Mapambano dhidi ya madawa ya kulevya

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,822
59,433
drug-addiction-abuse.jpg
images
drug-addiction-abuse.jpg


Inaonekana mwezi huu umekuwa mzuri kwa wale wanaopambana na uuzaji pia matumizi ya madawa ya kulevya baada ya watu kadhaa kukamatwa akiwemo msanii Chid Benz. Kwangu mimi hilo ni jema,tena sana, ila kusema ukweli nachoshwa sana kusikia watu wanavyosema ''hawa wanatuharibia watoto, hawa wanatuharibia ndugu zetu, wauzaji ni mashetani, ni wauji n.k'' pale wanapowaongelea wasambazaji.

Hivyo ndivyo dunia ilivyo, na ndivyo binadamu tulivyo. Binadamu ni wabinafsi na muda mwingi watu hufanya vitu kwa faida binafsi na sio kwa faida ya wengine.Ndio maana sumu ipo na inauzwa, bunduki na mabomu nayo vile vile, pombe na aina nyingine za vilevi navyo ni kwa madhumuni hayo hayo, ya kumteka mtu mwingine kifikra/ki-utu na kumtajirisha mwenyewe. Kukubali kushawishika na kujiingiza kwenye kitu ambacho kina madhara kwa mtu ni kosa kwa mtu mwenyewe kwanza kabla ya mwingine yeyote Yule.

Nashangaa kwamba lawama zote wanatupiwa hao wauzaji na hamna mtu anaejikosoa yeye mwenyewe kama mzazi ama ndugu wa muathirika wa madawa ya kulevya kwa kushindwa kwa namna moja ama nyingine kumuweka mtu wake wa karibu kwenye mstari ili asiingie kwenye janga hilo la madawa ya kulevya on the first place.

Jiulize ulikuwa wapi usiweze kumsaidia mtu wako kabla hajaanza kutumia? Ulitumia nafasi yako vizuri kumuelimisha na kumsaidia kama alikuwa na matatizo binafsi ili yasimsukume kwenye ulimwengu huo wa madawa ya kulevya? Ulim-support alipokuhitaji?Ulimuelimisha kama ni kijana mdogo aliyehitaji muongozo wako? Na kama ni kijana aliyejifunza kutumia madawa ya kulevya kwa kufuata mkumbo na ushawishi wa marafiki tu.

je umewahi kukaa nae chini ukamfundisha umuhimu wa kuwa na maamuzi binafsi bila kukubali kusombwa na makundi hata kama ataonekana sio mjanja? Fikiria, kama mtu alishawishiwa tu (that means anashawishika) kwanini wewe kama ndugu/jamaa/rafiki usimshawishi kutokujiingiza kwenye mambo kama hayo??

Nnachomaanisha ni kwamba, hao wote wanaolalamikiwa wameharibiwa na hao jamaa wa Magomeni, Ilala na kwingineko walilazimishwa kutumia madawa ama walijiingiza kwa hiari na matakwa yao binafsi?? Chukulia mfano wa msanii Ray C aliyekuwa anamlaumu mpenzi wake wa zamani Lord Eyez kwa kumshawishi atumie madawa ya kulevya (bangi iliyochanganywa na madawa mengine bila yeye kujua kama anavyodai mwenyewe).

Mwisho wa siku aliyefanya maamuzi ya kutumia alikuwa ni yeye au ni mpenzi wake? Watu wengi wanashawishiwa kufanya vitu wasivyovifanya ila mwisho wa siku maamuzi ni ya Yule anayeshawishiwa na sio mshawishi. Ndio maana mpaka leo kuna watu wasiokunywa pombe japo wamezungukwa na watumiaji kila upande kwa miaka nenda rudi, bila kusahau ushawishi wa kutosha kutoka kwa wale wanaowazunguka.

Kwahiyo tuache kumlaumu anayetengeneza sumu, kisha anaeuza sumu na kuangalia je aliyekunywa sumu alisukumwa na nini??Na sisi kama ndugu/jamaa na marafiki tulichangia kwa kiasi gani kumuacha/kumsukuma (kwa kushindwa kuwa nae pale alipotuhitaji) ndugu/jamaa ama rafiki yetu anywe sumu? Ukweli ni kwamba mwisho wa siku hao drug dealers ni wafanyabiashara. Wanachojali wao ni kuuza mzigo wao tu, hawachagui wa kumuuzia ili mradi apate hela. Wanaotakiwa kuleta mabadiliko ni sisi na sio wao kwasababu ushawishi wao ni mahsusi kuongeza victims ili biashara ikue na sio kupunguza.

Wewe kama mwana jamii, mwana familia, rafiki do your part. Muepushe rafiki, jirani,ndugu na jamaa yako na madawa ya kulevya. Usikae kutegemea ''drug dealer'' mwenye uchu wa pesa atakusaidia kwa hilo, kamwe haitotokea.

Mabadiliko yanaanza na wewe!
 
mleta mada umekuja vizuri na mada yako..kikubwa watu wafahamu haya madude yalikuwepo na yataendelea kuwepo kikubwa ni kutojingiza huko ktk utumiaji
huyo chidy benz naye kukamatwa kwake yeye ni mtumiaji na mgonjwa najua kwa kete hizo alizoshikwa nazo atapewa dhamana tu
 
Mada nzuri sana:ila kuna watumiaji walijikuta wako hivyo si kwa hiari yao.Nakumbuka wakati niko form 2,uvutaji bangi ulikuwa ni kuongeza uwezo wa "kupiga msuli".yawezekana kuwa na maisha mazuri basi ni kutumia hizo dawa.
 
Mada nzuri sana:ila kuna watumiaji walijikuta wako hivyo si kwa hiari yao.Nakumbuka wakati niko form 2,uvutaji bangi ulikuwa ni kuongeza uwezo wa "kupiga msuli".yawezekana kuwa na maisha mazuri basi ni kutumia hizo dawa.
KIKOSIKAZI ndio maana ni muhimu wazazi na walezi wakatumia juhudi kuwaelimisha vijana wao kuhusu madawa ya kulevya na madhara yake in the long run. Maana kama unavyosema wengine wanavuta bila kujua long time effect, wanadhani ule mzuka wanaoupata wakati wanavuta ndo kitu pekee watakachopata kwenye utumiaji.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom