Mapinduzi ya kisiasa Zanzibar

Mchoraji Cyper255

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
1,758
6,087
Leo ukienda Visiwa vya Zanzibar utashuhudia maghorofa kuanzia Unguja mpaka Pemba,mjini mpaka mashambani,maghorofa hayo yote naambiwa yalijengwa na Hayati Mzee Abeid Karume!.

Hayati Mzee Karume alijenga maghorofa haya kati ya 12.1.1964 baada ya mapinduzi na 7.4.1972 pale alipokutwa na umauti baada ya kupigwa risasi akiwa katika ofisi ndogo za CCM maeneo ya Kisiwandui Unguja!.

Mzee Karume alikuwa na kampeni ya kuhakikisha wazanzibar wanaishi katika nyumba bora,ndiyo maana ndani ya miaka nane Mzee huyu alijenga maghorofa kwa ajili ya makazi ya wazanzibar!.

Hayati mzee Karume alikuwa na mkakati wa kuifanya Zanzibar kuwa kituo cha utalii na pia alitaka kuifanya Zanzibar kuwa kituo cha Lugha Afrika mashariki kama siyo Afrika nzima.

Pamoja na nia njema aliyokuwa nayo mzee Karume kwa visiwa vya Zanzibar,bado kumbukumbu/kivuli cha uchaguzi wa kwanza visiwani Zanzibar uliofanyika July 1957 na kufatiwa na ule wa July 1963 na kushuhudia muungano wa vyama vya ZNP na ZPPP vikishinda uchaguzi huu wa pili dhidi ya mahasimu wao ASP na kumchagua Mzee Shamte Mohamed Hamad kuwa waziri mkuu,uchaguzi huu ulibaki kuwa kikwazo kwa utawala wa Hayati Karume!.

Mwaka 1964 (tarehe 12.Januari),ASP walifanya mapinduzi na kuuondoa utawala wa ZNP na ZPPP ambao ASP waliamini kuwa walikuwa bado wana vinasaba na sultan,mapinduzi hayo mara baada ya kufanyika ili kuimarisha usalama Hayati Karume alilazimika kwa niaba ya wazanzibar kwa kushirikiana na Rais wa Tanganyika wakati huyo hayati Julius Nyerere wakaunganisha nchi hizi mbili tarehe 26.4.1964 ikiwa ni miezi mitatu tu toka yafanyike mapinduzi huko Zanzibar!.

Historia inasema,Hayati Mzee Karume mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar alitangaza kuwa asingependa kuona uchaguzi unafanyika visiwani Zanzibar mpaka baada ya miaka 50,kwa maana hiyo kama hili lilikuwa ni dhamira ya dhati Zanzibar ilitakiwa kufanya uchaguzi wa kwanza mwana 2014!.

Pamoja na mapinduzi hayo kufanyika,Utawala wa Hayati Karume ulikuwa katika upinzani mkali kutoka kwa wafuasi wa vyama vilivyoshinda uchaguzi wa mwaka 1963(ZNP na ZPPP),kumbuka matokeo ya uchaguzi wa 1963 yalilalamikiwa sana na ASP waliodai kuwa walishinda kwa asilimia 54,ASP walilalamika kuwa waliibiwa kura!.ZNP kwa ushirikiano na ZPPP waliongoza Serikali ya Zanzibar kwa miezi mitano tu(July 1963-Jan 1964).

Taarifa za kichunguzi kutoka kwa wazee na waliofanya kazi na Mzee Karume wanasema baada ya mapinduzi ya Zanzibar,serikali iliweka katazo la kiwaajiri serikalini watu wasio wanachama wa ASP,ilikuwa sharti uwe ASP ndiyo utapata kazi serikalini kwa wakati huo!.

Sharti hili kwa mara kadhaa liliaababisha kutokuelewana kati ya Hayati Karume na Hayati Nyerere baada ya Mwalimu Nyerere kuwaajiri ndani ya serikali ya muungano baadhi ya wazanzibar ambao hawakuwa wana ASP,miongoni mwao alikuwa Prof Abdulahman Babu kutoka chama cha UMMA!.

Zanzibar pamoja na kufanya mapinduzi mwaka 1964,hayakuwaunganisha wazanzibar,maisha ya kutokuaminiana yaliendelea,kifo cha Mzee Karume mwaka 1972 kiliongesa hofu visiwani humo,hata baada ya Mzee Abood Jumbe kupewa madaraka ya urais wa Zanzibar baada ya mapinduzi ,Zanzibar ilipita kwenye kipindi kingine kigumu kati ya mwaka 1972-1984.

Kwenye kipindi hiki tulishuhudia Viguvugu la kuuvunja Muungano,baadhi ya wazanzibar walianzisha kampeni za chinichini za kuuvunja muungano kwa madai yalikuwa makubaliano ya watu wawili(Julius Nyerere na Abeid Karume).

Hata Rais wake mzee Jumbe inasemekana aliunga mkono vuguvugu hilo,kiliandikwa kwa siri kitabu kilichoitwa "Partnership",kitabu hiki hakikuwahi ingia mtaani na kusomwa baada ya kukamatwa na makachero!.

Serikali ya Muungano na ile ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwatumia makachero kilichunguza vuguvugu hilo,mwaka 1984,bila kujua kama anavhunguzwa,Hayati mzee Jumbe aliitwa Dodoma na kusomewa mashtaka ya kutaka kuuvunja muungano,Julius Nyerere alimsomea mashtaka yake mbele ya wajumbe wa kamati kuu,Mzee Jumbe alivuliwa madaraka ya Urais mjini Dodoma na kupelekwa kuishi Kigamboni alipoishi mpaka umauti unamkuta!.

