Mapendekezo ya Katiba mpya hofu ya CCM imeota mbawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapendekezo ya Katiba mpya hofu ya CCM imeota mbawa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, May 19, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Mapendekezo ya Katiba mpya
  Hofu ya CCM imeota mbawa?

  Godfrey Dilunga

  Toleo la 239
  16 May 2012


  [h=2][/h][h=3]Rais Kikwete Azindua Tovuti ya CCM[/h]

  [​IMG]














  [h=3]Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM[/h]

  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]

  Wajumbe wa Halamashauri Kuu ya Taifa CCM,wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wa White House Mjini Dodoma,wakati kikao cha siku moja kilichofunguliwa na Mwenyekiti wake Rais Dk.Jakaya M.Kikwete
























  MTUNZI wa vitabu mashuhuri vya Treasure Island, Kidnapped na Strange Case of Dr Jekyll and Mr Hyde, raia wa Scotland, Robert Stevenson, aliyefariki Desemba 3, mwaka 1894, alipata kusema usitoe hukumu kwa kupima mavuno uliyopata, bali mbegu ulizopanda.
  Stevenson alisema: “Don’t judge each day by the harvest you reap but by the seeds that you plant
  Kwa kuzingatia mtazamo huu wa Stevenson, tangu Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika mazuri au mabaya yaliyopo nchini msingi wake ni aina ya mbegu iliyopandwa na wanasiasa wa TANU na baadaye, CCM iliyoshirikisha wana-TANU na wana- Afro Shiraz Party.
  Kwa hiyo, kama mavuno yaliyopo sasa nchini ni pamoja na amani na utulivu, kwa namna fulani Stevenson anatuonya kwamba, tujisifu kwa kuegemea aina ya mbegu iliyopandwa na si wingi au uchache wa mavuno.
  Kwa kuzingatia mtazamo huo huo, katika mapendekezo ya Katiba mpya yatupasa kupanda mbegu bora na si kupanda mbegu dhaifu na kisha tukasubiri kushangilia kiwango cha mavuno kisichoweza kupatikana wakati wa msimu wa mavuno.
  Kwa mfano, katika suala la kutafuta maoni juu ya Katiba mpya hatuna budi kutambua kuwa mbegu yetu bora inayopaswa kupandwa ni utaifa. Tukubaliane kimsingi, tunakwenda kupanda mbegu ya utaifa, hakuna nafasi ya kupandikiza ukaskazini, u-CCM, u-CHADEMA wala u-wanaharakati katika Katiba mpya.
  Tunakwenda kuchambua namna utaifa wetu utakavyolindwa kupitia mifumo imara ya utawala usiozingatia utashi pekee wa mkuu wa nchi.
  Na ingawa tunayo matatizo mengi katika masuala ya uongozi lakini kama anavyoeleza mwanafizikia mashuhuri, mzaliwa wa Ujerumani, Albert Einstein kwamba; katikati ya matatizo, ndipo fursa ya utatuzi ilipotuwama (In the middle of difficulty lies opportunity), tujitahidi kutathmini tunakotaka kuelekea kwa kuamini kwamba katikati ya matatizo yetu ya sasa ipo fursa ya ufumbuzi.
  Naam, mapema wiki hii CCM kupitia vikao vyake vya juu imeonyesha nia njema katika kuelekea kuandika Katiba mpya, nia ambayo kwa namna fulani inazidi kuibua maswali zaidi.
  Ndiyo, maswali ni mengi na makubwa kati ya hayo ni je, CCM inakusudia upya kudhihirisha kuwa ni kati ya vyama bora Afrika vinavyomudu kupokea mabadiliko na hata kuiandaa nchi kupokea mabadiliko hayo bila misukosuko?
  Tuliona hali hii mwaka 1992, nchi iliporejeshwa katika mfumo wa vyama vingi katikati ya vuguvugu la mageuzi, bila viashiria vya umwagaji damu na tena, kupitia Mwalimu Julius Nyerere, CCM ikiwatangulia kimsimamo Watanzania wengi waliokuwa wakipinga mfumo wa vyama vingi kwa kuridhia mfumo huo.
