Sungurampole
JF-Expert Member
- Nov 17, 2007
- 984
- 205
Katika uzi juu ya mada ya maoni juu ya katiba mpya(12.2.2012) for curiosity nilipoyapitia nilipata haya wewe unasemaje lako liko hapa?
Najua ni ngumu lakini fikiri, chekecha, weka lako moja.
Najua ni ngumu lakini fikiri, chekecha, weka lako moja.
- Katiba yenye zero tolerance kwa ufisadi!!!
- Ukikamatwa unatoa au kupokea rushwa, kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya basi adhabu yake ni kunyongwa
- Azimio la arusha liingie kwa katiba
- Rais asiwe mwanasiasa
- Vyama vya siasa visidi vitatu -Wengine wawe wagombea binafsi.
- Vyama vipgiwe kura vitavyopata chini ya idadi fulani ya kura vifutiwa usajili hadi vibaki vitatu kama sio viwili
- Tutulieni kwanza tupigwe elimu ya uraia...
- Iwe marufuku kuuza mali ya umma
- Kupunguza madaraka ya RAIS
- Kurudisha kwa Tanganyika
- Teuzi za rais zote zithibitishwe na bunge kundoa nepotism
- Kusiwe na wakuu wa wilaya, wanaongeza mzigo wa gharama kwa serikali kuwalipa mishahara na marupurupu, wakurugenzi watosha.
- Mawaziri wasitokane na wabunge bali professionals
- Mgombea binafsi ni muhumu sana, kwa ngazi zote za uongozi wa kisiasa
- Muungano wa serikali moja
- Wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya wachaguliwe na wananchi kwa njia ya Kura
- Urais wa kifalme uondolewe
- Safari za rais za nje ya nchi ziwekwe kikomo- sizidi safari 20 kwa mwaka.
- Shule za secondary zote za kata zisizokuwa na waalimu wasiozidi 5 zifungwa kuepuka failures za aibu kila mwaka.
- Usalama wa taifa, majukumu yake yaelekezwe kwa taifa kweli na isiwe katika misingi ya kulinda viongozi wabovu na kufumbia maovu
- Ubunge uwe miaka 10 tu (vipindi viwili tu kama ilivyo uraisi)