Maoni yangu dhidi ya "Baadhi ya wananchi wahuni" wa Arusha kujaribu kuzuia wanahabari wa TBC

Maoni yako halafu iweje,kumbuka TBC ni TV ya taifa watu wanataka wapate habari bila chenga, kumbuka yaliyomkuta Marin Hassan pale Jangwani, ni sawa na yale yaliyotokea Cairo watu waliamua kutoka Tahrir square kwenda TV ya taifa(ya huko) kupinga yaliyokuwa yanaripotiwa juu ya kumpinga Mubarak, haya hayataishia Arusha
 
thibitisha kama hao ni wana CHADEMA! Huna maana Gamba wewe
 
Wanatangaza kufilisika lini na kuacha kutangaza, haina maana kwangu kabisa channel hiyo.
 
Inawezekana una nzuri lakn umefanya POOR Presentation kwa sababu inakuwaje uwaite wakazi wa Arusha ni wahuni wewe Mwandishi CcM? TBC mnadhararika namna mnavyo base upande mmoja wa CcM so unategemea nani avumilie ujinga wenu nyie TBC? watake radhi wana arusha kwa kuwadharau au huko hauna baba,uant,dada ako,mama ako,uncle? umeonesha dharau sana wewe kijana
 
Wewe kama unaanguka kwenye kundi la "Baadhi ya wananchi wahuni" basi hili ni saizi yako, linakuhusu siwezi kulifuta hata uje na panga.

mwanangu yani unadiliki kuniambia hvyo mimi babako,bas bwana kwani hata mamayako huwa ananiambia kuwa sikuhz kupewa vjisent na ccm umeanza zalau kumbe kweli wakati mama yako anamimba yako niliwaikuota unanitukana leo ndoto imekamilika jamani wakuza zaeni mi huyu mtoto kanishinda
 
Dotto mwanahabari ulijaribu kufuatilia au kujiuliza ni habari zipi haswa ambazo hao TBC walilalamikiwa kuhabarisha kwa kupotosha, je TV nyingine walitoa taarifa za namna gani? Kama wananchi wa Arusha ni wahuni kama unavyotaka tuamini huoni kuwa wangezuia TV zote? Unajua kwanza kuna vituo vya TV na waandishi wangapi waliripoti same taarifa na hawakulalamikiwa?
Hivi mfano mdogo, Marine Hassan anapotangaza kwenye TV ya serikali kwamaba mgombea wa chama fulani, au chama fulani hakitaingia madarakani wakati wa uchaguzi wewe ulilionaje hilo kama mwandishi wa habari makini? Mbona hukulalamika?

Acheni uandishi wa bahasha jamani.Ni jambo lililo wazi kabisa, waandishi uchwara wa TBC wako biased na lengo haswa ni kutafuta hizo nafasi za u DC, RC na ubunge wa kuteuliwa, ni njaa tu.Lakini tunawaambia wazi mnajiabisha!
 
CHADEMA ni nani? Unawezeje kujua huyu ni mfuasi wa chama fulani?
If I had my way TBC ningeifunga na kufanya eneo lake liwe kiwanja cha watoto kucheza. Wakati wa ajali ya Spice Islander TBC waliamua kuweza vipindi vya taarab! kama sio vyombo binafsi na mitandao kama ya jamii forums watu wasingepata habari.

Chaguzi ndogo zinanyika badala ya kujulisha watu nini kinaendelea TBC wanaweka sherehe za kitchen party! Na wakitoa habari imechakachuliwa. Kama unataka kujua nini hasa kimetokea mahali inabidi uangalie vyombo binafsi vya habari au mitandao! Na TBC inaendeshwa kwa kodi za hao hao unaowaita wahuni!
TBC ifutwe, tupate sehemu ya watoto kucheza.
 

Comments kama hizi zinatofauti gani na matusi ya Lema na Lusinde?
 
Hiyo ni haki kabisa maana inawakilisha hisia zangu kwa watu wenye tabia isiyofuata sheria na kanuni zilizowekwa. Watakuwa ni WAHUNI TU hakuna jina lingine la kuwatosha.

Sina sababu ya kutoamini kwamba wewe ndiye mhuni kuliko watu wa arusha.
Kwamba mnatoa taarifa za kupotosha halafu mnataka mheshimiwe?
Kumheshimu mwandishi wa habari asiyetambua nafasi yake katika jamii na asiyetambua thamani yake katika jamii ni zaidi ya upumbavu.
Umeshawahi kujiuliza kwani si ITV, STARTV, CHANNEL TEN ama MLIMANITV?
Nadhani kuanzia sasa mtajirekebisha, walichofanya watu wa arusha ni kuwaonya wahuni wa tbc muache uhuni wenu!
 
fulishness tbc endeleni na taarifa zenu za magamba na madevu hata hamna haya yani hamna mvuto hata kidogo. Ndio maana wenye akili waacha kazi ya kuwatumikia watu fulani badala ya watanzania. Mtoa mada shame upon you
 
kuweni wavumilivu kama wenzenu wanvyokuwa wavumilivu mnavyotumia vyombo vyenu vya habari kuwachafua,Tatizo lenu nyinyi mmezoea habari za CHADEMA YAUTEKA MJI WA ARUSHA. TBC WAKO SAHIHI KABISA
 
Tbc kama chombo cha Taifa yapasa isipendelee ktk kutoa habari, msipende baadhi ya makundi ya wachukie. Kwa kweli hata mimi siku hizi siipendi tbc kwa upande wa habari! Tofauti na kipindi cha tido.
 

I did not expect positive reaction hasa kama wanatoa watu waliojificha nyuma ya avatars...lazima mjue kuwa CCM inawachama zaidi ya milioni tano, hatuwezi kuwapuuza eti kwa sababu watu fulani wanajihisi wako sahihi kupita wengine. Wewe umenithibitishia kuwa "Mhuni mmoja wapo"
 
 
Hao watu si wajinga,uchaguzi Arumeru mliandika barua kuomba ulinzi, kama mligomewa ya nini kwenda? Muwe na ulinzi wa green guards kote. TBC ni Taarifa na Burudani kwa Ccm

Kama ni kweli walilindwa na Green Guard basi wanapoteza sifa ya kuwa chombo huru cha habari. Tena cha Taifa. Lazima wawe makini. Walimuacha Tido sasa itawatokea puani.
 
Ungeandika hivi hivi pia kuhusu yanayofanywa na CCM kwa wale wasiowaunga mkono pia tungekuona una busara na akili zinazofanya kazi.
Nyie mnapofanya upumbavu huwa siyo uhuni?

Huyu ni mpuuzi tu aliyeweka uchafu wake hapa,anaonakwa mtazamo wake tungefikisha ujumbe kwa namna gan? hiyo ndiyo njia sahihi ya kufikisha ujumbe ndiyo maana hata yeye ambaye ni Gamba ujumbe umempata na umemuumiza! Nafikiri huyu ni mjinga fulani anayefikiri kile akiwazacho ndicho kila mtu mwenye akili timamu akiwazacho
 

Sijakusoma kabisa mkuu, unataka kuniambia siruhusiwe kutoa maoni yangu? Kama hakuna "formal complaits" kutoka uongozi wa CDM basi madai yenu mengi ni ya kishabiki. Na kama hamridhishwi na namna TBC inavyoripoti habari basi njia ya kuwazuia kabisa si sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…