Mapishi ya kababu za nyama na kababu za mayai

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
40,598
52,298
1. Mapishi Kababu za nyama (Meat Ball)
Leo tuangalie mapishi ya meat ball (kababu) za nyama ya ng'ombe. Ni kitafunwa kizuri sana kwa asubuhi au hata jioni.

Mahitaji
· Nyama ya kusaga 1/2kg
· Yai 1
· Kitunguu maji 1
· Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1
· Pilipili manga kijiko cha chai
· Chenga za mkata (bread crumbs) kikombe cha chai
· Kotmir majani 3
· Chumvi kiasi
· Mafuta ya kupikia

Matayarisho
1. Katakata vitunguu maji vipande vidogo vidogo, kisha changanya nyama ya kusaga, vitunguu maji ,kotmiri iliyokatwakatwa, vitunguu saum (tangawizi ukipenda), na chenga za mkate.(Ukitumia chenga za mkate halisi ni nzuri zaidi kuliko zile spesho za madukani). Weka chumvi na pilipili manga. Waweza pia weka pilipili mbuzi kama utapendelea.

2. Pigapiga yai na kisha uchanganye kwenye mchanganyiko wako, hakikisha vimechanganyika kabisa. Kisha tengeneza madoge madogo ya mviringo na weka pembeni. Hakikisha madonge sio makubwa sana ili nyama iweze iva vizuri.

3. Weka kikaango jikoni na mafuta na kiasi ili madonge yako yasizame, weka kababu zako kwenye mafuta na ziache ziive upande mmoja kisha geuza na upande mwingine. Zingatia moto uwe wa kiasi ili zisibabuke bali ziive hadi ndani kabisa.

4. Epua na weka kwenye sinia yenye karatasi za jikoni ili zichuje mafuta yote kisha weka mezani tayari kwa kula.
Waweza kula na chai, juis, soda au hata mchuzi wa maharage, mboga za majani n.k jinsi upendavyo mwenyewe.



2. Kababu Za Mayai
VIPIMO

1. Mayai yaliochemshwa 6
2. Nyama ya kusaga 1 1/2 Ratili (LB)
3. Tangawizi na thomu iliyosagwa 1 kijiko cha Supu
4. Pilipili mbichi ya Kusaga 1
5. Mafuta 2 Vijiko Vya Supu
6. Unga wa mahindi (Constarch) 1 Kijiko cha Supu
7. Chumvi Kiasi
8. Bizari ya manjano 1/4 kijiko cha chai
9. Dania ya unga 1/4 Kijiko cha chai
10. Bizari ya Pilau 1/4 Kijiko cha chai


NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1.Changanya nyama na vitu vyake kisha gawanya madonge 6 yaliyosawa.

2.Chukuwa donge moja tia ndani yake yai uliochemsha na lifunike vizuri .

3.Ukisha maliza yote panga kwenye treya la kupikia katika jiko la oveni nyunyizia mafuta kidogo na choma moto wa 375F kwa muda wa dakika 25.

4.Yakishaiva epua na kisha ukate kama ilivyo kwenye picha .Tayari kuliwa

Viungo vinapatikana ktk maduka ya viungo au supermarkets
 
Daa!! wewe mama wa zamani san humu heshima kwako!!! kipindi hki nilikuwa nasoma chuo!! ila unaeza kulea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom