Mapendekezo kwa Serikali: Jinsi ya kuimarisha shilingi ya Tanzania

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,768
3,621
Hivi karibuni tumeshuhudia shilingi yetu ya Tanzania ikishuka thamani kwa zaidi ya asilimia 20 kiwango ambacho ni kikubwa sana na mpaka sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ili kuimarisha shilingi hiyo.

Kutokana na hali hiyo nimeona ni vyema nikaanzisha uzi huu ili tuweze kupeleka mawazo yetu kwa serikali ya Magufuli juu ya mambo ambayo yanapswa kufanywa ili shilingi yetu ya Tanzania iweze kuimarika.

Miongoni mwa sababu kubwa inayosababisha kuporomoka kwa shilingi yetu ya Tanzania ni balance of trade ambapo hapa tunaona kuwa nchi yetu inatumia bidhaa nyingi sana za nje kuliko za ndani na inauza bidhaa zake nje kwa kiasi kidogo.

Kutokana na hali hiyo ninapendekeza serikali ya Magufuli ipige marufuku uingizaji na matumizi ya bidhaa za nje ambazo sisi Watanzania tuna uwezo wa kuzizalisha na kuagiza tu zile bidhaa ambazo hatuzalishi na ambazo tuna uhitaji nazo na badala yake serikali itilie mkazo katika matumizi ya bidhaa za ndani ambazo tunazalisha sisi wenyewe.

Endapo serikali itachukua hatua hii kama hatua ya awali ya kuimarisha shilingi yetu itasaidia kwa kiwango kikubwa kuimarisha shilingi yetu ya Tanzania wakati hatua nyingine za kuongeza uwekezaji na viwanda zikifuata.

Nakaribisha mawazo yenu wadau na wazalendo wa nchi yetu juu ya namna ambavyo tunaweza kuimarisha shilingi yetu ya Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Natamani shillingi ibaki kuwa chini, imesaidia sana biashara yangu za kusafirisha mikeka na majamvi.

Hivi kwanini haswa unataka shillingi ipande? Hususan unapotaka tuuze sana nje.
 
hamna sababu ya msingi ya kulazimisha kupandisha shilingi, tukiwauzia nje kwa sasa faida ni lukuki, hiyo ni fursa!
 
Nataka shilingi ipande thamani ili mfumuko wa bei na bidhaa za hapa nchini hususani bidhaa ambazo tunaagiza nje upungue. Pia sijasema kuwa tuuze sana nje bali nimeshauri kuwa tupunguze uingizaji wa bidhaa kutoka nje hasa zile ambazo hatuna uhitaji nazo hasa bidhaa ambazo tuna uwezo wa kuzizalisha. Kwa kufanya hivyo tutapunguza matumizi ya fedha za kigeni hali ambayo itasaidia kuimarisha thamani ya shilingi yetu ya Tanzania.
 
hamna sababu ya msingi ya kulazimisha kupandisha shilingi, tukiwauzia nje kwa sasa faida ni lukuki, hiyo ni fursa!

Sababu ya kuimarisha shilingi ya Tanzania ipo tena nyingitu na sababu moja wapo ni kupunguza kama sio kuondoa kabisa mfumuko wa bei na bidhaa hapa nchini.

Pili, nadhani mkuu hujauelewa uzi wangu vizuri, mimi sijasema kuwa tusiuze bidhaa zetu nje, bali nimesema bali nimeshauri kuwa tupunguze uingizaji wa bidhaa kutoka nje hasa zile ambazo hatuna uhitaji nazo hasa bidhaa ambazo tuna uwezo wa kuzizalisha. Kwa kufanya hivyo tutapunguza matumizi ya fedha za kigeni hali ambayo itasaidia kuimarisha thamani ya shilingi yetu ya Tanzania na kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa hapa nchini.
 
Natamani shillingi ibaki kuwa chini, imesaidia sana biashara yangu za kusafirisha mikeka na majamvi.

Hivi kwanini haswa unataka shillingi ipande? Hususan unapotaka tuuze sana nje.
hamna sababu ya msingi ya kulazimisha kupandisha shilingi, tukiwauzia nje kwa sasa faida ni lukuki, hiyo ni fursa!
Wakuu,

Msiwe na hofu na hilo na naomba nitumie lugha ya kuimarika shilingi na sio kupanda. Jiulizeni swali moja la kizembe.

Pamoja na shilingi yetu kuwa inferior against foreign currencies je sisi km taifa tumeacha kuimport bidhaa? Kama jibu ni hapana basi hata shilingi ikiimarika hakutakuwa na madhara kwa kiwango hicho kwa hiyo msiogope cha msingi tuongeze thamani ya bidhaa zetu kwa kuuza finished products badala ya raw materials.

Na pia kama alivoshauri mtoa mada tupunguze kuagiza bidhaa ambazo tunaweza kutengeneza ndani ili kupunguza uhitaji wa fedha za kigeni zinazotumika wakati wa kuagiza kitu kitachopunguza demand ya dollar kwetu na hiyo itafanya thamani ya TSHS kuimarika, kama unauza bidhaa nje kama @FaizaFoxy, zingatia tu ubora wa bidhaa zako na utauza bila shida na kupata faida kubwa zaidi kuliko awali.
 
