Jumapili njema wakuu tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha tena kuiona siku njema machoni pa Mungu. Mungu ni mwema wakati wote
Mada kuu:
Mimi nina mpenzi wangu wa kike nimekuwa naye kimahusiano kwa muda mrefu toka mwaka 2018 mpaka sasa lakini sijawahi kufanya naye mapenzi.
Nimejaribu kumshawishi mara kadhaa lakini amekuwa haeleweki muda mwingine anakwambia muda bado hajaupata na akisha upata ataniambia, mimi nabaki najiuliza siku huo muda akiupata mimi nitajuaje? Au ataniambia?
Kuna baadhi ya vitu vyangu kashatumia na baadhi ya zawadi nimeshampa lakini yeye kutoa ananibania na mpaka sasa sijajua tatizo nini, lakini huwa ananipa muda wake tuna piga story kama kawaida.
Kuna siku alisema wanaume wana kasumba ya kutaka wakuchezee halafu wanakuacha; sasa hii point ipo kichwani mwangu au anahisi atakapo nitunukia papuchi nitamtema?
Alinithibitishia kuwa ananipenda hata tukiwa tunatembea ananishika sehemu za mwili wangu hata kukumbatiana huku tukiwa tunatembea, lakini bado ana wasiwasi kuwa mimi yaweza kuwa nina mtu mwingine sababu wanaume hatuaminiki wakati mi mwenyewe nipo kama nilivyo.
Kusudi:
Mpaka sasa sijajua huyu mpenzi ana maana gani mpaka sasa.
Je, yupo katka kunichunguza?
Au mimi ndo sina mbinu za kumshawishi?
Au ananipima kama nina mapenzi ya dhati kwake?
Bin Shaib Classic 2020
Sent using
Jamii Forums mobile app