Mapenzi

Mapenzi

Kama unamchukia si ukae mbali nae msionane, ya nini kuwa karibu na mtu unayemchukia?
 
Namchukia baba wa mtoto wangu nifanyeje

1)una sababu gani za msingi zinazokufanya umchukie mzazi mwenzio?
2)je huyo baba wa mtoto ni mume wako au mmezaa tu mtoto kwa bahati mbaya hamkudhamiria?
3)kwani yeye anakuchukia ? au anajua kwamba wewe unamchukia??
4)je ulikuwa na malengo yoyote ya baadae na huyo baba wa mtoto?
5)mtoto ana umri gani?
6)umepata mwingine unayempenda zaidi?
7)unapenda mungu akikujalia uwe na watoto wangapi na je kwa sasa unao wangapi?
8)je ungependa kuwa na familia ambayo kila mtoto ana baba yake?
9)je unafahamu madhara ya kuzaa kila mtoto na baba yake?
10)je una mikakati gani ya baadae juu ya huyo mwanao?
11)na je ungependa huyo mwanao alelewe na mama wa kambo endapo atachukuliwa na baba yake mtakapoachana?
12)je ungependa mwanao alelewe na baba wa kambo endapo mtaachana na huyo baba yake na wewe ukaolewa na baba mwingine?
13)ni muda gani toka umeanza kumchukia?
14)ulipoanza nae uhusiano ni nini kilikuvutia kwake zaidi?
15)mapenzi yenu yamedumu kwa muda gani?
16)ulipoanza nae uhusiano ulikuwa unampenda au kuna kitu kilikuvutia ambacho kwa sasa hakipo tena ndo mana unamchukia?
17)je una dalili zozote za ujauzito?
18)je mnasaidiana kumtunza mtoto?
19)hali yake kiuchumi imekua zaidi au imeshuka au iko kama zamani?
20)kitu gani kilikuvutia kwake mlipokuwa mnaanza mapenzi mpaka ukamkubalia kuwa naye?

jibu maswali haya ndo tutajua una tatizo gani haswa,mana umesema unamchukia baba wa mtoto bila hata kutoa sababu, sasa unategemea utashauriwa nini wakati watu hawajui chanzo cha tatizo lako?mana matatizo mengine ni ya kisaikolojia yanahitaji counselling kidogo tu.
 
Back
Top Bottom