nusuhela
JF-Expert Member
- Jan 26, 2014
- 5,736
- 6,972
Nikiwa nimekaa kwenye daladala huku nawaza kuhusu hatma ya taifa letu kutokana na janga la corona, nikajikuta nafikiria kuhusu usalama wa wasafiri kwa kutumia usafiri huo wa uma.
Watu bado wanashika vyuma kule juu, watu bado wanashika viti, watu bado wanashika madirisha.
Najiuliza, kwa siku huwa ni watu wangapi hushika sehemu hizo.
Mbali na kushika vyuma, viti na vioo vya daladala, watu wanatumia simu wawapo ndani ya daladala na wawapo nje ya daladala.
Issue yangu ipo kwenye matumizi ya simu. Baada ya kushika chuma, viti na vioo tunashika simu zetu. Ikumbukwe, kinachonawa ni mikono peke yake huku tukiacha virus kwenye simu zetu ambazo baada ya kunawa tunazitumia.
Je, tutaweza kushinda hii vita maana naona matumizi ya simu ni moja kati ya vinavyoweza kuwa sababu kubwa ya kusambaa kwa virus hawa?
Sent using Jamii Forums mobile app