Mapato ya Viongozi wetu na Mali zao... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapato ya Viongozi wetu na Mali zao...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, May 9, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kama kuna kitu ambacho Serikali ya Tanzania inasifika kwa usiri, ni kuficha kwa kipato cha viongozi na usiri wa mali zao.

  Tumeonelea kwa muda mrefu ni jinsi gani kila kitu kinafanyika kwa siri na kila mtu akidai kuwa keshawasilisha taarifa zake kwa tume ya maadili.

  Lakini tume hii ya maadili, si inafanya kazi kwa ridhaa wa Serikali na si Wananchi, na hivyo kuficha ukweli kuhusu mapato ya watumishi wa Serikali walioko katika nafasi za uongozi kama vile Rais, baraza la mawaziri, Wabunge na mpaka wakuu wa wilaya?

  Iweje kila kitu ni siri na kitafahamika kwa Umma pindi Raisi atakapoamua na isiwe ni jambo la kawaida?

  Wenzetu Wamarekani, kila mwezi wa nne wa mwaka mpya, kila raia na mkazi anayefanya kazi Marekani , huwasilisha ripoti za mapato yao ya mwaka wa fedha uliopita kwa Mamlaka ya kodi ili kupimwa kama wamelipa kodi ilivyotakikana au la.

  Hata Rais wa Marekani, hutoa ripoti kamili inayoonyesha mapato yake na mali zake iwe ni mshahara, rasilimali za soko la mitaji (hisa), mauzo ya mali kama vitabu na mali zingine anazomiliki kama nyumba, mashamba na hata magari na boti.

  Sasa nashangaa kwa nini Tanzania mambo haya ni siri na huku tunajitapa kuwa tunataka tuwe wazi na tuna demokrasia.

  Wakati wa Ujamaa, ilieleweka kwa nini Viongozi walikuwa wakificha ukweli kuhusu mali walizonazo, kwa kuwa miiko ya uongozi ilikataza kwa wao viongozi kuhodhi na kumiliki mali zaidi ya kipato chao cha mshahara.

  Hivi sasa, kila mwanasiasa aliyeko Bungeni au ngazi yeyote ya uongozi na uwakilishi, hudai kuwa ameshafanya wajibu wake kutaja mali zake kwa Mwenyekiti wa tume ya Maadili na hivyo tusimsumbue kujua ana mali kiasi gani.

  Sasa kama sisi tungekuwa kama Marekani;
  • Ingekuwa rahisi sana kujua mali za Chenge na hata kumtia mashakani kwa uharaka tuliposikia kuwa ana akaunti ya fedha za kigeni kule Cayman Island.
  • Tungeshituka mapema na kumhoji Mkapa alipopata uwezo wa kununua Kiwira na hata kupata mkopo ule wa Dola Laki 5.
  • Tusingepagawa kusikia kwamba Mwakyembe ana hisa za thamani kubwa kwa kampuni ya kufua Umeme.
  • Karamagi asingeangaliwa kwa mashaka na kampuni yake ya Makontena.
  • Alipoibiwa Kapuya mitambo ya kuchimba madini tusingejiuliza katoa wapi pesa.
  • Tungejua mapato halisi ya Rostam na mahusiano yake na Kagoda na Dowans.
  Lakini kwa kuwa kila kitu ni siri ya viongozi, basi ndivyo ilivyokuwa rahisi kwa sisi kama Taifa kuhujumiwa mchana mweupe na viongozi wetu kuingiwa tamaa na kushindania kuhujumu na kumiliki mali kuzidi uwezo wao wa kipato.

  Leo hii hakuna aliyediriki kuuliza swali alilouliza mwalimu Nyerere kwa Lowassa kuwa alipata wapi fedha za kujenga jumba kubwa la kuikodishia Ubalozi wa Afrika Kusini!

  Hivyo basi, safari yetu ya kupigana na ufisadi, haianzi na Manji, Lukaza au Mengi pekee, inaanza na Kikwete, Shein, Pinda, Sitta, Karume, Mwamnyange, Manumba, Jaji Ramadhani. Othman, Lowassa, Nahodha, Zitto, Slaa, Kimbisa na wengine wengi ambao ni viongozi.

