Miriamemmanuel
Member
- Jan 2, 2012
- 43
- 6
MAPENZI YANANITESA NIPENI USHAURI
Nimefikiria kwa muda mrefu naona nazidi kupoteza muelekeo. Naombeni ushauri wenu wa mawazo naweza kufarijika kwani nipo njia panda. Ninampenzi ambaye kwa kiasi kikubwa ninampenda , mwanzao wa mapenzi yetu alinieleza kuwa anampenzi lakini hawawezi kuwa pamoja kwasababu ya imani ya dini zao hivyo uwezekano wakuishi pamoja hautaendelea kuwepo. Mimi nilikubali kwani nilikuwa tayari nimeshampenza sana.
Hivi sasa mimi nina mimba, na yeye ananiambia na yule aliyekuwa mpenzi wake pia ana mimba sikujali. Tatizo lilokuwepo kila siku ananilazimisha nikatoe mimba mimi nimemwambia sipo tayari kufanya hivyo kwani mimi nina kazi yangu nimemwambia sitamsumbua lakini haelewi anatafuta mpaka watu waje wanishauri nikatoe. Pia ananiambia hataweza kuwa na mm bora aendelee na mpenzi wake wa mwanzo. Naombeni ushauri nifanyaje kwani bado nampenda sana.
hapo kwenye red, panaonyesha wazi kuwa huyo mpenzio hana mpango kabisa wa kuwa na wewe ingawa wewe unampenda. Inaoneka aliaanzisha mahusiano na wewe kwa faida zake mwenyewe na siyo ugomvi wa tofauti za kidini kama alivyokwambia.
Mimba yako anaona inaweza ikamsababishia yeye agombane na mpenziwe wa zamani hali ya kuwa hana mpango wa kumuacha (which is logic-si busara kumuacha mpenzi wa zamani bila sababu ya msingi,wakati tayari ameshampotezea muda)
cha msingi nafikiria uanze mapema kujipanga kujihudumia mwenyewe na mtoto wako, suala la kutoa mimba ni hatari kwani unaweza kupoteza maisha, na pengine yumkini ulipangiwa kuwa na mototo mmoja ambaye ndiyo huyo unayemuua.
Tafakari.
Una miaka mingapi??
Naona ni suala la umri zaidi hili.
Yaan dada angu imeniuma sana,kwann ameamua kukupotezea muda lakini daah anyway we mimba uctoe wala nn, cha muhimu jipange upya lea mimba yako na Allah atakutangulia, na hyo mwanaume mwnyzmungu atampa malipo yake inshaalla!h!
mmmh,jisemee nafsi yako tu.una uhakika gani kwa hayo niliyopigia mstari mwekundu?wanaume ni wanaume tu1. Dada zangu wengi hufanya makosa ya kiufundi wakidhani ukizaa na mtu ndio utakuwa nae daima.
2. Mtoto ni muhimu sana katika maisha,maadamu Mungu kakujalia,utunze mimba,mtoto ni asset yako ya baadae ila habari
ya maendeleo ya mimba na mtoto usiache kumjulisha baba yake hata kama ni jambazi wa roho changa(mimba)
3. Usitoe mimba...labda kama umechoka kula chips na mayai na unatamani KIFO.
4. Mwisho wanaume wengi ukituondoa sisi wa JF ni waongo sana. Hizo ni mbinu za uwindaji.....ALIKUDANGANYA. Lakini
hata wewe ulishawahi kudanganya......ndio hali ilivyo na maisha yanaendelea.
USITOE....USIGOMBANE NAE.
Kwa uzoefu wangu finyu wa forums nimegundua wadada wanasema sana kuwa wanaume ni waongo. Pia tena kwa mda ule mfupi nliokaa vijiweni nikaambiwa sana kuwa wanawake ni waongo. Sasa nikaconclude both of them r liers! tusinyoosheane vidole coz najua dada yetu kadanganywa na hata akija m2 kanishikia panga hapa ntazidi kusisitiza kuwa na yeye alimdanganya jamaa pia kwenye mambo kadha wa kadha. Uctoe mimba(ni kuua kwa kukusudia kabisa-tena macho makavuuu! na huyo kiumbe unayemuua hana hata uwezo wa kupiga kelele kuomba msaada), lea mtoto. Its not over- na he who laughs last laughs the best! Yani huko baadae nna uhakika wewe ndo utacheka wa mwisho. Best of lucks!mmmh,jisemee nafsi yako tu.una uhakika gani kwa hayo niliyopigia mstari mwekundu?wanaume ni wanaume tu
1. Dada zangu wengi hufanya makosa ya kiufundi wakidhani ukizaa na mtu ndio utakuwa nae daima.
2. Mtoto ni muhimu sana katika maisha,maadamu Mungu kakujalia,utunze mimba,mtoto ni asset yako ya baadae ila habari
ya maendeleo ya mimba na mtoto usiache kumjulisha baba yake hata kama ni jambazi wa roho changa(mimba)
3. Usitoe mimba...labda kama umechoka kula chips na mayai na unatamani KIFO.
4. Mwisho wanaume wengi ukituondoa sisi wa JF ni waongo sana. Hizo ni mbinu za uwindaji.....ALIKUDANGANYA. Lakini
hata wewe ulishawahi kudanganya......ndio hali ilivyo na maisha yanaendelea.
USITOE....USIGOMBANE NAE.