Hatujastaarabika vya kutosha kuitangaza Dar kimataifa. Ngoja kwanza tumalizane na kuwaondoa wamachinga na vibanda vyao kwenye maeneo yote wasiyostahili kuwepo, kufunika mitaro ya majitaka, kuondoa bodaboda wote wahuni barabarani, kujenga masoko ya kisasa ya vyakula sehemu mbalimbali, kumaliza matatizo ya kudumu ya maji na umeme na kuboresha miundombinu mingine kama barabara.
Baada ya hapo ndiyo tuzungumzie kuitangaza Dar es Salaam.
Bila hivyo tujiandae kutangaza aibu tu.