Mapato ya utalii nchini yashamiri

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
SERIKALI imesema mapato yatokanayo na sekta ya utalii nchini yameongezeka kwa asilimia 8.2 hadi kufikia Dola za Marekani milioni 2,006.3 (Sh bilioni 4.2) mwaka 2014 kutoka Dola za Marekani milioni 1,853.3 (Sh bilioni 3.9) mwaka 2013.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi alipokuwa anazungumzia ripoti ya utafiti wa watalii walioingia nchini mwaka 2014.

Alisema utafiti huo ulifanywa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Uhamiaji na Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT).

Alisema Zanzibar ilipata Dola za Marekani milioni 269.3 mwaka 2014 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 210.5 mwaka 2013.Dola moja ni sawa na Sh 2,100 kwa sasa.

Aidha, alisema wastani wa matumizi yote kwa mtalii kwa siku ilikuwa Dola za Marekani 221 chini kidogo ya Dola za Marekani 284 zilizoripotiwa mwaka 2013.

Pia alisema masoko makuu 15 ya utalii yanachangia asilimia 82 ya watalii wote wa kimataifa Zimbabwe, Uholanzi na China ni masoko mapya katika masoko makuu 15 kwa mwaka 2014 ambayo yamechukua nafasi ya Sweden, Uswisi na India katika masoko makuu 15 yaliyopatikana mwaka 2013.

Aidha, alisema utalii wa wanyamapori Tanzania Bara ulichangia asilimia 43.5 na wageni wengi waliokuja kwa ajili ya wanyampori walitokea Uingereza, Ufaransa na Italia.

Pia alisema ripoti hiyo inaonesha watalii wengi walionekana kutofurahishwa na kutokuwa na huduma ya malipo ya fedha kwa kutumia kadi katika maeneo yanayotoa huduma za kitalii na asilimia 87 ya watalii walilipia huduma mbalimbali za kitalii kwa kutumia fedha taslimu.
 
Correct your figures!!!!!
 
Figure haziko sahihi kwenye Tz shilling. Inatakiwa iwe Trillion shillings instead of Billion shilling!
 
Back
Top Bottom