Mapenzi yanavyochangia watu kuua na kujiua

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,320
11,323
IMEKUWA ni jambo la kawaida kusikia ama kushuhudia mtu akiamua kujitoa uhai ama kumtoa uhai mpenzi wake kwa sababu ya mapenzi siku hizi.

Katika visa viwili vikubwa vya wiki chache hizi, moja huko mkoa wa arusha mwanamume kamfumania mpenzi wake na mtu mwingine alichofamya akawachoma moto wakiwa hai, na tukio lingine ambalo liko kwenye vichwa vingi vya habari leo huko mwanza, mume amempiga risasi mkewe na badae mume akaamua na yeye ajimalize japo chanzo hakijajulikana lakini hapo kwa haraka haraka unaweza kua ushajua sababu.

Wataalamu wanasema baadhi ya watu huandika ujumbe wakieleza kwamba waliamua kujitoa uhai baada ya kushindwa kuvumilia maumivu ya penzi walilotarajia lingewatuliza moyo lakini mambo yanakuwa kinyume.

Kiragu Paul, mwanasaikolojia na mtaalamu wa masuala ya mapenzi katika kituo cha Maisha Mema jijini Nairobi, anasema watu hujiua kwa sababu mapenzi huvuruga akili za mtu kabisa.

Mtu huanza kwa kufanya vitendo visivyo vya kawaida, anachanganyikiwa, maisha yote yanakuwa magumu kwake hata anashindwa kulala.

“Kinachoweza kumfanya mtu amuue mtu mwingine, ni kwa sababu amekubali kutoa moyo wake na maisha yake kwa mtu mwingine ambaye hajali.”

“Mapenzi ni kugawana maisha kati ya watu wawili. Na ndio maana tunasema mapenzi ni hisia kali. Ina maana mtu huwa kisaikolojia, ameathirika katika mambo yote, kiroho na kiakili pia. Unapoamua kumpenda mtu umeamua kifo. Ndio maana wanasaikolojia husema mapenzi yana nguvu,” asema Bw Kiragu.

Kulingana na mwanasaikolojia huyu, ni walio na mapenzi ya dhati wanaoathirika kiasi cha kuua au kujiua, wakihisi kusalitiwa.

“Ibainike kwamba penye penzi la dhati, pana wivu na hisia za usaliti zinapotokea, ni rahisi kifo kutokea,” asema.

Mtu anapoingia kwenye mapenzi, aeleza Bw Kiragu, huingia kwenye agano, ndio maana mtu husema amekufa kwa ajili ya mwingine.

Anasema mapenzi yanapoenda mrama, mtu hukosa utulivu wa moyo.

Mpende anayestahili

Ili kuepuka mauti kutokana na wivu au usaliti katika mapenzi wataalamu wanashauri watu kuwekeza penzi kwa mtu anayestahili.

“Macho na tamaa visikupotoshe, mengi uyaonayo ni fahari ya macho tu. Kila siku ni vyema ujifunze kutofautisha tamaa ya macho na kifaacho moyoni na maishani,” aeleza Aisha Rashid, mshauri wa masuala ya mapenzi katika shirika la Love Care, Nairobi.

Anasema watu wengi wamedanganywa na tamaa ya macho, wakaingia kwenye mapenzi na baadaye kujipata katika hali inayowafanya wasababishe kifo baada ya kuwekeza muda, nguvu na rasilmali zao nyingi kujenga uhusiano. “Hakikisha unayempenda, ni mtu anayeweza kurejesha upendo unaompa. Mapenzi yake kwako yawe yanatiririka sawia na yale unayompa. Hakikisha ukiwekeza mapenzi kwake, naye yupo tayari kwa ajili yako.

Penzi la upande mmoja huzaa matokeo mabaya. Hugeuka mateso makubwa kwako, huumiza moyo kabla ya kusababisha madhara ya kiafya na hata kifo. Omba sana usipoteze dira kwa sababu ya mapenzi,” asema Bi Rashid.

Unaweza kuteseka na kuishi na maumivu yasiyomithilika kwa sababu ya matendo ya yule unayempenda.

Duniani kuna watu wabaya hivi kwamba kadiri unavyomuonyesha mwenzio mapenzi, ndivyo na yeye anavyozidisha maringo ambayo hukusababishia maumivu makali sana moyoni.

Lakini Rhoda Akinyi anasema hawezi kujiua kwa sababu ya mapenzi.

Hawajui mapenzi

“Wanaoua kwa sababu ya mapenzi hawajui kuogelea kwenye bahari hii. Mwache na umsahau mwenzio akikutema. Uhai ni muhimu kuliko mapenzi,” aeleza na kutaka wachumba kutafuta ushauri badala ya kuchukua hatua za kikatili.

