Maoni ya Tendwa Kuhusu Uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni ya Tendwa Kuhusu Uchaguzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kichuguu, Dec 15, 2010.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Dec 15, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280

  Huyu jamaa ameongea jambo moja zuri kuhusu katiba mpya. Ila melezo yake kuhusiana na lowa turnout si ya ukweli unless aseme kuwa wanachi wa leo ni mbumbu kuliko wa miaka iliyopita, in which case atakuwa ana-imply kuwa uongozi wa sasa umewapumbaza sana raia kiasi cha kutokufahamua hata umuhimu wa kupiga kura. Tangu nchi hii inapata uhuru, haijawahi kuwa na low turnout, na wakati huo ndipo tulikuwa na umma wa wasiokuwa na elimu yoyote. Leo hii kila kijana anapata elimu ya msingi, na hiyo ingemwezesha kabisa kujua umuhimu wa kupiga kura. Sehemu zote ambazo CHADEMA imeshinda, ni kwa sababu vijana walilirinda kura kwa karibu sana. Imani yangu ni kuwa pamoja na vitisho vilivyotolewa na vyombo vya usalama siku chache kabla ya uchaguzi, na njia makusudi zilizofanywa na Tume kuvuruga daftari la wapiga kura ili vijana wasipige kura, bado kuna kura nyingi sana zilizopigwa, ila tume haikuzitangaza zote kusudi ionekane kuwa wanapenzi wa CCM pamoja na uchache wao, walipga kura za kuipa CCM ushindi wakati wale wapenzi wa vyama vya upinzani pamoja na wingi wao hawakupiga kura za kutosha kuvipa vyama vyao ushindi.


  Ni afadhali jamaa hawa wasiongelee tena swala la upigaji kura wa Oktoba 2010 kwa vile wote walishirikiana kuhakikisha CCM inashinda kwa njia yoyote hata bila kupigiwa kura
   
Loading...