  Lakini swali la pili; je, ni kweli baada ya CCM kubaki madarakani kwa miaka mingi sasa inajiandalia mazingira mazuri ya kuendesha siasa kama ikitokea ikapigwa kumbo na kung’olewa madarakani?
  Kuna dalili zinaanza kujionyesha kwamba, CCM kinawapa mtihani wananchi kutafakari upya kuwa kinahitaji kuzidi kupewa fursa kwa sababu kinamudu kuongoza nchi katika misimu migumu ya mabadiliko na fursa hiyo kwa sasa ni mchakato huu wa Katiba mpya.
  Kuna masuala mazito yamependekezwa na vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kuhusu Katiba mpya, ambayo yanaweza kulegeza mioyo ya baadhi ya Watanzania kuhusu ‘busara’ za chama hiki katika kuivusha nchi salama katika misimu migumu ya mawimbi ya mabadiliko nchini.
  Kwa mfano, mapendekezo ambayo yanatajwa kushikiwa bango na Rais Jakaya Kikwete binafsi kwenye vikao hivyo vilivyohitimishwa Jumatatu, wiki hii mjini Dodoma ni kwamba katika Katiba mpya, matokeo ya Rais baada ya Uchaguzi Mkuu yaweze kuhojiwa mahakamani ndani ya muda maalumu.
  Pili, kuitambua ofisi ya Maadili ya Viongozi wa Umma ndani ya Katiba na ofisi hiyo iweke mfumo mzuri wa kiutendaji bila kuibana.
  Haya pamoja na mengne yaliyoamuliwa ni masuala machache kati ya mengi yaliyopendekezwa na CCM ambayo tafsiri yake inaweza kuwa ni mosi, kujiandaa kuwa chama cha upinzani kitakachoweza kusimamia vizuri serikali mpya.
  Pili; kujiundia fursa mpya na ya kipekee kwa kuzingatia kuwa ni chama tawala. Fursa hii inadhihirishwa na mapendekezo yake yanayoelekea kuwashawishi Watanzania kwamba ni chama chenye uwezo wa kuongoza nchi katika misimu migumu ya mabadiliko pengine kuliko hata viashiria vya hovyo vinavyoanza kuonyeshwa na baadhi ya vyama vya upinzani nchini.
  Kwa muda mrefu nchini tatizo limekuwa ni kuporomoka kwa maadili ya viongozi wa umma na hasa baada ya kuhujumiwa kwa Azimio la Arusha lililokuwa likiweka miiko ya uongozi. Kwamba maadili ya uongozi yamekuwa yakidhibitiwa na Rais.
  Pengine sasa, ripoti kwa mfano za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zimetoa uzoefu mzuri kwamba, ni vizuri sasa kujenga mfumo unaoruhusu uwazi zaidi utakaowaumbua wezi na wasio waadilifu mbele ya umma.
  Kwamba kuwaumbua viongozi wasio waadilifu ni hatua moja ya kuwaanzishia safari yao ya hukumu. Jamii inaanza kuwapa hukumu kupitia ripoti ya wazi. Kwa hiyo, katika mapendekezo ya kutaka Tume ya Maadili kuwa zao la Katiba na iwe huru katika mfumo wake wa utendaji ikiwajibika pengine kwa Bunge au kwa umma moja kwa moja, ni jambo zuri na kati ya mapendekezo yanayokipa hadhi mpya CCM.
  Ni jambo ambalo kwa namna fulani linaondoa zile hisia za muda mrefu za viongozi wa CCM kulindana katika ufisadi. Ni kanuni rahisi kuielewa kwamba, tume imara ya maadili ni kikwazo dhidi ya mfumo wa kulindana.
  Jambo jingine ni hilo la kutaka Katiba itambue rasmi mchakato wa kimahakama wa kuhoji ushindi wa Rais kama yanajitokeza malalamiko dhidi ya matokeo yaliyompa ushindi.
  Kama suala hili litakuwapo kwenye Katiba mpya maana yake, majaji watakuwa huru kwa mujibu wa Katiba na kama hawatakuwa huru kosa litakuwa si la mfumo wa kiutawala bali udhaifu wao binafsi na kwa ujumla, dhana ya uhuru wa Mahakama hapa haina shaka.
