Mapendekezo ya Zitto balaa

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC),Zitto Kabwe, amesema kamati yake itatoa hoja ya kuanza mchakato wa kikatiba wa kumvua ujaji, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, jaji Frederick Werema.

Mbali na dhamira ya kutaka jaji Werema avuliwe ujaji pia, Zitto amesema kamati yake itapendekeza watu wote waliohusika katika kashfa ya wizi wa akaunti ya Tegeta Escrow, wachukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufilisiwa mali zao.

Zitto, alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na Tanzania Daima Jumapili, kuhusu sakata la Escrow linaloendelea hivi sasa.

Majibu ya Zitto yalitokana na maswali ya gazeti hili yaliyotaka kujua hatua zitakazopendekezwa na kamati yake baada ya kukamilisha kazi ya kupitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali(CAG), juu ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Alisema kimsingi kilichofanyika katika tukio hilo ni zaidi ya wizi wa kawaida na kwamba wahusika ni vema wakafilisiwa mali zao kisha wachukuliwe hatua nyingine za kisheria.

"Suala hili sio wizi wa kawaida bali ni ‘money laundering'. Kwa hiyo kufilisiwa ili kurejesha fedha hizo ni hatua nyingine itakayopendekezwa"alisema Zitto.

Alisema hatua hiyo itakuwa ni fundisho kwa wengine huku akikumbushia matukio ya wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje(EPA) na sakata la kampuni ya kufua umeme wa Richmond.

Alisema kamati yake bado inaendelea na kazi na kwamba walichogundua ni kuwa fedha zilizokuwa katika akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwa za umma na kwamba kampuni ya Pan Africa Power Resources (PAP) hawakuwa na uhalali wa kuchukua fedha hizo.

"PAC bado inaendelea na kazi. Watu wote ambao wamehusika katika wizi huu tutapendekeza wawajibishwe na kuchukuliwa hatua za kisheria."alisema

Tishio kwa wabunge

Baadhi ya wabunge wanaonekana vinara wa kusimamia suala hilo wanaelezwa kutishia maisha ambapo mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ameshatoa ripoti polisi

Wasiwasi wa usalama wa wabunge hao umeongezeka zaidi baada ya taarifa kuwa mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM), kulishwa sumu akiwa safarini nchini Uingereza

Mkono inadaiwa ndiye anayejua sakata la IPTL kwakuwa kwa muda mrefu amekuwa akishiriki kwenye kesi akisimamia Tanesco na wizara ya Nishati na Madini

Mbunge huyo anadaiwa kuvujisha siri ya uchotwaji wa fedha hizo kwakuwa Wizara ya Nishati na Madini mwanzoni mwa mwaka huu haikuingia makataba wa kuitumia kampuni ya uwakili ya mbunge huyo

Hata hivyo Mkono, mwenyewe mara kadhaa alishakanusha madai ya kushiriki kwenye kuvujisha siri za ufisadi huo wala kuwa nyuma ya sakata hilo.

Chanzo: Tanzania daima
 
Sio wafilisiwe tu wanyongwe kabisa watu wanawalisha sumu wenzao kuwazoofisha na kuwauwa nao wakikamatwa kitanzi hadharani tu
 
Matamu ukisikia yakisemwa,lakini kutekelezwa kizaazaa,haya tunasubiri majina mengine manake kuna nafasi nyengine katolewa ANAERAMBA amewekwa anae KOMBA ndio kamaliza mchezo ...
 
Kuna taarifa kuwa nyaraka mhimu zenye majina ya wahusika zimeibwa?
 
Duuuuuh Kumbe Jamaa wa me poison kwa kua kamwaga Mbona !!!!!!!!!!!!!!!!!!, lakini walimwaga ugali ,
 
Ushirikiano wetu na China unakua sana kwa sasa nadhani watusaidie kutoa mapendekezo ya namna ya kushughulikia tatizo la ESCROW. Si unajua siku zote ukipata tatizo unapata ushauri kwa rafiki wako wa karibu au sivyo?
 
Tumeshaumizwa sana na huu mtambo wa Iptl haswa swala la capacity charges. Natumaini ni wakati muafaka moja ya mapendekezo yatakayoletwa na kamati ya PAC yalenge katika kumalizana once and for good na mtambo huu.
 
We unasema kumaliza once and for good wakati wameshaingia mkataba wa 400m capacity charges mpaka 2033!
 
We unasema kumaliza once and for good wakati wameshaingia mkataba wa 400m capacity charges mpaka 2033!

Hii sasa itategemea na taarifa ya kamati. Kama tulivyosikia hata hizo hisa 70 alizonunua singa hazina uhalali na kutokana na hilo mkataba mzima kati ya tanesco na pap utakua null and void.
 
Ni lazima mkataba uvunjwe kabisaaa, tuondokane na huyu IPTL, hata kama wamesaini tena, kuna kipengele katika mkataba kwamba ikiwa kuna upande utafanya hujuma basi upande wa pili una haki ya kuvunja mkataba.
 
Katika kile kinachoonesha kama kupanic na hofu kwa ripoti ya CAG baada ya kuonesha kuwa hakuna kasoro katika mchakato wa utoaji wa fedha za escrow, Mwenyekiti wa kamati ya PAC ameibuka na kutoa mapendekezo yafuatayo

1.PM KUJIUDHURU KWA KUSHINDWA USIMAMIZI

2.AG AMESAMEHE VAT

3.PROF AJIUZURU KWA KUMLETA RUGEMALIRA

4.MASELE AJIUZURU KWA KUMSHAMBULIA BALOZI.


Katika mapendekezo yake hapo juu Zitto ameonyesha kuweweseka na kile ripoti ya CAG kimebaini kuhusu mchakato wa utoaji fedha za escrow ambazo inasemekana ni malipo halali ya IPTL
 
Haraka za nini, leo si ndo tunajua mbivu na mbichi? Au ni kesho?
 
Wewe ulitaka aseme Mzee wa Tezi aachie ngazi? Wanaotakiwa kuwajibika ni Pinda na genge lake na pesa zirudi. Ningefurahi kama serikali ingevunja mkataba na IPTL mara moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…