Mapingamizi (Objections) Kwenye Kesi Mahakamani

Apr 26, 2022
64
100
Kwenye sheria kuna objections (mapingamizi), kama ukikosea au ukishindwa kufata utaratibu wa kufungua kesi au kuwasiliana na Mahakama, basi unaweza kukumbana na pingamizi ambalo litapelekea kesi yako iondolewe Mahakamani (dismissed) au kutupiliwa mbali kabisa (struck out) bila hata kusikilizwa unadai nini. (Kwa sababu pingamizi lazima lianze kusikilizwa kwanza kabla ya kuendelea kusikiliza kesi ya msingi (merit of the case).

LENGO LA PINGAMIZI

Lengo la pingamizi ni kuokoa muda wa Mahakama na muda wa wanaoshtakiana kwa kutoendelea mbele na kesi wakati kuna hoja ya kisheria itamaliza kesi mapema tu. (Ingawa kwa kweli haiko hivyo wakati wote, muda mwingine mapingamizi yametumika kuchelewesha kesi).

Namnukuu aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mheshimiwa Jaji Rutakangwa, kwenye hotuba yake aliyoitoa kwenye Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa
Mahakama ya Tanzania, Bagamoyo, tarehe 23-25 April, 2013, alisema,

“watumiaji wengi wa Mahakama ama kwa kutojua au kwa makusudi ya kuchelewesha shauri mahakamani wanatumia vibaya pingamizi hizi. Kwa bahati mbaya sisi pia tunawavumilia. Pingamizi ambazo ni “misconceived”, ni lazima zitupiliwe mbali “at the threshold”. Zisitupotezee muda wetu na wa wateja wetu wengine.”

AINA ZA MAPINGAMIZI (TYPES OF OBJECTIONS)

1: Preliminary Objections (ya awali)
2: Trial Objections (wakati wa kesi)

1: Preliminary objections (mapingamizi ya awali): Ni mapingamizi ambayo huibuliwa katika hatua za mwanzo wa kesi. Lakini kuna masharti, sio kila hoja inafaa kuwa pingamizi la awali, usipinge pinge tu chochote unachotaka.

Pingamizi la awali lazima liwe ON PURE POINT OF LAW (hoja tupu za kisheria) sio maneno au mambo ambayo mpaka tukae tena kuita mashahidi. Usiweke pingamizi ambalo kufanikiwa kwake mpaka tena tuanze kuita mashahidi. Kama pingamizi lako ili lithibitike hadi walete ushahidi, hilo halifai kuwa pingamizi la awali. Pia pingamizi la awali lenye mashiko, ni lile ambalo kama likisikilizwa, likifanikiwa linamaliza kesi papo hapo.

Sifa za Pingamizi la awali zimeelezwa na Mahakama kwenye kesi pendwa na maarufu sana ya Mukisa Biscuit Manufacturing Co. Ltd. vs West End Distributors Ltd [1969] E.A. 696.

MFANO WA OBJECTIONS (MAPINGAMIZI)

Objections ziko nyingi, mfano kama umefungua kesi kwenye Mahakama ambayo haina mamlaka (tena hili pingamizi unaweza kukumbana nalo kwenye hatua yoyote ya kesi, halina cha ulichelewa kusema, hata kama umekuja kuligundua wakati wa kusikiliza rufaa, Mahakama ikijiridhisha kwamba kule chini ulikoanzia hawakuwa na mamlaka, wataporomosha chini maamuzi yote yaliyofanyika kuanzia huko chini mpaka hapo ulipofikia, alafu mtaanza upya).

Sasa hapo ndo utajua kama inaokoa muda au inachelewesha?

Mapingamizi mengine ni kama vile unakuta umefungua kesi nje ya muda, umefungua kesi bila idhini au ruhusa (leave) ya Mahakama (kwa kesi zinazohitaji idhini au ruhusa), umerudia upya kesi ambayo ilishawahi kusikilizwa ikaisha, au hauna uwezo (capacity) au miguu ya kusimama Mahakamani (locus stand), umekosea au haujaweka kifungu sahihi, umekosea nyaraka (document), au Wakili hana leseni n.k.

2: TRIAL OBJECTIONS - Ni mapingamizi yanayoibuliwa wakati wa kesi. Mfano wakati wa kutoa ushahidi wa nyaraka, sheria inataka original document (nyaraka halisi) we unaleta vivuli (kopi) bila kueleza sababu (grounds), lazima utawekewa pingamizi.