Shiling itapanda tu endapo exportation itakuwa zaid ya importation otherwise tusahau kuhusu shiling yetu kupanda
 
Sababu ya kuimarisha shilingi ya Tanzania ipo tena nyingitu na sababu moja wapo ni kupunguza kama sio kuondoa kabisa mfumuko wa bei na bidhaa hapa nchini.

Pili, nadhani mkuu hujauelewa uzi wangu vizuri, mimi sijasema kuwa tusiuze bidhaa zetu nje, bali nimesema bali nimeshauri kuwa tupunguze uingizaji wa bidhaa kutoka nje hasa zile ambazo hatuna uhitaji nazo hasa bidhaa ambazo tuna uwezo wa kuzizalisha. Kwa kufanya hivyo tutapunguza matumizi ya fedha za kigeni hali ambayo itasaidia kuimarisha thamani ya shilingi yetu ya Tanzania na kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa hapa nchini.
kama bidhaa ipi isiyohitajika au inayozalishwa kwa tija TZ?
 
Serikali ipige marufuku matumizi ya US dollar na foreign currencies zote zisitumike ktk mihamara (transactions ) yoyote hapa nchini.
 
Mbona zipo nyingi tu mkuu! Mfano: Tanzania tuna viwanda vingi sana vya kuzalisha vinywaji vya soda, juisi na vileo (pombe) lakini cha ajabu watu tunaingiza bidhaa za aina hizo ambazo sisi tuna uwezo wa kuzizaisha hapa Tanzania tena kwa wingi tu. Watu tunaingiza mpaka soda na juisi kutoka nje wakati nchi yetu ina viwanda vingi tu vya kutengeneza juisi na soda tena zenye ubora wa hali ya juu. Watu tunaingiza hadi toothpick kutoka nje, hivi kuna haja kweli ya kuingiza toothpick kutoka nje?

Bidhaa ambazo ambazo zinaingizwa hapa nchini ambazo ambazo tunazizalisha na ambazo hatuna uhitaji nazo ni nyingi sana ambazo siwezi kuziandika zote hapa.
 
Nashukuru kwa pendekezo/ushauri wako. Lakini je, hatua hii itasaidia vipi katika kuimarisha shilingi ya Tanzania? Naomba ufafanuzi wako mkuu.
 
Biashara ya kununua na kuuza foreign currency ni kama ilivyo biashara nyengine inakuwa gorverned na demand and supply policy. Inapokuwa unalazimika kulipia baadhi ya bidhaa ama huduma kwa US$ inakulazimu ukainunuwe, wakati kungekuwa hakuna ulazima huo kama ingekuwa unalipia kwa local currency.

Mwenye kuuza foreign currency anaweka faida (Ths 5-20) kwa kila US$, kwa mfano. Inapokuwa wateja wa kununuwa wamezidi yeye hupandisha bei ya kununulia na matokeo yake bei ya kuuzia inazidi. Inapokuwa wateja wa kununuwa kidogo na hela za kigeni anazo nyingi, anaogopa US$ kumlalia na bei kuporomoka akala hasara. Na matokeo yake bei ya kununulia inaanguka kwa vile hana uhakika siku chache zijazo rate itaanguka au kupanda kiasi gani. As simple as that
 
Nashukuru kwa ufafanuzi wako mkuu. Nimekuelewa vyema. Bila shaka wazo lako hili kama litatekelezwa na serikali litasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha thamani ya shilingi yetu ya Tanzania.
 
Mbona zipo nyingi tu mkuu! Mfano: Tanzania tuna viwanda vingi sana vya kuzalisha vinywaji vya soda, juisi na vileo (pombe) lakini cha ajabu watu tunaingiza bidhaa za aina hizo ambazo sisi tuna uwezo wa kuzizaisha hapa Tanzania tena kwa wingi tu. Watu tunaingiza mpaka soda na juisi kutoka nje wakati nchi yetu ina viwanda vingi tu vya kutengeneza juisi na soda tena zenye ubora wa hali ya juu. Watu tunaingiza hadi toothpick kutoka nje, hivi kuna haja kweli ya kuingiza toothpick kutoka nje?

Bidhaa ambazo ambazo zinaingizwa hapa nchini ambazo ambazo tunazizalisha na ambazo hatuna uhitaji nazo ni nyingi sana ambazo siwezi kuziandika zote hapa.

Serikali ipige complete ban ya kuingiza baadhi ya bidhaa ambazo zinazalishwa hapa nchini na kutosheleza. Kama ulivyosema, vinywaji baridi na most of vinywwaji moto, fruits na vegetable za makopo, mchele, sukari, unga wa ngano ( ngano nzima ni ruhusa), long life milk, frozen red and white meats, mafuta ya kula, chumvi na vyengine vinavyozalishwa nchini. Can you imagine Tanzania tunaagiza tomato na mahindi ya kopo au tomato puree? Kwa nini Serikali isiwashawishi hao wenye kiwanda cha kusindika nyanya wakafanya hivyo hapa nchini, nyanya zimejaa.