  Maudhui ya mapendekezo haya ni kutorejea makosa ya awali, tangu tuanze kujitawala hadi sasa. Makosa ya kuongoza nchi kwa kutegemea tu umakini wa mkuu wa nchi. Kwamba nguvu za kimaadili miongoni mwa watumishi wa umma, vita dhidi ya ufisadi, mabadiliko ya sheria mbalimbali, yote haya yafanyike au kutofanyika kwa kutegemea zaidi utashi wa mkuu wa nchi.
  Kama ambavyo watu mbalimbali wamepata kutoa maoni yao kwamba katika awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Taifa kwa ujumla wake akiwamo Mwalimu Nyerere ‘tulijisahau’ na kujenga imani kwamba tutaendelea kuwa na Rais wa aina ya Mwalimu Nyerere, mwenye mapenzi ya dhati katika misingi ya utawala bora na kimsingi, anayetenda kwa niaba ya umma wakati wote.
  Katiba mpya haipaswi tena kuachia mianya ya namna hii. Mianya ya kuongoza nchi kwa kuegemea zaidi tabia za mkuu wa nchi. Na katika suala hili na hasa kwa kuzingatia kuwa CCM ni chama tawala, napongeza dalili hizi njema kwa Katiba mpya zilizojidhihirisha katika vikao vya chama hicho Dodoma.
  Kwamba angalau zile hisia za CCM kuweza kuhujumu mchakato huu wa Katiba kwa manufaa yake zinaweza kupunguzwa makali miongoni mwa wananchi. Hata hivyo, inabidi kufuatilia kwa karibu mno kuhusu dalili hizi njema zinazozua maswali ya msingi.
  Je, CCM inajiandaa kuendesha salama siasa zake kama chama cha upinzani? Au je, CCM inazidi kudhihirisha kuwa ni chama chenye kuzingatia alama za nyakati katika masuala ya kuivusha nchi katika mawimbi ya mabadiliko na hivyo kuendelea kuaminiwa kama ilivyokuwa mwaka 1992 iliporuhusu mfumo wa vyama vingi licha ya Tume ya Jaji Francis Nyalali kueleza asilimia 80 ya Watanzania hawataki mfumo huo?
  Lakini kubwa zaidi, kwa kuzingatia mapendekezo haya ya CCM, taasisi nyingine vikiwamo vyama vya siasa nchini vinaonyeshwa mfano sasa wa kuanza kubishana kwa hoja zenye mantiki kuhusu nini kiwepo kwenye Katiba mpya kwa manufaa ya nchi na si malengo binafsi ya vyama au taasisi husika.
  Bila kuzingatia ajenda za ukaskazini, kusini au magharibi mwa nchi, tujenge Taifa moja. Tungependa kuona ushindani wa hoja za kuunganisha Watanzania wakati huu wa kuelekea Katiba mpya na si mbinu za kudhibiti hoja au kuwagawa Watanzania kwa dini zao, kanda wanazotoka au kwa wingi ama uchache wa rasilimali za maeneo yao.
  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
   
 2. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Tanzania si ya ccm ni ya Watanzania wote, kazi ya Serekali nikuwaskiliza Wananchi wa vyama vote sio halmashauri ya ccm kuwa ndio wenye mamuzi ya mwisho, Jee wajibu wa Serekali Serekali iwaskilize wajumbe wa cc or wananchi maoni yao?.


  Hapa ndipo ccm inapo zidi kujikoroga na kuwa mbali na jamii ya wananchi wa Tanzania, kuhamwa kwa ccm nikuwa mbali na vilio vya wananchi, ccm wameweka tabaka la walio nacho vigogo na wasio nacho wananchi.


  hii ni nchi ya watu wote sio ya chama, mamuzi ya Watanzania ndio ya kuheshimiwa na ndio mamuzi ya mwisho kwa Serekali ulimwenguni, halmashauri kuu ya chama cc haina mamuzi ya kuwamulia Watanzania million 45.


  Madamu washalikoroga ccm nilazima chadema wawanyeshe tu.
   
 3. MBUTAIYO

  MBUTAIYO JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  ccm wameshajitambua kwamba watakuwa chama pinzani, wakibana itakuwaje....si itakula kwao!?
   
Loading...