Mapenz na ndoa ya kulipa fadhila!!

Mapenz na ndoa ya kulipa fadhila!!

mutahappy

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2012
Posts
529
Reaction score
188
Heshima wana JF;
Hil jambo la kulipa fadhila kwa kuingia katika mahusiano na mhisan au kuamua kuoa/kuolewa mhisan japo humpend lakin kisa alikusaidia jambo fulan maishan.

Kuna dada mmoja rafik yangu ameingia katika mgogoro wa hil suala na kulipa fadhila kimapenz.
Mama yake katika biashara zake alikutana na kijana katika biashara zake ambae alimsaidia sana.
Kutokana na msaada alioutoa kijana huyo kwa mama, mama akampenda na kuja nae home ambapo alikutana na huyo bint yake mama.

Kijana akampenda msichana na kutupa gia zikapanguliwa zote na bint.kijana akajaribu akashindwa na akaamua kumweleza mama mtu.

Mama mtu akamweleza bint yake amkubal lakin bint akakataa na kusema anamtu wake anaempenda

sasa mama mtu kachachamaa na kudai lazima aolewe na huyo kijana b'coz ni kijana mzur na amemsaidia sana na hiyo ndo njia ya kurudisha asante kwa huyo kijana,

mdada wa watu kila siku ,analia hamtak huyo kijana, anampenz wake lakin mama yake ndo kakomaa na hatak kuelewa chochote zaid ya kuona ndoa na bint anampenda mama yake na hatak kumuudh mama yake ila hayupo tiyar kuolewa na huyo kijana

Anaomba ushaur wanaJF.

Nawasilisha!
 
Nakusabahi. Mimi niko kwenye ndoa. Mke wangu wakati tukiwa wachumba zamani kiasi alishawahi kulazimishwa kuolewa na kijana kisa eti ni kabila moja na wao! Alilazimishwa sana na mama yake lakini alikataa kata kata.

Ushauri
Mapenzi hayalazimishwi wala sio fadhila. Nashauri binti aache kulia kwanza, anaweza kushirikisha ndugu wa karibu kama kaka, dada, baba* ambao wanaweza kumpa ushauri na kuwaweka chini na mama.

Pia huyo kijana atafutwe na aelezwe ukweli ili asiharibu maisha ya wengine.

Tatizo la approach hii ni kwamba kama akikosa support ya ndugu atakuwa katika hali ngumu sana.

Approach ya pili amueleze mchumba wake(ingawa hapa lazima mchumba wake atajisikia vibaya na atakasirika/atamkasirikia mama yake na msichana)

Tatizo hapa kama huyu mchumba hampendi msichana kiukweli au labda ni muoga(anaweza kudhani familia ya msichana ina matatizo etc) anaweza kuamua kuachana na huyo msichana.

Mwisho wa yote alichopanga Mungu mwanadamu hawezi kupangua kamwe! Kama binti hana fikra na huyo jamaa hata afanye nini there won't be any love.

Mama anaweza kufurahisha nafsi yake tu kwa kumuuza binti yake ila ipo siku Mungu atamuadhibu!!
 
Back
Top Bottom