Nimezungumzia vyakula ni kwa sababu hivi ndio vinatumika kwa wingi kila siku. Lakini vyakula hivi hivi pia vinazalishwa na kupatikana nchini. Ukiamua kukaa mwaka mzima bila ya kula chakula kilichotoka nje ya nchi basi inawezekana kirahisi tu. Kuanzia asubuhi mpaka usiku.

Uzuiwaji huu unaweza kusababisha bei za vyakula kupanda kidogo kwa 10-20% kwa muda, lakini kwa upande mwengine utaipa nguvu sarafu yetu kwa 10 - 15% minimum, na matokeo yake ni bidhaa za nje kushuka bei. Na vile vile kwa kupanda bei za vyakula kwa muda itawapa nguvu wakulima kuzidisha bidii katika kilimo na matajiri wakizalendo ku invest kwenye kilimo kwa vile wataona kina tija. Matokeo yake ni kuwa uzalishaji utakuwa mkubwa san, bei itashuka na kwa vile wafanya biashara wakubwa na wao watakuwa kati ya wakulima wataanza ku export badala ya ku import tulipokuwa tunafanya mwanzo. Bila ya kufanya hivyo, dhana ya kujitegemea kwa kilimo, itakuwa haifanyi kazi. Tunahitaji wafanya biashara wakubwa wavutike ili wa invest kwenye kilimo cha kisasa na nchi ifaidike
 
Last edited:

Mawazo yako ni mazuri sana mkuu na ninaunga mkono hoja.
 
Hivi karibuni tumeshuhudia shilingi yetu ya Tanzania ikishuka thamani kwa zaidi ya asilimia 20 kiwango ambacho ni kikubwa sana na mpaka sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ili kuimarisha shilingi hiyo.

Kutokana na hali hiyo nimeona ni vyema nikaanzisha uzi huu ili tuweze kupeleka mawazo yetu kwa serikali ya Magufuli juu ya mambo ambayo yanapswa kufanywa ili shilingi yetu ya Tanzania iweze kuimarika.

Miongoni mwa sababu kubwa inayosababisha kuporomoka kwa shilingi yetu ya Tanzania ni balance of trade ambapo hapa tunaona kuwa nchi yetu inatumia bidhaa nyingi sana za nje kuliko za ndani na inauza bidhaa zake nje kwa kiasi kidogo. Kutokana na hali hiyo ninapendekeza serikali ya Magufuli ipige marufuku uingizaji na matumizi ya bidhaa za nje ambazo sisi Watanzania tuna uwezo wa kuzizalisha na kuagiza tu zile bidhaa ambazo hatuzalishi na ambazo tuna uhitaji nazo na badala yake serikali itilie mkazo katika matumizi ya bidhaa za ndani ambazo tunazalisha sisi wenyewe.

Endapo serikali itachukua hatua hii kama hatua ya awali ya kuimarisha shilingi yetu itasaidia kwa kiwango kikubwa kuimarisha shilingi yetu ya Tanzania wakati hatua nyingine za kuongeza uwekezaji na viwanda zikifuata.

Nakaribisha mawazo yenu wadau na wazalendo wa nchi yetu juu ya namna ambavyo tunaweza kuimarisha shilingi yetu ya Tanzania.

Cha msingi turekebishe sheria zetu zinazoruhusu matumizi ya dollar nchini. Sheria hizi ni za madini na utalii. Mahoteli na madini zote zitatoza shilingi hivyo kuwa highly demanded na dollar kuwa supplied. The higher the demand the higher the price na kinyume chake. Wote watakao toza dollar watashughurikiwa na kuifanya shilingi kuwa ya thamani kubwa.

Kumbuka dollar ni sarafu kubwa kuichanganya na shillingi kwenye uchumi mmoja lazima sarafu dhaifu shilingi itayumba. Mengine ya balance of trade yatakuja baadaye lakini lazima nyumba yetu iwe in order. Matumizi ya shilingi maeneo yote iwe wimbo wetu.
 
Kwa hiyo unamaanisha kuwa biashara na maduka yote ya kubadilisha fedha yafungwe? Kama ndivyo je, watu wanaokuja Tanzania kutoka nje hasa Watalii ambao watahitaji kubadili fedha zao za kigeni kuwa shilingi ili waweze kupata huduma, unashauri fedha hizo ziwe zinabadilishiwa wapi? Ama iundwe taasisi maalum ya serikali ambayo itashughulikia swala la kubadili fedha za kigeni?
 
Hapana maduka yawepo tu lakini hakuna manunuzi ya aina yeyote yatakayo fanyika kwa kutumia dollar. Si nyumba za kupanga, hoteli, huduna za kitaalamu nk. Ukija na dollat ili uishi badilisha kwanza ziwe shilingi. Hapo ndipo shilingi itasakwa kama lulu!!
 
Back
Top Bottom