Wakati Mzee Jumbe anavuliwa madaraka,CCM ilimuibua Ally Hassani Mwinyi ambaye miaka mitatu iliyopita alilazimika kujiuzuru nafasi ya uwaziri wa mambo ya ndani kwenye serikali ya Muungano na kumteuwa kuwa Rais wa Zanzibar nafasi aliyohudumu kwa mwaka mmoja tu kwani mwaka 1985 alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania!.

Wakati wote huo wa mzee Jumbe akivuliwa madaraka,Katibu mkuu wa sasa wa CUF Maalim Seif alikuwa Waziri Kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar,zipo taarifa kuwa Maalim Seif alikuwa kipenzi cha Julius Nyerere na alikuwa akiaminiwa sana na Nyerere!.

Mwaka 1985,Maalim alichukua fomu ya kuwanua urais wa Zanzibar akipambana na akina Abdul Wakili,Salim Ahmed Salim.Nasikia Salim Ahmed Salim alishawishiwa ajitoe!.

Kinyan'ganyiro kilikuwa kikali,Maalim Seif alikuwa na mashabiki wengi,wachambuzi wa masuala ya siasa za Zanzibar wanasema mchuano huu ulikuwa mkali kama ule wa 1957 na 1963,tofauti yake ni moja tu,wa mwaka 1985 ulikuwa ndani ya CCM!.

CCM walipokaa Dodoma walilipitisha jina la Abdul Wakili,uamuzi huo uliwasononesha baadhi ya wazanzibar hususani kutoka Pemba,hawakukubaliana na uamuzi wa kulikata jina la Maalim,kilichofanyika mwaka 1985,ni wazanzibar baadhi kuichagua Sehemu ya kivuli na kutompa kura ya ndiyo Abdul wakili!.

Baada ya uchaguzi,CCM ilianza kuwasaka iliowaita wasaliti walioratibu kura za maruhani,msako huu ukawanasa kwenye hatia akina Juma Duni Haki,Maalim Seif Sharif Hamad,Hamad Rashid Mohamed n.k ambao walijikuta wakifukuzwa ndani ya CCM!.

Wafukuzwa hawa walianzisha chama chao ambacho hakikuwa kimesajiliwa kisheria,mwaka 1992 baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza,kundi lililofukizwa visiwani Zanzibar ndani ya CCM liliungana na akina Shaban Mloo na James Mapalala kutoka bara kuanzisha chama cha CUF,ambacho kimeendelea kuwa chama kikuu cha upinzani huko Zanzibar!.

Mwaka 1995,2000,2005,2010na 2015,CUF kimetoa ushindani mkali kwa CCM hususani kule Pemba,mara mbili kuliibuka mtafaruku wa utangazwaji wa matokeo,mwaka 1995 kituo kimoja cha TV kilimtangaza Maalim kama mshindi na kikajikuta kikifungiwa kwa kukiuka sheria,mwaka 2015,Maalim aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kusema atangazwe mshindi haliniliyosababisha uchaguzi kufutwa na uliporudiwa CUF waligoma kushiriki!.

Mwaka 1995 mchuano mkali ulikuwa kati ya Dr Salmin Amoor na Maalim Seif,kati ya Mwaka 1995-2005,Zanzibar ilipita kwenye siasa kali,zilizoifanya dunia nzima kuhamia Zanzibar kufuatilia nini kinaendelea huko!.

Mwaka 2000,CUF waligomea uchaguzi na kutangaza maandamano mwezi Jan 2001,maandamano yaliyoshuhudia risasi za moto,baadhi walikimbia visiwani humo na kwenda Shimon Mombasa,wengine wakaja bara,baadhi wakapoteza maisha,hapo tukaanza shuhudia wasuluhishi wakija nchini!.

Mwaka 2005,Ikawa zamu ya Maalim Seif dhidi ya Aman Karume,ulikuwa uchaguzi mgumu,upande wa Muungano alishinda Jakaya Kikwete,baada ya ushindi,kwenye hotuba yake ya kwanza alitangaza kusononeshwa na kinachoendelea Zanzibar,ziliundwa tume ikiwemo ile ya Shelukindo zilizokuwa na kazi ya kujua kero za Muungano!.

Kipindi cha miaka mitano 2005-2010 kilikuwa cha kusaka suluhu za mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar,suluhu ilisakwa kwa kuja na pendekezo la mabadiliko ya katiba ili kuweka hali sawa huko Zanzibar na kutekeleza mapendekezo ya Kamati ya Shelukindo ili kuondoa kero za Muungano,naambiwa Jakaya Kikwete alizipunguza kutoka 24 mpaka 4.

Nadhani umeona jinsi siasa za Zanzibar zilivyongumu,tangu uchaguzi wa 1957 kumekuwa na malalamiko ya kubiwa!mwaka 1963,CCM wakati huo ikiwa ASP ilishindwa uchaguzi wa pili na kulalamika kuwa ilishinda kwa asilimia 54 lkn ikadai iliibiwa kura!.

Ugumu huu wa siasa za Zanzibar ndiyo uliowafanya Maalim Seif Sharif na Aman Karume kukubali marekebisho ya katiba mwaka 2010 na kuruhusu serikali ya umoja wa kitaifa!.

Mpaka Juma Nature na Prof J walitunga wimbo waliouta CCM na CUF!

Mungu vibariki visiwa vya Zanzibar,Mungu ibariki Tanzania!.

Nawatakia Siku njema.

Credit to: Dotto Bulendu
 
Back
Top Bottom