Mapendekezo yangu kwa tume ya katiba mpya

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
Ndugu wananchi;
Mimi napenda kutoa mapendekezo yangu kwa tume ya Katiba Mpya ili kuweza kuona namna gani ya kuyafanyia kazi. Nafanya hivi kwasababu kwasasa nipo nje ya nchi na mimi kama Mtanzania nawajibika pia kutoa maoni yangu katika Tume husika. Najua mengi sana yatachangiwa na Wananchi ili tuweze kuwa na Katiba Bora kabisa inayojali maslahi ya Watanzania walio wengi/watanzania wote na si katiba inayojali maslahi ya kundi fulani dogo la wenye nazo tu wakati wananchi walio wengi wanaumia na kukosa haki hata katika nchi yao. Hivyo napenda kutoa mapendekezo yangu, na ni matumaini yangu na wewe kama Mtanzania utaweza pia kutoa maoni yako hapa hata kabla ya hiyo tume kuanza kukutana na watu.

Hili ni la muhimu sana kwani si wote watakaoweza kukutana na tume moja kwa moja na hivyo utakapotoa maoni yako hapa, then itakuwa pia ni njia nzuri kwasababu Tume pia itaweza kuangalia Maoni ya watu katika vyanzo mbalimbali.

Mapendekezo yangu;
1. Nafasi za uteuzi mbalimbali zinazofanywa na Rais au Waziri mkuu ziweze kuwa na approval ya Bunge kabla ya huyo mtu kuruhusiwa kuhold hiyo post.
2. Pia vigezo vya ki utaalamu vizingatiwe katika teuzi mbalimbali ili kuondoa hali iliyopo sasa ya mtu kuweka mtu kumteua mtu kwasababu ya uswahiba, urafiki, undugu, ukabila,udini, mapenzi, jamaa, n.k bila kujali vigezo vya kiutendaji.

3. Swala la Dini liendelee kuwa la hiari ya mtu husika na si jukumu la serikali kuingilia uhuru wa dini. Na iwekwe wazi kabisa kwamba Dini yoyote pia isiingilie mamlaka ya Serikali. Hili lizingatiwe sana, kwani kwasasa kuna chokochoko nyingi sana za kidini hapa TZ ambazo kwa hakika hazina maslahi kwa Taifa letu.

3. Vyeo hasa katika ofisi nyingi ziangaliwe upya, kwani kuna mkanganyiko mkubwa sana katika utendaji kazi. Hapa nitatoa mfano katika ngazi ya Wilaya/Mkoa. Katika ngazi ya Wilaya/Mkoa kuna vyeo kama vifuatavyo (mtanirekebisha kama nitakuwa nimekosea au kuchanganya-lkn naamini concept imeeleweka.
a. Mkuu wa Wilaya/Mkuu wa Mkoa
b. Mkurugenzi Mkoa/Wilaya
c. Katibu tawala Mkoa/Wilaya
d. Kaimu Mkuu wa Mkoa/Wilaya
e. Kaimu Mkurugenzi Wilaya/Mkoa
f. Kaimu Katibu Tawala/Mkoa
g. n.k

Sasa ukiangalia watu wote hao katika ngazi ya Wilaya na Mkoa utakuja ona kwamba kuna muingiliano wa hasa wa kikazi ( chukua mfano wa Mkuu wa Mkoa/ Wilaya kuwa Mwenyekiti wa Ulinzi wakati kuna OCD na RPC wa sehemu husika.
Tatizo la vyeo hivyo ni gharama ya uendeshaji na nyingi katika vye hivyo ni vya kupeana tu bila kujali utendaji wa mtu, na matokeo yake gharama kubwa sana ya uendeshaji kwa Serikali yetu-ndiyo maana TRA inajitahidi kukusanya pesa lkn Matumizi ni mengi kuliko kinachopatikana. Ninapoangalia gharama za uendeshaji hapa naangalia vitu kama mishahara yao, posho zao, magari, mafuta, wahudumu wao, madereva wao, n.k.

Hapa napendekeza iangaliwe upya na kuona umuhimu wa vyeo vunavyohitajika tu na pia iangaliwe vigezo vya kumpata mhuhusika kama ilivyo sometimes kwa Mkurugenzi.

4. Kinga kwa kiongozi wa nchi iangaliwe upya ndani ya Katiba hii kwasababu wengi wao wanatumiahiyo nafasi na kufuja au kuiba mali za Watanzania huku wakijua kwamba wako chini ya Kinga, hivyo hawatashtakiwa.

5.
6.
7.
Endeleza na wewe mapendekezo yako.

Ahsanteni sana.
RDI.
 
Kuwe na bunge la Tanganyika (Tanzania Bara) kama Zanzibar walivyo na baraza la wawakilishi. Bunge hili lishughulikie masuala yasiyokuwa ya Muungano. Kwa sasa wabunge toka Zanzibar huwa wanaingia kujadili hata masuala yasiyokuwa ya muungano.

Eneo la uwakilishi katika bunge la muungano ambalo litakuwa linashughulikia mambo ya muungano tu, liwe linagawanywa kutokana na idadi ya watu. Si mbunge mmoja toka kahama awakilishe watu 120000 wakati mwingine toka Nungwi anawakilisha watu 5200.
 
Kuwe na bunge la Tanganyika (Tanzania Bara) kama Zanzibar walivyo na baraza la wawakilishi. Bunge hili lishughulikie masuala yasiyokuwa ya Muungano. Kwa sasa wabunge toka Zanzibar huwa wanaingia kujadili hata masuala yasiyokuwa ya muungano.

Eneo la uwakilishi katika bunge la muungano ambalo litakuwa linashughulikia mambo ya muungano tu, liwe linagawanywa kutokana na idadi ya watu. Si mbunge mmoja toka kahama awakilishe watu 120000 wakati mwingine toka Nungwi anawakilisha watu 5200.

Sawa kabisa; hata marekani states zina electoral colleges tofauti tofauti kutegemea na ukubwa, wingi wa watu na nguvu za kiuchumi.
Angalia hii tume ya katiba, watu 15 kutoka zanzibar wanawakilisha wati wasiozidi milion 2 na watu 15 kutoka tanzania bara wanawakilisha watu zaidi ya milioni 40!
 
Back
Top Bottom