MAONI: Katiba, Sheria na kanuni za nchi yetu zina mapungufu au watu waliopo ndo wana mapungufu

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
. Ndani ya katiba ile kulikuwa na mambo mengi sana muhimu ambayo endapo yangelifuatwa nadhani hili la mkuu wa mkoa lingekuwa lilisha patiwa ufumbuzi mapema sana tena kwa tuhuma za awali kabisa bila kusubiri vioja zaid na kusinge kuwa na haja ya kusubiri mtu mmoja ajisikie kutoa maamuzi au laa!

. Kulikuwa na haja ya kuipitia na kuzipa mamlaka za uwajibisha kuwa na nguvu kuliko rais hata pale wapendwa wake wanapo kiuka taratibu ndio maana TAMISEMI najua wanayaona haya kuwa hayapo katika utaratibu lakin hawana namna ya kufanya na hili lilielezwa vyema kwenye rasimu ile lakin baadhi ya wabunge wa CCM kwa kuto kujua MASKINI wakapelekwa pelekwa tu na kuungana kwa umoja mtakatifu.wakasahau katiba ni ya taifa lakin uongozi wao utapita na taifa litabaki tu, baadhi yao sijui niseme hawakuifikiria kesho! Waliijali njaa ya leo pekee

. CCM na baadhi wabunge wake ndio chanzo cha kila kitu kinacho enda hovyo hovyo katika nchi hii , nitawalaumu wabuge wa CCM hadi siku ya mwisho kwa kuungana kukataa kitu kilicho kuwa na faida kwa taifa zaid kuliko mtu mmoja mmoja na walio wengi walikataa bila hata kuisoma rasimu ya warioba bali waliungana na wenzao walio ikataa bila kujua kilichomo ndani na kama kuna maisha baada ya hapo

. Naamin sasa wameanza kuona umuhimu wa katiba itakayo jenga misingi ya kuto kumpa mtu mmoja mamlaka na nguvu zaid ya chombo chochote, na ukiisoma katiba yetu vizuri utajua kuwa mtu mmoja anakuwa na nguvu na mamlaka kuliko mihimili yote mitatu maana anakuwa na maamuzi juu ya mihimili hiyo nini zifanye na nini aid fanye maana haiwezekani kumuwajibisha bosi wako aliye kupa madaraka na hiyo ni katiba si yeye.

. Bali kuwe na vyombo vinavyo weza kuwajibisha hata aliye juu na asiwe na mamlaka wala nguvu ya kukataa au kupinga kwa vyovyote vile maamuzi ya walio muwajibisha sababu kama katiba iko vizuri atakosa nguvu na support ya kukataa lakin si kwa katiba hii iliyopo.

. Maana kwa katiba yetu ya sasa hata kama wabunge wakiungana kupiga kura kuto kuwa na iman na rais bado rais ana uwezo wa kukataa maamuzi ya bunge hata kama ni kinyume cha sheria kukataa, na hii ni kwa sabaubu tu ana mamlaka makubwa na vyombo vya dola , na vyombo vya dola ndivyo vinavyo iendesha nchi indirectly, hivyo vyombo vingine vipo tu kisheria lakin mwisho wa kilakitu ni vyombo vya dola nikimaanisha majeshi and co.vinginevyo mataifa jirani yaingilie kati kitu ambacho kwa nchi za AFRICA MASHARIKI si rahisi maana mambo mengi yanafanywa kinyume na ukiukwaji mkubwa wa katiba za nchi zao na haki za binadamu na nchi wanachama na hawawajibishani katu.

WABUNGE ! WABUNGE !WABUNGE NDIO KILIO CHANGU KIKUU MAANA NDIO WATUNGA SHERIA ZINAZO IENDESHA NCHI HII.
 
Tumekuwa tukihitaji katiba ya nchi iliyo bora kwa nchi yetu, lakini je tatizo ni katiba na sheria peke yake ndo mbovu?

Sio mtaalamu wa katiba na sheria lakini hata ile katiba ya Warioba nayo haikukidhi haja ya mazingira yetu ya kisiasa.

