Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,068
- 151,315
TUNA UWEZO WA KUJITEGEMEA LAKINI SI SASA.
Uamuzi wa M.C.C umeleta kelele nyingi sana mitandaoni na vijiweni.Ni kelele kwa sababu mihemko inayotokana na itikadi za kisiasa na mahaba ya wanachama imetawala kuliko hoja.
TUPO TAYARI KUJITEGEMEA?
Nchi kujitegemea sio jambo LA kulala na kuamka.Hatuwezi kujitgemea bila kujiandaa kujitegmea.
FIKRA NA UTAMADUNI TEGEMEZI
Tunaimba kujitegemea huku tunapaka "mkorogo" usoni? Unaimba kujitegemea na wigi kichwani hizi fikra za "weupe ni uzuri" ni ushahidi mwingine kwamba BADO HATUKUJIANDAA KUJITEGEMEA.
VIWANDA VYETU!
Tulipopata Uhuru viwanda vyetu vilikua vikichangia 3.5% la pato la taifa(G.D.P) huku vikitoa 9% ya ajira zote za wakati huo.
Miaka 37 baadae (2008) viwanda hivi vinatoa chini ya 20% ya ajira zote zinazopatikana nchini.
Viwanda ni Eneo muhimu na kubwa lenye kutoa ajira
Kwa Nchi "inayowaza" kujietegeme.KWA kiwango hiki cha ajira ni wazi HATUNA VIWANDA VYENYE UWEZO WA KTUFANYA TUJITEGEME.Kusema tupo
tupo tayri kujitgemea ni kujidanganya.
Nchi inayoshindwa hata kufanya sensa ya viwanda haiwezi kua ni nchi inayoamini kwenye viwanda.Tangu tupate huru sensa ya viwanda imwfanyika Mara 4 tu.
Mwaka 1961,1978,1989 na baada ya miaka 24(ilitarajiwa ifanyike 2015 sina uhakika kama imefanyika).Utafanyaje sensa wakati una viwanda ambavyo unaweza kutumia "bodaboda" kuzunguka na ukavimaliza vyote kuvihesabu?
TUNA AKIBA YA PESA YA KUTOSHA?
Tamko la Sera ya fedha lililotolewa na benk kuu(B.O.T) June 2015 linasema mpak mwezi april 2015 tulikua na akiba ya fedha za kigeni dola za kimarekani million 4.043 ambazo zinatosha kuagiza bidhaa na huduma toka nje kwa miez 3.9(robo ya mwaka ni miezi 4..haijafika)
Lakini deni la taifa (mpaka april 2015)ni dola za kimarekani million 14,762.7( Zaidi ya Mara 3 ya akiba Yetu)
Nchi kudaiwa ni kawaida lakini unapokua na deni kubwa kuliko uwezo WA kilipwa kwenye deni lenye riba tegemea kukua KWA deni hilo kutokana na malimbikizo ya riba.Hizi sio dalili za Nchi iliyotayari kujtegemea.
TUTAJITEGEMEA NA AFYA MBOVU?
hatuna viwanda vya kutoa ajira lakini hatuna afya murua ya kujiajili sisi wenyewe.Afya mbovu husababisha hupotevu wa nguvu kazi ya taifa kutokana na vifo.NI kuanzia huduma za afya mahospitalinj mpka mazingira ya kiafya ya MTU mmoja mmoja
NI hapa kwetu inakadiriwa Zaidi ya wakina mama wajawazito 7.900 sawa na vifo 22 kila siku (Gazeti la mwanchi 1/23/2015)
Jumla ya watoto 40,000 wenye umri chini ya mwezi mmoja hufa na TANZANIA ni Nchi ya 11 duniani miongoni mwa Nchi zinazoongoza KWA vifo vya watoto(UNICEF 17/Nov/2014)
Jumla ya watoto 600,000 wenye umri chini ya miaka 5 wanakisiwa kufariki KWA kipindi cha miaka kumi iliyopita kutokana na ugonjwa WA UTAPIAMLO.
Idadi ya vifo hapo juu unaweza kulinganisha na idadi ya watu waliokufa Rwanda kwenye mauaji ya kimbari mwaka 1994.Hii ni sababu nyingine inayoifanya TANZANIA iwe miongoni mwa Nchi zinazoongoza DUNIANI kua na watu wenye huzuni(Msiba haufurahishi).Idadi hii kubwa ya vifo ni sababu nyingine inayothibisha HUU SI WAKATI WETU KUANZA KUJITEGEMEA.Mgonjwa hana uwezo WA kujitegemea.
Kuna taarifa juzi serikali imepokea billion 116 za Japan za nini sasa kama tupo tayari KUJITEGEMEA.
AFRIKA!!AFRIKA,,TUACHE UWONGO
Kuwaamini viongozi WA kiafrika yataka moyo.NI sawa sawa na kumuamini dakatari akutibu wakati mkewe ni muuza majeneza.
Wengi wanajua "kuigiza " sisi inapopanda bei ya mchele,sukari,kodi za nyumba tunaoumia ni sisi tunaovaa kofia na khanga za chama (nguvu zaidi na kasi zaidi,hapa kazi tu)tulizopewa wakati wa uchaguzi

Bajet Yetu mwaka wa fedha uliopita ilikua trillion 22.Wengi tunapata matumaini ya kwamba tupo tayari kujitegemea kwakua T.R.A wametuambia mwez February walikusanya triliom 1.4(izidishe Mara 12 ).inakuja trillion 22+ ..? Amin mafanikio haya ya T.R.A yaliletwa na upya WA serikali na hofu tu na si mfumo Mpya WA ukusanyaji kodi.

Wakati wanasema tupo tayari kujitegemea bado elimu yetu inatoa wasomi legelege, bado maji safi ni shida,umeme haujawa wa uhakika,viwanda hatuna,usafiri WA reli WA kubahatisha ,wagonjwa wanalala chini.
Tujitegemee sasa kwa kilimo hiki cha minjingu?na umeme huu usio na uhakika?NA barabara hizihizi za "shukeni tuvuke kwanza?" acheni utani nchi kujitegemea si sawa NA NDOA YA MKEKA
TUPO TAYARI KUJITEGEMEA BILA MAJI?
Kwa mujibu WA utafiti uliofanya na TWAWEZA mpka mwaka juzi 2014 ni asilimia 53% tu ya WATANZANIA wanoishi mjini wenye uwezo WA kupata maji safi na Salama huku kijijini ni asilimia 44% wenye uwezo.Kama bado maji ni changamoto tusidanganyane kuhusu KUJITEGEMEA KWA sasa
Hatuwezi KUJITEGEMEA muda huu kama bado hatujarekebisha sheria zetu zinazoruhusu 2.3% ya pato la serikali kupotea kupitia misamaha ya kodi.Kwa mwaka 2009/2010 peke yake serikali ilikosa shilingi billion 695 zilizotolewa kama misamaha ya kodi.
Tukiri TULIIBAKA DEMOKRASIA ZANZIBAR kuliko kutunisha kujiliwaza na mashairi ya sungura"SIZITAKI MBICHI HIZI"Ingelikua tupo tayri tungejitoa wenyewe kabla ya "kufukuzwa"
Source:Joss Nassari facebook page