Bi Rashid aeleza kwamba hulka ya watu kunywa sumu, kujitia kitanzi au kujiangusha kutoka maghorofani kwa sababu ya mapenzi zinatokana na usaliti wa mapenzi.

“Inatokea kwamba mpenzi anamsaliti mwenzake na kumdharau pengine kwa sababu amepata mwingine anayehisi anamfaa zaidi na kusahau alikotoka na wa kwanza. Kuna uchungu ambao wengi hushindwa kuuvumilia na kuamua liwe liwalo,” akasema. Anaongeza kuwa kwa kawaida, kujiua au kuua mtu kwa sababu ya mapenzi sio suluhisho kamwe.

“Watu wanaofikiria kujiua kwa sababu ya mapenzi wanapasa kujiuliza faida ya kufanya hivyo. Jiulize ikiwa ulipozaliwa ulitarajia kukutana na mtu kama huyo duniani na uelewe kwamba kuna watu wanaokujali zaidi ya huyo anayekufanya utake kujiua ambao utawaumiza sana kwa hatua yako,” anasema.

Wazuri zaidi

Bw Kiragu anasema huwa anawashauri watu wanaofikiria kujiua kwa sababu ya mapenzi kufahamu kwamba kuna wanaume na wanawake wengi duniani wazuri kuliko wanaowasononesha kiasi cha kutaka kuwaua au kujitia uhai.

“Ukweli wa mambo ambao watu wengi wanapasa kujua ni kwamba mapenzi ya dhati ni yale yasiyo ya kuumizana, akikuumiza basi ujue hana mapenzi na wewe na kwa hivyo hakuna haja ya kujiua kwa sababu yake,” anasema.

Kulingana na mtaalamu huyu, kujiua kwa sababu ya mapenzi huonyesha kiwango cha juu cha ukosefu wa ukomavu wa kiakili na hata kiroho.

“Ukijiua, mwenzako ataendelea kuishi, haitakupa furaha wala ushindi kwa sababu utakuwa umekufa. Kuua na kujiua ni dhambi na unaweza kujipata ukiteseka jela kwa maisha yako yote kwa kuua pia,” akasema Bw Kiragu.

Broken-Heart-Boy-put604desi49.jpg

boy-and-girl-broken-heart-graphic.jpg
 
ivi mbona sijawai sikia mwanamke kamuua mumewe kisa kamfumania ama yeye kuamua kujinyonga kisa mapenzi


ni kwamba hatupendi kama wanaume?
au we are strong ?
au ni wavumilivu sana?
 
ivi mbona sijawai sikia mwanamke kamuua mumewe kisa kamfumania ama yeye kuamua kujinyonga kisa mapenzi


ni kwamba hatupendi kama wanaume?
au we are strong ?
au ni wavumilivu sana?
Sababu.moyoni mnajua its normal kwa mwanaume kutoka nje. Kwa jinsi tulivyoumbwa but kwa nyie ni tofauti.
 
Hilo tukio la Mwanza mm Niko karibu tu na sehemu tukio lilipo tokea inasemekana ni kitendo cha mwanamke kutomsikiliza mumewe alipomwambia arudi huko alikokua ambako ni harusini japokuwa mke alitihi sauti ya mumewe na kumtaka radhi na kurudi nyumbani na kumkuta mwanaume akiwa na hasira na kuamua kufanya kitendo hicho cha ajabu
 
Hilo tukio la Mwanza mm Niko karibu tu na sehemu tukio lilipo tokea inasemekana ni kitendo cha mwanamke kutomsikiliza mumewe alipomwambia arudi huko alikokua ambako ni harusini japokuwa mke alitihi sauti ya mumewe na kumtaka radhi na kurudi nyumbani na kumkuta mwanaume akiwa na hasira na kuamua kufanya kitendo hicho cha ajabu
Duh kumbe
 
Ndiyo maana Mimi swala LA kuuruhusu moyo wangu kumpenda mtu nalipiga Vita vibayaaa sina elements zozote za kupendaa hata km unajijua wewe mi ndiyo mpnz wako unapoteza muda wako na Mimi.....
..mapenziii hahaaa nayasikiaga tu kwa watuuu
 
ivi mbona sijawai sikia mwanamke kamuua mumewe kisa kamfumania ama yeye kuamua kujinyonga kisa mapenzi


ni kwamba hatupendi kama wanaume?
au we are strong ?
au ni wavumilivu sana?
Tuna opportunities a.k.a fursa nyingi sana katika mapenzi kuliko wanaume
 
Back
Top Bottom