Mapenzi kwangu ni...

Mapenzi kwangu ni...

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
35,768
Reaction score
86,455
Mapenzi kwangu ni uchoyo!
Ndio ni uchoyo kwa maana ni nafasi ya kuwanyima wengine na kumpa yule special wako ambae ndio kiberenge wa moyo wako!.

Mapenzi kwangu ni utimilifu, utimilifu wa kimaumbile baina ya me na ke. Utimilifu ambao huongozwa na ukiherehere wa hisia tamanishi, hisia zenye kutaka yule kilamba mwiko wa rohoni ndio azitulize na kuzijali kama pengo la mtoto linapoota jino..

Mapenzi kwangu ni ujali, kujali si lazima kuombwa huja tu automatic kama chafya ya afya!..

Mapenzi kwangu ni wivu!, wivu kwa maana ya kuwa na tamanio la husuda kutaka kujua kikomba mboga wangu ana dukuduku gani juu ya huba langu..

Mapenzi kwangu ni nipe nikupe!, sote kwa nafasi zetu tuwajibike kupeana kile ambacho embe ng'ong'o wako hana au anauhitaji nacho.

Mapenzi kwangu ni mikwara! Ndio ni mikwara ila isiyokata ngwara! Lazima tupime maji kwa mikwara mbalimbali ili ujue huyu kinyeramumo wangu je, Ni kiasi gani nipo kwenye limoyo lake!.. mapenzi yasiyo mikwara ni sawa na mapengo yasiyowasha!

Mapenzi kwangu ni muda! Yes ni muda maana muda ndio ujali, uchoyo kwa wengine na kumpa yeye, mikwara, nipe nikupe n.k bila kumpa muda komamanga wa moyo wako ni sawa na kutaka kuendesha gari bila nishati elekezi!

Kwangu ni hayo tu, kwako je mapenzi ni nini..?
Kuna mjomba huku kwake mapenzi ni kuzima Netiweki..
 
We kiberenge asubuhi yote hii unawaza mapenzi? 😀

Hebu jiandae huko kwenda kuwangalia mabingwa wa Taifa, SSC 😎
Sasa Kama asubuhi tu nimepikiwa maji ya kuoga unataka nizungumzie nini..? 😂 Na hapo nimepewa ujumbe huku akitabasamu ati "leo jiandae nitaifinyia kwa ndani!!" Halafu mtoto jicho remburembu utafikiri kile ki retina sijui kinataka kudondoka.. hebu niwache na asubuhi yangu pana..🤣
 
Kuna gesti nimelala mashuka yake yananuka matope. Siyo matope gogo matope matope.

Anyway make sure haulali gesti ipo Mwembeyanga jina linaanzia Es room namba 15.

Ningekua na mdada sijui km ningeweza kuperform.
 
Mapenzi kwangu ni mauzo ninapo uza mali au bidhaa fulani basi nakuwa mwingi wa furaha
 
Sasa Kama asubuhi tu nimepikiwa maji ya kuoga unataka nizungumzie nini..? 😂 Na hapo nimepewa ujumbe huku akitabasamu ati "leo jiandae nitaifinyia kwa ndani!!" Halafu mtoto jicho remburembu utafikiri kile ki retina sijui kinataka kudondoka.. hebu niwache na asubuhi yangu pana..🤣
😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom