Maoni ya Katiba Mpya-Kilio cha Zanzibar Chasikika!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Hatimaye kilio cha Wanzanzibar kusikilizwa maoni yao kwenye ukusanyaji maoni ya marekebisho katiba ya Tanzania kama sehemu inayojitegemea, kimesikilizwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, Mhe Pindi Chana, ametangaza rasmi leo asubuhi kupitia kipindi cha Jambo Tanzania.
Update.
Pindi Chana amesema Public Hearing ya Dar es Salaam itafanyika kesho sikukuu ya Karume Day, katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 3 asubuhi. Public Hearing ya Zanzibar, itafanyika kesho mjini Zanzibar katika ukumbi ambao haujajulikana.

Wakati huo huo, Ofisi ya Bunge, imetoa tangazo kwenye magazeti ya leo kuwaalika wadau na wananchi kuja kutoa maoni yao juu ya Muswada huu wa Mapitio ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011. Tangazo hili la Bunge, linaonyesha ukusanyaji wa maoni hayo utafanyika kwa siku mbili, Tarehe 7 na 8 katika kumbi za Karimjee (Dar es Salaam) na Pius Msekwa (Dodoma). Huu ni uthibitisho, uamuzi wa kukusanya maoni ya Zanzibar, umefanyika jana usiku na leo asubuhi kutangazwa na Mhe. Pindi Chana.
Hii ni zimamoto!.
 
Back
Top Bottom