Mapinduzi Cup: Ashanti Yadundwa, Azam Yatakata

Mapinduzi Cup: Ashanti Yadundwa, Azam Yatakata

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
AZAM WAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI, WAWAFUMUA 2-0 ‘TIMU YA TAIFA' YA UNGUJA

Home » Unlabelled » AZAM WAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI, WAWAFUMUA 2-0 ‘TIMU YA TAIFA' YA UNGUJA
Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC leo wameanza vyema michuano hiyo, baada ya kuifunga Spice Stars mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi C jioni hii Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Hata hivyo, Azam ililazimika kusubiri kuanza kushangilia mabao yake dakika ya 71, baada ya mshambuliaji Mganda, Brian Umony kuwatoka mabeki wa Spice na kumchambua kipa Mohamed Silima, kufuatia pasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy'.[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Wachezaji wa Azam FC wakimpongeza Brian Umony kushoto kwa kufunga bao la kwanza[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Brian aliyeingia dakika ya 59 kuchukua nafasi ya Muamad Ismael Kone, alikuwa mwiba wa safu ya ulinzi ya Spice.
Himid Mao aliifungia Azam bao la pili dakika ya 86, baada ya kuuwahi mpira uliokuwa unaelekea mikononi mwa kipa Silima kufuatia shuti la Salum Abubakar na kupiga shuti lililotinga nyavuni.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Mfaume Ali, mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mcameroon Joseph Marius Omog kipindi cha pili kuwatoa Khamis Mcha ‘Vialli', Kipre Herman Tchetche na Kone na kuwaingiza Umony, Joseph Kimwaga na Seif Abdallah ndiyo yalileta ushindi huo. [TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche akijiandaa kupiga krosi dhidi ya beki wa Spice Stars, Said Mussa 'Udindi'[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Azam walitawala zaidi mchezo katika dakika 45 za kwanza, lakini wakakosa mbinu za kuivunja ngome ya Spice, inayoundwa na wachezaji mchanganyiko wa Unguja.
Kocha Omog alifanya mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza cha Azam leo, akimrejesha Himid Mao kucheza nafasi ya kiungo pamoja na Salum Abubakar ‘Sure Boy' na Kipre Michael Balou, huku Erasto Nyoni akicheza beki ya kulia na Waziri Salum beki ya kushoto.
Azam ilitawala sehemu ya kiungo na pasi nyingi ziliwafikia washambuliaji Kipre Herman Tchetche na Muamad Ismael Kone, lakini wakashindwa kabisa kufunga kipindi cha kwanza.
Kwa ushindi huo, Azam inaongoza Kundi C kwa pointi zake tatu, na kubaki au kushuka itategemea na matokeo ya mchezo wa pili jioni ya leo Uwanja wa Amaan kati ya Ashanti United ya Dar es Salaam na Tusker FC ya Kenya.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Erato Nyoni, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar, Muamad Kone/Brian Umony dk59, Kipre Tchetche/Seif Abdallah dk 70 na Khamis Mcha ‘Vialli' dk49.
Spice Stars; Mohamed Silima, Abdallah Salum, Suleiman Ally/Abdulhakim Abdul dk81, Said Mussa, Said Ahmed, Hassan Said, Mohamed Salum, Mohamed Nassor/Yunus Bernad dk80, Ibrahim Hamad/Hakim Hamisi dk46, Abdallah Seif na Mohamed Abdulrahim.
Katika mchezo mwingine wa Kundi A, Uwanja wa Gombani, Pemba, URA ya Uganda imetoka sare ya 2-2 na Chuoni ya Zanzibar.
Mabao ya URA yamefungwa na Owen Kasuule dakika ya 44 na 57, wakati ya Chuoni yalifungwa na Shaaban Moke dakika ya 21 na Mwinyi Mngwali dakika ya 45

ASHANTI United imeanza vibaya michuano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kufungwa bao 1-0 na Tusker ya Kenya katika mchezo wa Kundi C usiku huu, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bao pekee lililoizamisha Ashanti hii leo limefungwa na Joshua Oyoo dakika ya 24, akiunganisha krosi ya Ali Abondo

​
 

Kipa wa Tusker, Samuel Odhambo akiokoa hatari langoni mwake dhidi ya mshambuliaji wa Ashanti
 

Mshambuliaji wa Ashanti United, Kassim Kilungo kushoto akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Tusker kulia
 

Mchezaji wa Tusker akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Ashanti
 
Wachezaji wa Tusker kulia na wa Ashanti kushoto wakigombea mpira wa juu
 

Kiungo wa Ashanti, Malik Jaffar akiambaa kulia
 

Kikosi cha Ashanti le
 

Benchi la Ufundi; Kutoka kulia kocha wa makipa, Mfaume Athumani, Kocha Msaidizi, Nico Kiondo na Kocha Mkuu Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden
 

Kiungo wa pembeni wa Azam FC, Khamis Mcha 'Vialli' akimtoka beki wa Spice Stars ya Zanzibar katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi, uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni ya leo. Azam ilishinda 2-0
 

Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche akiondoka na mpira baada ya kumlamba chenga ya hatari beki wa Spice kwenye chaki
 

Kiungo wa Azam FC, ambao ni mabingwa mara mbili wa Kombe la mapinduzi, Himid Mao akiwatoka mabeki wa Spice
 

Beki wa Spice, akiwa ameudodokea mpira huku mshambuliaji wa Azam FC, Muamad Ismael Kone akitafuta maarifa ya kuuchukua
 

Muamad Ismael Kone anaugulia maumivu chini huku Kipre Tchetche akipambana na mabeki wa Spice kugombea mpira
 
Back
Top Bottom