Maoni yangu, mikopo elimu ya juu ifutwe

Maoni yangu, mikopo elimu ya juu ifutwe

LEVEL

Senior Member
Joined
Jul 4, 2013
Posts
195
Reaction score
51
Nimekua nikitafakari sana kuhusiana na hii mikopo inayotolewa kama msaada kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kwa kweli imesaidia watu wengi kutokana na wengi wetu kutoka katika familia za kipato cha chini na hivyo kushindwa kumudu gharama hizi kwa hili naipongeza serikali kwa mipango mizuri ya kuinua kiwango cha elimu.

Ila pindi mtu anapomaliza chuo huwa na deni kubwa ambalo bodi ya mkopo hukata kidogo dogo ili kuweza kurudisha pesa hizi na hapa madeni hutofautiana kulingana na kiwango cha mkopo alichopewa mhusika unakuta mtu unamaliza chuo una deni la hadi 12 mil, hata kabla ya ajira.

Maoni yangu ni kwamba, kama serikali wanao uwezo wa kutoa mikopo hii kwa wanachuo wengi kiasi hiki ni kwanini wasifute au kupunguza ada za vyuo ili watu wajisomeshe wenyewe na hizo pesa wanazotoa mikopo zikapelekwa vyuoni kujenga miundo mbinu pamoja na kuwalipa walimu na wafanyakazi wengine wa vyuo kwa sababu inauma sana mtu unapewa mkopo sawa ila mwisho wa siku unaanza tu kazi salary slip ya kwanza tu inakuja na deni la milioni kadhaa.

Pili, hizo hela wanazotoa mikopo nyingi zinapotea kwa mfano kuna watu wana disco, kufa, kuacha chuo nk. Sasa kuliko serikali kuendelea kupata hasara ya hizo ela zinazo potea kwa sababu mbalimbali ni bora watupunguzie tu ada tujisomeshe lakini vyuo watoe hela hizo kuviendesha wao.
 
ni haki yako kikatiba ila wa tz tulioweng tunaishi katika hali ya chini
 
Kukopesha ni business, hayo ni mawazo yako tu unayohisi lengo la serikali ni kutoa msaada.
Ungekuwa msaada usingekuwa na riba. Hiyo ni biashara ya serikali kama zilivyo zingine.
 
Kukopesha ni business, hayo ni mawazo yako tu unayohisi lengo la serikali ni kutoa msaada.
Ungekuwa msaada usingekuwa na riba. Hiyo ni biashara ya serikali kama zilivyo zingine.

du kama serikali imeamua kufanya biashara kwa wananchi wake hii ni kali
 
Kwani kuchukua mkopo ni LAZIMA?? Halafu kwanini msiwashauri "Makamanda Wakombozi" kina Mbowe wapeleke muswada bungeni wa KUTAKA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU WAPEWE RUZUKU Badala ya MIKOPO(Maana bodi ya mikopo ya Elimu ya juu upinzani hawakuitaka[kwa mujibu wa Hansard]).Au ninyi mnaona ni SAWA KWA MWANAFUNZI KUPEWA MKOPO NA VYAMA VYA SIASA VIPEWE RUZUKU Makamanda???
 
Mkopo ni muhmu kwa mwnafunz wa chuo,mkopo xio ada tu peke ake kwamba ikipunguzwa unaweza kujilipia...HV wakipunguza ada ili uweze kujilipia je hela ya chakula na malazi ambalo ndio tatzo LA watt weng wa kimaskin utawalipia ww???...you have 2think b4 kuropokwa
 
Kukopesha ni business, hayo ni mawazo yako tu unayohisi lengo la serikali ni kutoa msaada.
Ungekuwa msaada usingekuwa na riba. Hiyo ni biashara ya serikali kama zilivyo zingine.

nimekuelewa sanaaaaaaa
 
Mkopo ni muhmu kwa mwnafunz wa chuo,mkopo xio ada tu peke ake kwamba ikipunguzwa unaweza kujilipia...HV wakipunguza ada ili uweze kujilipia je hela ya chakula na malazi ambalo ndio tatzo LA watt weng wa kimaskin utawalipia ww???...you have 2think b4 kuropokwa

tatzo utakua umeandika post yako ukiwa una njaa ungekua unauelewa wa kutosha ungeelewa ninacho maanisha mm ila kwa kuwa una njaa umeona swala la msingi ni kula tu kwani swala la kula lipo degree tu secondary, diploma na masters hawali sio
 
Nakuomba ktk jina la Tanzania futa huu uzi wako uurudishe Mara bodi itakapokuwa imehitimisha hili zoezi linaloendelea.Na ikikupendeza usiurudishe kabisa PLEASE!
 
Back
Top Bottom