BAKOI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2016
- 1,211
- 2,328
Anaandika Dr Onesmo Mhadhiri Kitivo cha sheria UDSM.
Swala la bei ya umeme ni siasa uchwara. Kuna wakati wanasiasa wanakuwa kama watoto, eti wanasema bei ya umeme haitapanda ili tuone kuwa serikali inawatetea wananchi kitu ambacho si kweli.
Utaratibu wa kupandisha umeme upo hivi. TANESCO inaandika mapendekezo na sababu za kutaka kupandisha umeme. Mapendekezo hayo yanapelekwa EWURA.
Ewura inafanya inquiry kwa kushirikisha wadau wote wakiwemo serikali, vyama vya walaji, wafanyabiashara nk.
Baada ya hapo inatumia wataalam wao kuangalia kama kuna sababu za kukubali ombi la kupandisha bei kama lilivyo au wanaweza kukubali kiasi fulani au wakakataa.
Baada ya kutoa maamuzi kama kuna mtu hajaridhika ikiwemo serikali inatakiwa kukata rufaa Fair Competition Tribunal. Na wangeweza kuomba temporary injunction kuzuia kutumika bei mpya.
Kwa hiyo si kweli kwamba serikali haijaona hiyo writing ya sababu za kupandisha umeme na Waziri hana mamlaka ya kuzuia maamuzi ya EWURA.
Mimi kama mwananchi ninafurahia umeme kutopanda lakini tusipofuata utaratibu wa sheria tunazidumaza taasisi zilizopewa mamlaka ya kutoa maamuzi.
Utawala wa sheria ni muhimu sana katika ustawi wa nchi. Ni maoni yangu tu.
Happy new year.