Mapenzi ni kitendawili

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Hapo za mani za kale Prisca alikutana na Kwesi raia wa Ghana lakini wazazi wake walikuja Tanzania kama waajiriwa wa UN. Kweli ni kijana smart mno. Alipata shahada ya kwanza ya uzamili katika masomo ya fedha na uchumi akiwa na miaka 25. Hakutaka kufanya PhD alisoma tena shahada ya pili ya kodi na mapato. Kwesi aliajiriwa na Investment Bank. Zile kazi za milioni 20-15 kwa mwezi.

Kweli alisafiri sana kazi yake inaweza kumpeleka Columbia kwa miezi sita. Baada ya hapo atachukua holiday wiki mbili anapelekwa Johannesburg kwa miezi sita. Kwa kifupi alikuwa anabadilishwa nchi kila baada ya miezi sita au mitatu. Lakini kila alikokuwa alimtumia Prisca milioni tatu za kujikimu kila mwezi kama mpenzi wake kwakua Prisca alikuwa bado mwanafunzi pale UDSM.

Ndoa ilikuwa ngumu kati ya Pirsca na Kwesi kwakua wazazi wa Kwesi walimtaka aoe binti wa ki Ghana. Walisahau kuwa hawako Ghana na Kwesi ni mtu wa kusafiri mno. Baba Kwesi kidogo alikuwa hana tatizo lakini mama hakutaka hata kumzoea Prisca hasa pale Kwesi alipomuomba amfundishe Prisca kupika michuzi ya ki Ghana.

Prisca ni msichana mrembo, walikubaliana na Kwesi watabaki marafiki. Prisca alikutana na Lyimo na kufunga ndoa Kwesi akiwa Ujerumani kazini. Miaka miwili imepita Prisca alikutana na Kwesi Mlimani City.

Kwesi machozi yalimtoka kumuona Prisca. Walitafuta mahali wakakaa na kuanza kuongea. Wazazi wa Kwesi walisharudi Ghana. Kwesi hakuwa na ajira na kwakua haelewani sana na mama yake aliamua kuja Tanzania akitafuta kazi. Kuna mama alifahamiana na wazazi wake alimpa guest wing akae.
Prisca alianza kumsaidia Kwesi laki tatu, mbili mpaka tano akipata. Sikunyingine alimuomba Lyimo pesa ili amsaidie Kwesi. Baada ya miezi sita Kwesi alipata ajira Addis na kuondoka.

Mapenzi na kitendawili.
 
Last edited:
Episode ya pili ya hadithi yako itatoka lini bibie Sky Eclat ??
Hongera kwa utunzi!!
 
Yaani umekaa nayo moyoni ukaona haitosshi hadi uje utusimulie kama watoto wa darasa la tatu,
Sawa sasa hadithi yako inatufundisha nini???
 
Yaani umekaa nayo moyoni ukaona haitosshi hadi uje utusimulie kama watoto wa darasa la tatu,
Sawa sasa hadithi yako inatufundisha nini???
Huwezi kuifahamu kesho yako
 
Reactions: lup
Kuna Mdada alikataa kila mwanaume aliyetaka kufunganae ndoa kisa ana jamaa yake wameahidiana kufanya hivyo ambaye yupo Urusi kikazi. Jamaa aliporudi kumbe alishatafutiwa mchumba na wazee wake akaoa akasepa kurudi Urusi, Mdada akaachwa njia panda. KWELI MAPENZI KITENDAWILI
 
Huyo hakuwa rizki yake. Mapenzi ni kitendawili Kwesi akimpenda Prisca kwa moyo wake wote lakini siye aliyeandikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…