  Tunataka tujue mapato yenu ya mshahara kwa mwaka, mapato mengine ambayo si mshahara na thamani na orodha za mali zenu! Haya ya siri na kutuficha yana lea ufisadi na ukosefu wa uadilifu na nidhamu kati yenu.

  Aidha kila pato (mshahara, masurufu, bakshishi, bonasi) ni lazima likatwe kodi! Hii mambo ya kujilipa masurufu na kutafuta safari kila kutwa kuchwa ni wizi wa mchana!

  Naambatanisha habari ya mapato ya Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama kama kithibitisho cha nchio iliyojijenga Kidemokrasia na uwazi kutoka kwa viongozi wake. Sitakubali kisingizi kuwa sisi ni bado nchi changa kufikia hatua kama Marekani kuwa wazi katika kujua mapato ya Viongozi wetu!

  [​IMG]
   
 2. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hii ni taarifa rasmi kutoka Ikulu ya Marekani kuhusu mapato ya Rais na Makamu wake kwa mwaka 2008.

  The White House - Press Office - President and First Lady Release 2008 Income Tax Returns

  The White House - Press Office - The Vice President and Dr. Jill Biden Release 2008 Income Tax Returns
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Huu utamaduni mzuri ndugu yangu: Pia upo nchi zingine pia zilizoendelea! Jk wanaogopa madudu, na wanataka siri, na hakuna mtu wa kuwauliza!

  Hivi kazi ya Tume ya Maadili ya Umma Tz ni nini? Kwa nini isifutwe?
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  sasa ungependa ibadilishwaje? Kupitia serikali, bunge au mahakama?
  Kitu kimoja ukumbuke, zipo sheria zinazowalinda hawa viongozi, kwa mfano defamation. Wewe ukienda kulalamika fulani ana pesa nyingi kuliko mshahara wake, ujue ni kumchafulia jina na unaweza kudaiwa fidia kubwa sana.

  Lakini, kwa upande wangu na ninavyoelewa sheria ya 'defamation', vyombo vya habari vina uwezo mkubwa sana katika kutoa habari hata kama zitaonekana kuwa zinachafua jina la mtu. Kama habari hiyo, sio ya kutunga na inakuwa ya 'national interest', basi hata kama inamchafua mtu jina, habari hiyo haiwezi kuwa chini ya defamation. Watu wengine walio na uwezo wa kusema bila kuvunja sheria ya 'defamation' ni wabunge, KAMA akitoa habari hiyo ndani ya bunge (parliamentary privileges).

  Sheria hii ni kwa nchi za Uingereza na some Commonwealth. Kwa Tz sijui maana sijasoma sheria huko! Kuna wanasheria wengi sana bongo, sema ndo ivyo, kila mtu anatafuta maslahi yake, sio kujenga nchi.
   
 5. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Duh! but that is good. May be Tanzania will adopt it in near future
   
 6. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Rev acha wivu kwa viongozi wetu.......
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  day 900000000000000000000000000000000000000000000000

  ikulu haina website
   
 9. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hakuna haja ya kluleta rabsha, tuchore mstari mmoja tuseme tutajie mapato yako na mali zako. Wakishataja, mwaka unaofuata tutawauliza swali hilo hilo, tukiona yasiyoeleweka, ndipo tuanze kuhoji hizo tofauti.
   
 10. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Typical kula kulala. Ngoja uanze kufanya kazi/biashara halali na kulipa kodi serikalini.
   
 11. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani kwa kila mwaka wa fedha, itolewe na kuchapishwa kwenye magazeti orodha ya mishahara na marupurupu ya positions zote serikalini kuanzia Rais mpaka watendaji wa serikali za mtaa.
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Viongozi wetu tunajua background zao huko vijijijni wanakotoka; sasa wanapopata vyeo hiyo inakuwa passport ya kujilimbikizia mali na ndio maana wanafanya siri hizo form zao kwani hawaandiki ukweli wanaongopa!! Angalia Andrew Chenge kwenye declaration yake hakuorodhesha vijisenti vile alivyoficha ulaya!!
   
