na soy source kisha koroga vizuri mpaka mchanganyiko wako wote uchanganyike vizuri (hakikisha wali unapata
  moto na vegetable haziivi sana) . Na baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari
  2011 005[1].JPG [/h]
   
Loading...