kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 753
Wana bodi,
Kwanza nitoe pongezi kwa Serikali kwa ujenzi wa lile daraja la Nyerere, yaani limekuwa msaada mkubwa kama kiunganishi kwa wakazi wa kigamboni lakini pia ni kivutio kikubwa kutokana na miundombinu yake ilivyojengwa kwa ustadi na ubunifu mkubwa. Binafsi ule muundo nilizoea kuona kwenye TV tu kwenye nchi za huko ughaibuni.
Nimekuwa nimtumiaji mkubwa wa lile daraja licha ya ghalama ya Tsh. 2000 ninayolipia kila nikivuka lile daraja ila huwa na lipiza kwa kukodolea macho maeneo yote ya daraja hilo ili kupunguza maumivu ya sh. 2000 yangu. Na wakati mwingine huwa natembea hata speed ya 08kph huku nikiwashangaa wale wanaopita kwa mwendo mkubwa hadi wanakamatwa na wale trafick wenye tochi pale darajani na kupigwa faini ya elfu 3o/= hivi hawaoni kama shilingi elfu 2 ninayoitumia mimi kushangalia pale kwa sasa ni kubwa tofauti na ile buku mbili ya miaka ya nyuma?.
Licha ya ujenzi kuwa mzuri na unaovutia ila kuna sehemu kidogo nimeiona haiko sawa, hivyo ningeomba mamlaka zinazohusika kulifanyia kazi.
Yale maandishi makubwa pale juu ya zile gates yanapofanyika malipo yanayosomeka "DARAJA LA MWL NYERERE" hayajakaa sawa hasa upande yalikogeukia. Kwani yamewekwa mbele kabisa tena upande wa kigamboni baada ya kulivuka daraja hivyo kuleta mkanganyiko kwa watumiaji wageni kwani unaweza sema labda baada ya kuvuka zile gate kuna daraja la Nyerere mbele ake.
Mapendekezo: Ni vizuri yale maandishi yakageuziwa upande wa kigamboni ili mtumiaji ayasome kabla hajavuka daraja au kama lengo yasomwe na wanaovuka kuelekea kigamboni basi yawepo huku mwanzo kwenye zile njia panda za bandarini. Kwani kwa vile yalivokaa yataleta mkanganyiko kwa watumiaji wageni na wenye uelewa mkubwa.
Kwa wengi huku mitaani tunalitambua kama daraja la kigamboni na ukianza kuvuka unajua unavuka daraja la kigamboni ila baada ya kuvuka kuelekea kwenye zile gate mara ghafla unaona juu maandishi yanayokwambia DARAJA LA MWL. NYERERE kwa hiyo unaweza sema baada ya kulipia unaelekea vuka tena daraja la mwl. Nyerere.
Nawasilisha,