Mapenzi kwa mwanangu yaliniondoa Maskani

Mapenzi kwa mwanangu yaliniondoa Maskani

Mjani huwa unanipa ,mzuka sana..akili huwa inatulia sana!!
 
Kwahyo mkeo alimtupa mwanao barabarani Alaf akarudi nyumbani..ye ndo alikuwa anamhudumia!?? NEVER MAKE SENSE!!!!
 
Wahenga husema ujana maji ya moto, japo sijui kuni na sufuria ni nini na nini kati ya uzee na utoto.

Mwaka 2007 tarehe kama ya leo, mida ya saa kumi na moja nikiwa natoka kwa "mchomeshaji" kupata dawa na machozi ya simba narejea nyumbani.. Nilikua nimetinga na mkononi nina chupa ya konyagi ambayo nilikua nimeijaza gongo, njiani nilimuona mtoto mdogo akiwa barabarani (barabara kuu ya songea-dar, wakati huo ndo nilikua nimeajiriwa kijiji Fulani huko songea) kwakua nilikua stimu niliingiwa na huruma ya ghafla sana nikatia chupa mfukoni na kumuokota yule mtoto.. Maskini MUNGU sio Afande Sele yule mtoto mdogo alikua ni mwanangu wa miezi mitatu.. Nakumbuka nililia sana, nililia mpaka stimu zote zikapotea kichwani.. Nilimkumbatia mwanangu mpaka home, ile nafika home namkuta mama wa mtoto wangu analia sana, nikiwa nimemkumbatia mwanangu nikaanza kumuhoji nini haswa kisa cha kutaka kumuua mwanangu nikaambiwa kwanza yeye alishajua mtoto kakanyagwa na gari.. Lakini akaniambia chanzo haswa ni tabia yangu ya kutomsikiliza yeye na kutotaka kulea malaika yule.

Niliishiwa sana nguvu, na sikujua nimfanye nini yule mwanamke.. Nilitamani kumzibua.. Nilitamani kumchinja.. Lakini uwoga ulinijaa sana sikuweza kufanya lolote kwa wakati ule.

Kiukweli mama wa mtoto huyu alinifundisha mambo mawili makubwa sana.. Kwanza alinipa nguvu ya ajabu ya kuacha kukaa maskani na kula majani (pia ndiye aliyenifanya niache kabisa fegi toka siku ile) lakini pia alinifundisha kuyavaa majukumu kisawasawa ambayo pengine nilikua nayaogopa au nilikua sijisomi kama nimekua dingi sasa. (Bahati mbaya huyu mwanamke nilishatemana nae)... Siku ile niliapa siendi tena maskani kula ganja wala kunywa gongo, badala yake nigejiwasha na kujilipua nyumbani kwangu tu.

Leo hii niliamua kurudi maskani kujiwasha (hasa ukizingatia wanangu wapo likizo kwa shangazi yao).. Nilienda kwa sadari wangu kipenzi sadari mwajuma, akanipikia kwanza dona ndondo, samaki na majani ya maboga.. Baada ya kukandamiza menu sadari akanipa Vichwa vya ganja nichambue mwenyewe na hii ni kwakua nimemfurahisha kula dawa maskani kwake, nimejiwasha sanaaaa.. Ila walitokea madogo kama watatu hivi hawa watoto nina uhakika bado wapo shule, tena o-level, wamekula bomba moja afu wakaanza kuzingua sanaaaa, mmoja wao ndo kwanza anaonekana anajifunza kupuliza, nimesikitika na nimewaambia ukweli hawatakiwi kubweteka kijiweni, wasake life.. "kula msuba, kafanye yako" kauli ambayo baba yangu alipenda sana kuniambia alipogundua nimeanza kuchoma.

My take, wadogo zangu mnaoshinda maskani 24/7 punguzeni sasa, jitahidini mtafute life lenu na mta-enjoy sana... Cha ukucha kwa sadari sio mpango wala nini, kula dawa tambaa.
Afadhali umejileta mwenye coz wakati tunakataza matumiz ya bangi wewe unafanya matangazo huku. Kesho tukutane central
 
Kweli ganja si mchezo songea kuna barabara ya songea - Dar. Songea kuna barabara ya songea - njombe
 
Kushi tulishanyonga sana maskani kwa machigu hainaga kwere arifu.

Ila tuwape somo machalii waache kupemesa unga tule majani.

Nitembezee ninja nikiwashee nipo arosto kinyama.
 
Afadhali umejileta mwenye coz wakati tunakataza matumiz ya bangi wewe unafanya matangazo huku. Kesho tukutane central
Muwege mnaangalia cha kumtia mtu bangili..kete mbili wanagonga nyundo, wezi wa Mali za umma wanatanua mtaani.

Umenikumbusha ya bashite na sepengaaa.
 
Mwanzo nililua nakusoma nimefka kat kat Kila nikianza kukuelewa aya ijayo unanipoteza, kwa ufupi nimefka mwisho wa stori yako nimeshndwa kuelewa mwisho wako hasa ulikuaje, japo inaonesha hujaacha ila labda umepunguza
 
Back
Top Bottom