Mapanga yamezidi yombo vituka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapanga yamezidi yombo vituka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shedafa, Oct 21, 2008.

 1. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2008
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwa wiki ya pili sasa eneo la Yombo Vituka limekuwa katika hali ngumu ya usalama, ni eneo kuanzia Buza hadi kufika Vituka Sigara. Kuna kikundi cha vijana ambacho kimeamua kupiga watu mapanga hovyo nyakati za jioni, cha kushangaza wakati mwingine hawachukui chochote. Inaonekana nia yao ni kuua tu kwani hadi kufikia leo asubuhi wamekwisha piga mapanga watu 18, na inasemekana kati ya hawa kuna waliopoteza maisha. Sina uhakika nalo kwa kuwa majeruhi wamekuwa wakichukuliwa na polisi kupelekwa hospitali, baada ya hapo tumekosa taarifa ya maendeleo yao. Tunajaribu kuweka sungu sungu maeneo yote haya lakini hatujafanikiwa kulizima hili wimbi ingawa mara 2 moja ya vikundi vya sungu sungu wamefanikiwa kupambana na hili kundi na kuwaua 3 wao, hali bado ni ngumu. Jana tu kijana mmoja jirani katokea tundu la sindano baada ya kufanikiwa kuwazidi mbio na hii ilikuwa majira ya saa 1 tu usiku.
   
 2. PgSoft2008

  PgSoft2008 JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2008
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  can not believe if this is Tanzania Nchi ya Amani
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Doh, Poleni sana!
  .
   
 4. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2008
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Asante kwa pole mkuu!
  Hata sielewi hii roho ya kinyama hawa jamaa wameipata wapi, kwa sababu binafsi nimepata bahati ya kuwaona wanne kati ya hawa waliopigwa mapanga. Watatu waliopigwa siku ya kwanza na mmoja kati ya waliopigwa siku ya pili. Huwezi kuamini kama kati yetu watanzania kuna wenye roho ya kinyama kiasi hiki. Huyu wa kwanza alikuwa amepanda baiskeli akitokea kipunguni kuelekea maeneo ya vituka sigara kupitia katika pori la jeshi, basi wakamdaka hapo katikati. Walimshambulia kiasi mkono wake wa kushoto waliumaliza kabisa kama mbavu za mbuzi tayari kwa kuchomwa, alijitahidi kujikokota hadi kwenye nyumba za karibu ili kupata msaada. Polisi walikuja baadaye na kumpeleka hospitali na kuna tetesi kuwa alifariki. kwani kuna waliomfahamu kuwa ni mwalimu wa shule ya msingi. Polisi walipokwenda eneo la tukio wakaikuta baiskeli yake, lakini wakati huo wengine watatu walikuwa tayari wamekuja huku wakiwa wanalia na majeraha. Kesho yake wakamshambulia mzee wa watu akiwa amebeba mtoto katika baiskeli, wakamshambulia huku mtoto wake akiona huku akipiga kelele za kuomba msaada, walipomuacha naye akajikokota jirani kuomba msaada. Majuzi wameshambulia kwenye msiba, wamesubiri wanaume wameenda kuzika wakawavamia wakina mama wakawajeruhi 7. Ukweli hali ni ngumu, polisi wanakuja kupiga doria lakini hawajafanikiwa kuwanasa. Nasi tunaweka sungu sungu lakini bado hatujafanikiwa kulizima hili kundi.
   
 5. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Inasikitisha,
  Kuna dalili kwamba hao watu wana wivu. Maeneo ya jirani kuna watu wenye maisha duni kupindukia?

  Nimewahi kusikia hadithi inayofanana na yako miezi kadhaa nyuma. Sikumbuki ni wapi, ila kama sio kwenye wilaya za Dar, basi ni kilometa chache nje ya Dar es Salaam.
  .
   
 6. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2008
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wivu!, sina hakina kama inaweza kuwa ndio sababu. Kama ingekuwa ndio sababu wangekuwa wanachagua wa kupiga, ila hawa hawachagui na sehemu kubwa ya wahanga ni watu wa kawaida tu. Ila inaweza kuwa wanalipiza kisasi, inawezekana kuna kitu wamefanyiwa mahali ndio wameamua yeyote watakayemuona kwao sawa tu.
   
Loading...