Mapenzi kwa mwingine msaada anakuja kuomba kwangu.

The Donchop

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
294
Reaction score
381
Habari za leo?
Jamani nina tatizo. Aliyekuwa mpenzi wangu ambaye ndiye aliniacha kwa kunichoka sasa amepata mwanamke mwingine.
Kupata kwake mwanamke hakuniumizi lakini kinachonishangaza ni tabia yake ya kupenda kuwasiliana nami na kunitafuta kila anapopata shida.
Mwanzo nilijitoa kwake kwa mapenzi ya dhati. Tatizo lake nililibeba kama langu na nikahangaika nalo mpaka nipate suluhu.
Nilitambulika kwao na tuliongelea swala la kuachana na mtoto wao maana ilikuwa ni kesi hadi iliyowahusisha wazazi.
Ndugu na wazazi wake walinishauri kujitenga nae kwasababu amekuwa mlevi na anabadilisha wanawake kupitiliza.
Kweli nimeachana nae kiroho safi na hata ikitokea nimempigia basi ni kweli ni jambo la lazima kumpigia. Ila mwenzangu kila anapopata tatizo ananitafuta mimi. Leo alipata shida ya kipesa, akanipigia simu na kunieleza. Kiukweli sio kwamba sikuwa na hiyo pesa na sio kwamba simuonei huruma lakini nahisi tu kuwa anapojisikia kufanya starehe zake ndipo anakuja kuniomba msaada. Nimeamua kufuata ushauri wa ndugu zake kuwa nisikubali akanitumia namna hiyo unless ni kweli yupo kwenye shida.
Ndugu zangu, ninakosea wapi?
 
upo sahihi, lakini tumeumbwa na mikono miwili ili mmoja utumike kumsaidia mwenzako, cha msingi, msaada usizd uwezo
 
Mh nahc kama bado unampenda vile jamn

Ni ngumu sana kuacha mawasiliano na mtu uliyemzoea lkn tafuta njia ya kujiweka mbali nae amasivyo utakutumia atakavyo na unaweza potezea mda wakati huo yake yajiendea
 
Kama hampendani mnawasiliana ili iweje? Mblock uendelee na mambo yako. Kuwa busy na maisha yako. Mahusiano yana milima na mabonde, busara zenu zinatakiwe zitumike kusolve matatizo yenu. Kama bado mnapendana na mmoja yupo legelege, hayo ni matokeo yake. Mnahitajiana lakini hamuwezi kutumia akili kusuluhisha.
 
upo sahihi, lakini tumeumbwa na mikono miwili ili mmoja utumike kumsaidia mwenzako, cha msingi, msaada usizd uwezo
Mkuu kwa jinsi scenario inavyojieleza nahisi huyo jamaa anamfanya binti atm coz anajua alimpenda sana na alijitoa sana kwake. Kinamshinda nini kuomba msaada kwa girl wake mpya hadi amfate wa zamani kila mara?
 
Yani mwanamke mzuri anapataga mwanaume kichaa sikiliza mtaftie RB
 
Hujakosea ila nakumbuka kuna mwanaume mmoja wa hata use na shida gani haoni hasara kukupa pesa
 
Hata kama mimi ningekuwa ndugu yako ningekushauri the same. Sio kwamba usimpe msaada, ila the way alivyo na tabia yake,unaona kabisa licha ya kuachana nae amekugeuza wewe kuwa atm yake. Tangu mwanzoni ungefunga milango.
 
😀Aiseeee kumbe wapo wanawake wanaochunika nilifikiri sisi wanaume tu hupigwa vizinga.
 
Habari za leo?
Jamani nina tatizo. Aliyekuwa mpenzi wangu ambaye ndiye aliniacha kwa kunichoka sasa amepata mwanamke mwingine.
Kupata kwake mwanamke hakuniumizi lakini kinachonishangaza ni tabia yake ya kupenda kuwasiliana nami na kunitafuta kila anapopata shida.
Mwanzo nilijitoa kwake kwa mapenzi ya dhati. Tatizo lake nililibeba kama langu na nikahangaika nalo mpaka nipate suluhu.
Nilitambulika kwao na tuliongelea swala la kuachana na mtoto wao maana ilikuwa ni kesi hadi iliyowahusisha wazazi.
Ndugu na wazazi wake walinishauri kujitenga nae kwasababu amekuwa mlevi na anabadilisha wanawake kupitiliza.
Kweli nimeachana nae kiroho safi na hata ikitokea nimempigia basi ni kweli ni jambo la lazima kumpigia. Ila mwenzangu kila anapopata tatizo ananitafuta mimi. Leo alipata shida ya kipesa, akanipigia simu na kunieleza. Kiukweli sio kwamba sikuwa na hiyo pesa na sio kwamba simuonei huruma lakini nahisi tu kuwa anapojisikia kufanya starehe zake ndipo anakuja kuniomba msaada. Nimeamua kufuata ushauri wa ndugu zake kuwa nisikubali akanitumia namna hiyo unless ni kweli yupo kwenye shida.
Ndugu zangu, ninakosea wapi?
yan we ndo tajili yake au? au yeye kiwete?
 
Unless ni kweli yu kwenye shida...sasa utajuaje....kama ni kweli au si kweli...we amua tu moja
 
Habari za leo?
Jamani nina tatizo. Aliyekuwa mpenzi wangu ambaye ndiye aliniacha kwa kunichoka sasa amepata mwanamke mwingine.
Kupata kwake mwanamke hakuniumizi lakini kinachonishangaza ni tabia yake ya kupenda kuwasiliana nami na kunitafuta kila anapopata shida.
Mwanzo nilijitoa kwake kwa mapenzi ya dhati. Tatizo lake nililibeba kama langu na nikahangaika nalo mpaka nipate suluhu.
Nilitambulika kwao na tuliongelea swala la kuachana na mtoto wao maana ilikuwa ni kesi hadi iliyowahusisha wazazi.
Ndugu na wazazi wake walinishauri kujitenga nae kwasababu amekuwa mlevi na anabadilisha wanawake kupitiliza.
Kweli nimeachana nae kiroho safi na hata ikitokea nimempigia basi ni kweli ni jambo la lazima kumpigia. Ila mwenzangu kila anapopata tatizo ananitafuta mimi. Leo alipata shida ya kipesa, akanipigia simu na kunieleza. Kiukweli sio kwamba sikuwa na hiyo pesa na sio kwamba simuonei huruma lakini nahisi tu kuwa anapojisikia kufanya starehe zake ndipo anakuja kuniomba msaada. Nimeamua kufuata ushauri wa ndugu zake kuwa nisikubali akanitumia namna hiyo unless ni kweli yupo kwenye shida.
Ndugu zangu, ninakosea wapi?
Mwanza kwema? Haaaah haaah
 
Back
Top Bottom