Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Ndugu zangu,
Nikiwa kama mwanachama mwaminifu na mtiifu wa CHADEMA, najitokeza tena kwa mara nyingine kuelezea maskitiko yangu juu ya minyukano hii inayoendelea ndani ya CHADEMA.
Niweke wazi kwamba ninasikitishwa sana na mwenendo wa kisiasa uliopo ndani ya CHADEMA hivi sasa, na ukimya wa viongozi wa juu wa chama katika kuyashughulikia haya. Kama ningekuwa na sababu ya kumlaumu yeyote iwapo chama changu CHADEMA kitakufa, hivi leo, basi nitawalaumu Mbowe na Slaa. Kusema ukweli sijui ni nini kinaendelea kwa hawa wakubwa. Zinapojitokeza tofauti kubwa za kichama kama hizi ni kwanini visiitishwe vikao vya dharura ili kuweka mambo sawa kabla kurupushani hizi hazijasababisha madhara zaidi? Kulikoni hata viongozi wengine wa chama wameshindwa hata kuwaandikia viongozi wenzao barua kali za onyo na kuzikopi kila ngazi inayokubalika, kulalamikia yale wasiyoridhishwa nayo, badala yake wanaelezea dukuduku zao kwenye vyombo vya habari na hasa mitandao.
Mimi si shahidi wa kumtetea Zitto au Mkumbo mahali popote, lakini sioni kabisa faida ya kufanya haya. Kama kuna intelligensia ya CHADEMA (kama ipo) inayoweza kugundua mienendo yote ya wanachama wake kwanini wasiyapeleke hayo kwenye vikao na kuwaita hawa wenzetu na kuwaonya? Je kwa kuyaweka haya mitandaoni tunakisaidiaje chama chetu?
Ninaamini na ninapenda wengi waelewe hivyo, kwamba mtu awaye yote anayetoa siri za chama au za mtu mhimu ndani ya chama na kuziweka kwenye mitandao, kwa hakika huyo si mwanachadema. Hata kama taarifa hizi hutolewa na Mbowe au Slaa, basi hao ni lazima wawe ndiyo wasaliti namba moja wa chama kushinda hata wale wanaowaita wasaliti. Siamini kwamba mtu mwenye mapenzi ya kweli ya CHADEMA anaweza kuthubutu kuandika chochote kinachohusu chama kwenye mitandao, na akajinasibu kwamba anafanya hivyo kwa nia ya kukisaidia chama. Hili nalisema wazi pia kwa Lema, achilia mbali Mwigamba. Tufike mahali tujifunze kufanya siasa za kistaarabu. Kwa kuanza kuwaandika watu na kuwachafua kwenye vyombo vya habari hata kama wameshiriki kwa namna moja au nyingine katika huo tunaoamini ni usaliti ni kujaribu kutengeneza maadui wa chama. Jambo ambalo hatutafaidika nalo.
Niweke tu wazi kwamba nina imani haya hayafanywi na wanachadema bali ni wanaCCM wanafanya haya kwa nia yao ovu ya kuvuruga utengamano ulio ndani ya chama. Lakini imani yangu hii inafifishwa na ukimya wa uongozi wa juu wa chama. Tafadhari viongozi wetu wa chama, zishughulikieni tofauti hizi kabla hazijaleta madhara makubwa chamani.