Mapafu Kujaa maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapafu Kujaa maji

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 10, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Ni pale ambapo kunakuwa na mkusanyiko wa maji kati ya kuta mbili zinazozunguka mapafu. Kujaa huku kwa maji husababisha mgonjwa kupata shida ya kupumua vizuri.
  [​IMG]

  Je mapafu kujaa maji husababishwa na nini?


  Sababu za Mapafu kujaa maji zinaweza kuelezewa kutokana na aina ya maji yaliyojaa:

  • Transudate – hapa maji huliki kutoka kwenye mishipa ya damu na kuingia kwenye mapafu mfano kwenye magonjwa yafuatayo:
  • Moyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi (congestive cardiac failure)
  • Ini kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi (liver failure)
  • Figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi (renal failure)
  • Exudate – hapa maji hujaa kutokana na kuta zinazonguka mapafu kitaalamu pleura zinapovimba au kutokana na magonjwa ya mapafu mfano:
  • Kansa ya pafu au ya titi
  • Lymphoma
  • Kifua kikuu
  • Vichomi
  • SLE
  • Figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi
  • Asbestosis
  • Majipu ndani tumbo
  Dalili:

  • Kusindwa kuhema vizuri
  • Maumivu ya kifua
  • Kifua kikuu- Jasho jingi kutoka kipindi cha usiku, kukohoa damu, kupungua uzito
  • Vichomi- homa , kukohoa, makohozi yenye rangi
  Vipimo:

  • Picha ya kifua kikuu (x-ray)
  • Ultrasound ya kifua
  • CT-scan
  • Thoracentesis
  • Vipimo vya damu

  Matibabu:
  Kwasababu ya kusababisha matatizo ya kupumua inabidi kuanza na ABC za kuokoa maisha, angalia mfumo wa hewa na kadhalika . tibu magonjwa yanayosababisha kupunguza maji kwenye mapafu kunaweza kutumika kwa ajili ya kipimo au matibabu ya kumpa nafuu mgonjwa. Mapafu Kujaa maji
   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,216
  Likes Received: 10,579
  Trophy Points: 280
  Shukrani sana.
   
 3. tembekezad

  tembekezad Member

  #3
  Sep 12, 2016
  Joined: Jul 23, 2016
  Messages: 15
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  vipimo hivyo hospitali ya mkoa vinapatikana?
   
Loading...