 13. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  There is a wealth/assets disclosure policy in our parliament, which requires all MP's to fill a form and attach all documents of the claimed ownership or wealth. MP's fill those forms, i am not sure if president fills it. However, in Mkapa's inaugural speech to parliament in 1995 he declared his assets - houses, 10 acres of land, cars and number of plots. I can't remember what he said exactly. That was a good start which could be followed with his successor and other leaders!

  Despite the fact that Mkapa declared his properties in 1995, there was no commission in place to follow up and monitor his assets to measure if he used his leadership position to benefit himself when he finished his two terms in the office. It would have been interesting when he finished his presidency to declare what he owned then!

  The same story goes to MPs, once they fill the forms their declaration is protected by law, a top secrete document - why? Second, even though MP's fills the forms, there is no procedure in place which continue to monitor or put an eyes on them to prevent the misuse of their position for personal gain.
   
 14. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  Tanzania ina sheria kali za maadili ya kutangaza mali kuliko U.S.A. Tatizo hakuna mwenye mwamko kudai rekodi.

  Barack Obama alipotangaza mapato yake alisema ``As another demonstration of the President’s commitment to openness and transparency, today the White House ... is making the President’s tax returns public.``

  Hakutakiwa kisheria kutangaza tax returns zake. Kama raia yeyote yule, ingeweza kuwa siri yake na IRS. Kwa Tanzania, Kikwete ni lazima, hana chaguzi, ni lazima atangaze mali zake Tume ya Maadili.

  Na cha muhimu, sheria ya Maadili inasema, ibara ya 21(2), mwananchi yeyote anaweza kuomba kuchunguza daftari la mali na maslahi ya kiongozi. Ni juu yetu wananchi kudai hizo nyaraka tuzione. Tusisubiri Kikwete atufanyie hisani ya kutangaza mali zake kama Obama, tutumie sheria zetu ambazo ni kali kushinda za kina Obama.

  Au tusubiri siku Mtikila akinyimwa mikopo na matajiri akasirike aende kusaidia kutuombea hilo daftari mahakamani.
   
 15. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mchungaji,
  Wiki chache zilizopita Wabunge wetu walimzomea Dr. Silaa kwa kutaja mapato ya Ubunge. Hao ndio wanaopaswa kuwa wasimamizi wa mapato na matumizi ya Serikali yetu. Hivi kweli wataweza kushinikiza sheria ya viongozi kutaja mapato yao izingatiwe ipasavyo? Tunahitaji uwepo uzalendo ndani ya nyoyo za Watanzania wote hususan viongozi wetu ili zoezi kama hilo liweze kufanikiwa.
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Rev,

  - Siku hizi viongozi wetu wamegundua EPA mpya, nayo ni kusafiri tu! Yaaani maofisa wa serikali na viongozi wanasafiri nje kama wendawazimu, yaani nasikia sasa imefikia mahali hata ukiwakamata na mali nyingi wana sababu kubwa sana ya kusafiri,

  - Siku hizi sio ajabu Waziri kusafiri akiwa amechukua padei ya shillingi millioni 50 kwa safari moja, ambayo wanahakikisha kwamba inapitia nchi nyingi sana kabla ya kwenda anakotakiwa, ikiwa ni safari moja tu yaani kwenda nchi moja na kurudi hawatakai wanawapa maofisa wa chini yao!

  - Hili nimelipata majuzi kutoka kwa ofisa mmoja wa bongo, aliyekua safarini badala ya kwenda kwenye mkutano alikua ana-shop tu, sasa nasikia mkuu wakaya anaposafiri ndio utalia machozi na hela zinazochotwa! na hajawahi kusafiri na chini ya watu 40!

  Mungu Aibariki Tanzania.

  FMEs!
   
 17. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Suala hili si kwa viongozi tu bali lilitakiwa liwe kwa watanzania. Taarifa zao zingeingizwa kwenye database na kupewa namber maalum. Hiyo ndio ingetumika hata kutathmini kodi mtu anayopaswa kulipia. kila mwaka, kila mtu alitakiwa ajaze form ya mapato yake yote na kuwasilisha sehemu husika. Kama atandanganya basi anapigwa fani kubwa ili liwe fundisho kwa wengine. Hili linawezekana pale tu takapokuwa na rais ambaye hana ubia na mafisadi.
   
 18. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Nothing to say
   
Loading...