Maoni yangu kuhusu Majimbo

Maoni yangu kuhusu Majimbo

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,711
Reaction score
1,738
Ukweli usiopingika kuwa nchi yetu ingekuwa na majimbo au mikoa michache sasa hivi kiuchumi tungepiga hatua mno. CHADEMA wametoa maoni yao kimgawanyo wa majimbo kama ifuatavo:-
1. Nyanza Magharibi = Kagera, Geita na Shinyanga.
2. Nyanza Mashariki = Mwanza, Mara na Simiyu.
3. Ziwa Tanganyika = Kigoma, Katavi na Rukwa.
4. Kati = Dodoma, Tabora, Singida na Iringa.
5. Kaskazini = Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
6. Pwani ya Kaskazini = Tanga, sehemu za Pwani na sehemu za Morogoro.
7. Dar es Salaam.
8. Pwani ya Kusini = Mtwara, Lindi, wilaya za Mafia, Rufiji na Ulanga na
9. Nyanda za Juu = Njombe, Mbeya na Ruvuma.
Mie nawasifu sana CHADEMA kwa kianzio hicho ila mie ninawazo kuwa pasitumike majina yaliyopo kimikoa hivi sasa u-pwani na u-ziwani katika kutambulisha jimbo lolote na nimeona kama jimbo la Kati ni kubwa mno.
Maoni yangu ni kama ifuatavo:-
1. Mashariki = Pwani na Dar es Salaam.
2. Kati = Singida, Dodoma, Iringa (excluding wilaya za Makete, Ludewa na Njombe) na Morogoro (excluding wilaya ya Ulanga).
3. Magharibi = Shinyanga (excluding wilaya za Bariadi, Maswa and Meatu), Tabora, Kigoma na wilaya ya Mpanda,
4. Kaskazini = Kagera, Mwanza, Mara na wilaya za Bariadi, Maswa na Meatu.
5. Kaskazini Mashariki = Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
6. Kusini = Ruvuma, Mtwara, Lindi na wilaya za Ludewa na Ulanga na
7. Kusini Magharibi = Rukwa (excluding Mpanda), Mbeya na wilaya za Makete na Njombe.
Angalizo kimikoa nimetumia Atlasi ya mwaka 2005.
Wana JF inasomekaje hii.
 
Utawala wa majimbo utakuja ccm watakapoondoka madarakani
 
Utatuambiaje bila aibu kuwa kimikoa umetumia atlas ya mwaka 2005! Huna habari kuwa atlas hiyo ni outdated? Kuna mikoa kama Katavi, Simiyu, Njombe ....... Kwenye hiyo atlas yako inapatikana?????
 
Back
Top Bottom