Mf. 1:Tunajinasibu kuwa tuna mihimili mitatu inayojitegemea ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Katika mihimili yote hiyo, inasemwa mhimili mmoja hauingilii mwingine. Mimi naona hii ni nadharia zaidi kuliko uhalisia. Rais ana uteuzi Serikalini, Bungeni na kwenye Mahakama. Hapo hiyo mihimili tunasema inajitegemea kwa mtindo gani.

Bunge lina viongozi wao ambao si wabunge, kwanini katibu wa bunge ateuliwe na Rais, ipi mantiki yake na huyo mtu akiteuliwa kutoka kwa watendaji waandamizi wa bunge kuna athari gani. Hilo swali wajibu wanaona ni sahihi Rais ateue katibu wa bunge.

2:Uteuzi wa majaji na jaji mkuu. Hii ni nafasi nyeti sana Serikalini na ni mhimili tunaouita unajitegemea kinadharia. Hawa majaji kwanini wanateuliwa na Rais, mantiki yake ni ipi na je wakijiteua wenyewe kwa kuomba hiyo nafasi itatokea athari gani kwa nchi. Je, Rais anapoteua jaji au jaji mkuu kuna sifa za lazima aziangalie na asipoangalia ataulizwa kwanini umemteua Y wakati X ana vigezo vingi kuliko Y? Au mapenzi ya kiongozi tu yanateua mtu? Kwanini mhimili mmoja uteue viongozi wa mhimili mwingine?

Kuna suala la katiba ya sasa na hata ya Warioba, haitoi uwezekano wa Rais kushtakiwa akiwa madarakani au hata baada ya kutoka madarakani. Lakini katiba hiyo hiyo haitoi nini cha kufanya iwapo Rais atakiuka katiba.Kwa siasa za Africa ni vigumu sana Rais kutolewa madarakani na wabunge,ni ngumu na haiwezi kutokea labda kama wabunge wa upinzani ni wengi kuliko wale kutoka chama tawala. Tunajua siasa zetu zinaangalia sana chama zaidi kuliko nchi, kwanini waandaa katiba walishindwa kuliona hilo.

Rais kuwa na mamlaka makubwa sana hata katika katiba ya Warioba. Anateua watendaji wengi bila sababu technical reason.

Pia, katiba ingetoa mmojawapo kati ya makamu wa Rais au waziri mkuu. Nchi zilizo nyingi kama makamu wa Rais yupo basi Waziri mkuu hayupo na kinyume chake, sababu zipi Tanzania tuwe na makamu wa Rais na Waziri mkuu kwa pamoja?

Kuna suala la ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao. Hapa police ndo naowazungumzia zaidi. Hawa police wamekuwa wakitumika isivyo na hii imesababishwa na kufanya kazi kwa maagizo kutoka kwa watendaji wengine ambao hata si askari.
Msingi wa usalama na ulinzi ni kiwa police wenyewe wagundue makosa wao wenyewe na sio kuonyeshewa makosa. Hii ingekuwa katika sheria zetu, kusiwe na kiongozi wa kutoa maelekezo kwa askari. Nini msingi wa mwanasiasa kuelekeza askari kukamata mtu, ina maana police hawajui wajibu wao.
Hawa police nao wasingekuwa na kiongozi wa wa kitaifa. Kwani nini majukimu yao hawa viongozi wa kitaifa. Reform ya jeshi letu pendwa inahitajika. Kila kiongozi awe na maamuzi ya eneo lake hii italeta ubunifu na uwajibikaji zaidi kazini.

Pia, serikali za majimbo sijui ina kasoro gani sana kuliko huu mfumo tunaotumia. Naweza kuorodhesha faida zake chache:
A)Matatizo hayawezi kufanana kote nchini, mf. ujenzi holela, maji, kilimo na ardhi,ajira kama ilivyo sasa.

B)Ubunifu na ushindani wa kimaendeleo katika majimbo.

C)Maamuzi yatakuwa ya haraka na ufuatiliaji wa shughhuli za kimaendeleo utakuwa ni wa makini zaidi.

D)Tunaweza kupata viongozi bora wa kitaifa kwa kuangalia maendeleo aliyoyapata kutoka uongozi wa jimbo aliloliongoza iwapo atatogombea Urais akitokea Ugavana/senetor.
 
Back
Top Bottom