Kuna kitu kingine kinaitwa OBJECTION PROCEEDINGS (KESI PINGAMIZI).

(Usichanganye kati ya Objection Proceedings (kesi pingamizi na mapingamizi mengine)

Objection proceedings (KESI PINGAMIZI) kama jina lake lilivyo ni kesi inayofunguliwa Mahakamani kupinga utekelezaji wa hukumu. Na inafunguliwa na mtu mwingine kabisa ambaye hahusiki kwenye kesi (third party) lakini mali yake imeunganishwa kwenye hukumu.

Mfano, umeshinda kesi na sasa unataka kutekeleza (kufaidi) hiyo hukumu, umeunganisha au unataka kuuza mali ambazo unafikri ni za mdaiwa aliyeshindwa kesi (judgement debtor). Ikitokea hivyo, yule mmiliki halisi anaweza kwenda Mahakamani kupinga mali yake isiambatanishwe kwenye kutekeleza hukumu - Kesi ya namna hiyo ndio tunaita Objection proceedings.

AINA ZA OBJECTION PROCEEDINGS

Zipo objections proceedings nyingi

Soma Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Madai (Civil Procedure Code), kwa kifupi tunaiita CPC. Soma Order XXI kuanzia rule 57 - 62.

HOW TO INSTITUTE OBJECTION PROCEEDINGS (JINSI YA KUFUNGUA KESI KUPINGA MALI ZAKO ZISIAMBATANISHWE)

Ukitaka kupinga mali zako zisiambatanishwe na kuuzwa kwenye kutekeleza hukumu ya Mahakama, unafungua kesi kupitia nyaraka (documents) zinazoitwa CHAMBER SUMMONS na AFFIDAVIT. Order XXI rule 57 ya CPC.

Kesi itakuwa ni kati yako na upande wa pili watakuwa wale waliokuwa wanahusika kwenye kesi. Mahakama ikikuta mali yako imeambatanishwa kimakosa basi itaondolewa.

FAILURE OF OBJECTION PROCEEDINGS: REMEDIES AVAILABLE
(UKISHINDWA KESI, UTAENDA WAPI ZAIDI):

Ikiwa Mahakama itaamua kwamba hiyo sio mali yako, njia pekee iliyopo ni kurudi kufungua kesi mpya. (Huruhusiwi kukata rufaa.

Kwa hiyo kama Mahakama ikitoa amri ambayo inakuathiri wewe wakati haukuhusika kwenye kesi, kuna njia mbili:
1: Fungua kesi kupinga (objection proceedings)
2: Ukishindwa rudi ufungue kesi upya, uwashtaki wale waliokuwa wanadaiana kwenye kesi wote wawili.

Sasa swali, objection proceedings (kesi ya kupinga mali zako zisiambatanishwe) unafungua wakati hukumu inataka kutekelezwa, mfano wakati wanataka kuuza. Je, ikitokea wameshauza mali zako na wewe hauhusiki na hiyo kesi, utafanyaje? Mwenye maswali zaidi wasiliana na Mawakili.

-----MWISHO----

Angalizo: Position au maelezo haya ni kwa mujibu wa kesi na sheria zilizokuwa zinatumika mpaka siku ya kupost hili andiko. Hivyo unaposoma leo haya maelezo, soma kesi na sheria zilizopo sasa hivi, ili ujue utaratibu bado ni ule ule au la! Sheria zinarekebishwa na mpya zinatungwa kila siku.

Pia natoa angalizo, wale wazee wa kukopi machapisho ya watu na kuweka majina yenu. Ni kosa kisheria. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejimilikisha andiko hili. Unaruhusiwa tu kusambaza lakini usibadili yaliyomo. Ni heri uanze kuandika ya kwako mpya.

Disclaimer: Lengo la hii makala ni kutoa elimu kwa jamii. Huu sio ushauri wa kisheria kwa mtu yeyote. Ikiwa utaamua kufungua kesi kwa kufata haya maelezo na ukapata hasara, mwandishi wa maelezo haya hatawajibika kwa vyovyote vile. Kama unahitaji ushauri wa kisheria wasiliana na Mawakili.

Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke. 0754575246 - WhatsApp.
(Karibuni kwa nyongeza na maswali).
 
Ahsante mkuu.
 
Back
Top Bottom